Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Uliishawahi kuusikia uchawi au ushirikina huu?

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Mwanzoni wakati nilipokuwa mtoto mdogo nilikuwa siamini kabisa haya mambo lakini kadiri nilivyokuwa nakuwa ndio nikaanza kufahamu kuwa kweli uchawi upo, Na mtu akiamua kukuharibia au kukuchafua ndio imeisha hiyoo..uliishawahi kukutana Na mtu ambae Kila janga lazima yumo tena kwa babati mbaya..

Basi kuna ushirikina mmoja upo huko Kagera wanautumia sana wahaya , kwa kirugha unaitwa "nyaamazi" yaani mpakwa mavi au kitu chochote chenye harufu mbaya, uchawi huu mshirikina au mchawi anaetaka kukuharibia uwe ni mtu wa mikosi mwanzo mwisho, Huwa anategeshea Na kukuibia Ile nguo unayoipenda sana kuivaa unaweza kuwa ni tisheti au suruali,..ataipeleka kwa mganga Na kuipaka huo uchawi unaoitwa "nyaamazi" Na baada ya hapo uirudisha kwa kificho Bila ya wewe kufahamu au kujuwa.. mchezo unaanza pale siku utakapoivaa au kuichanganya Na nguo nyingine kama sio mtu wa ibada sana lazima utaanza kuona rangi zote .

Kama ni mtumishi wa ofisi flani Basi utaanza kuona mabadiriko wafanyakazi wenzako wataanza kuku kataa, bosi wako anakuona kama kero tu, jamii inayokuzunguka imani yao kwako inapungua, ikitokea tatizo Basi wanaanza Na wewe, unakuwa huaminiki Na wala hupendeki Na yeyote, Kila unachokifanya kinaonekana ni hovyo tu, hata ufanye jambo zuri vipi...haya nimeyafahamu baada ya kutembea, elewa Neno KUTEMBEA..

uchawi upo hasa huku Africa (shit hole countries) tujikinge kama ni mtu wa ibada Basi sali sana, kama ni mtu wa ndumba Basi oga sana....
 
Huwa namshangaa sana mtu anaesema uchawi haupo😀😀😀 Nina imani yanakuwa hayajamkuta.
Mkuu huwezi amini yameshanikuta sana haya majanga tena kwa kusomewa dua tu. Mtu unatapika nywele na viini vya njano kama mayai, kubwa kuliko 1 month ago tena ilikuwa ni kama incident tu Boxer yangu imebanwa kufuri na t-shirt yangu kama miaka 10 iliyopita ilifukuliwa. Imagine 😅
 
Uchawi upo mkuu, kuna mwingine nimeukuta daressalam hasa mitaa ya uswahilini mtu anaoga madawa ya kuondoa nuksi mwilini mwake halafu yale maji anayojisuuzia mwilini anayamwaga kwenye njia ambayo watu wanapita hasa njia za vichochoroni,..ebwanaee nyote mtakaopita njia hiyo mapema hasa asubuhi inakuwa imeisha hiyoo yaani moja itakuwa haikai wala mbili haikai...ukija kugundua muda umeenda
 
Attachments

  • FB_IMG_1717598792712.jpg
    FB_IMG_1717598792712.jpg
    46.4 KB · Views: 13
Uchawi upo mkuu, kuna mwingine nimeukuta daressalam hasa mitaa ya uswahilini mtu anaoga madawa ya kuondoa nuksi mwilini mwake halafu yale maji anayojisuuzia mwilini anayamwaga kwenye njia ambayo watu wanapita hasa njia za vichochoroni,..ebwanaee nyote mtakaopita njia hiyo mapema hasa asubuhi inakuwa imeisha hiyoo yaani moja itakuwa haikai wala mbili haikai...ukija kugundua muda umeenda
Uswahilin kuna mambo sana mkuu. Mm niliwh kukaa mazibgira flan hiv wamakonde kibao. Nilisaga meno, hali si hali. Hupati hata mia wiki nzima. Ilifika kipindi natoka pale kwenda Kunduchi Mtongan nd napigiwa na kupata sim za hela. Ilifika kipindi unapogiwa sim ya hela ukiwa kunduchi ukirud home tu ile dili lazim ipinde 😁
 
Mkuu katika pita pita yako umehai kutana na mafundi wa ukweli? Maana wengi hapa mjini matapeli sana, eti fundi anavaa cheni na ana account insta!
Wapo Ila hawapo mjini kwa asilimia kubwa..waliopo humu mjini wengi wao ni mataperi Na wafanyabiashara.yaani wanatumia matatizo ya watu kama fursa
 
Kuwapata wale konki haswa ni kimbembe
Mpaka kwa connection sana , kuna mmoja yupo huko kanda ya ziwa siku nikiamka Na mood nzuri nitawapa connection yake...moja ya jambo alilolifanya ni kumtoa mtu gerezani aliekuwa Na kesi nzito.....hivi anafahamu ilikuwaje?......ndugu wa mfungwa walienda kwa Yule mtaalamu, mtaalamu akawaambia nunueni nguo mpya halafu mniletee hapa, Ile nguo ikanunuliwa Na ikapelekwa kwa mtaalamu, mtaalamu akaifanyia mambo flani flani halafu akawaambia wale ndugu wa mfungwa wampelekee ndugu huko gerezani, jamaa akawa anaivaa usiku Ile nguo haikupita hata wiki moja ikitokea" nole" Na jamaa akaachiwa huru
 
Wataalamu wapo mkuu ila mpk umpate wa kwel inachukua gharama na muda pia na wapo mbali sana c hawa wa Facebook
 
Back
Top Bottom