Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Ahsante sana mkuu, huu ni mwaka wa 4 tangu nikumbane na hiyo hali nishaachiwa madhara hasa upande wa miguu kuwa stable, baadhi ya vidole vya miguuni haviko sawa kabisa
Mi uwa nikiwaza sana,chini kidogo ya paji la uso uwa kunakua ganzi kama vile kuna kitu kimeganda, mpaka niwekepo kitu cha baridi ndo napata nafuu kidogo
 
Hiyo 'aya' ya mwisho imenifurahisha Sana.......😂😂😂😂
 
Ndio hali niliyonayo sasa
 
Mshukuru Mungu kwa kukupitisha katika kipindi hiki. Kumbuka kuwa kila kitu ni temporary na sio permanent. Ila utajifunza mambo kadhaa ambayo yatakusaidia sana mbeleni.
1. Utawajua marafiki wa kweli
2. Utamfahamu mwenza wako vizuri katika kipindi hiki
3. Utajifunza discipline ya matumizi ya Fedha
4. Utagundua unahitaji a very strong supporting system wakati mwingine utakapoanguka tena
5. Imani yako itazidi sana ( Aidha kwa Muumba au kwa Waganga )

Muhimu ni kutokuta tamaa na kila siku kuendelea kuchungulia fursa mpya.
 
Natamani katika maisha kila mtu apitie hicho kipindi. Ni kipindi utawajua rafiki wa kweli, ndugu wa kweli, utamjua vizuri mpenzi wako (mkeo).
Utafahamu kuwa unaweza kuishi kwa kula mlo mmoja au 2 kwa siku.
Utafahamu kuwa unaweza kutembea kwa miguu yako na ukafanikisha mambo mengi.
Utafahamu kuwa unaweza kuishi uswahilini kodi sh 50K kwa mwezi na maisha yakaenda.
Utajifunza kujibana kifedha ili ufanikishe mambo kadhaa.

Unayotakiwa kuyafanya:
1. Usikate tamaa
2. Wewe una thamani na uwezo mkubwa tu sema Mungu hajaamua bado.
3. Siku utakapotoka katika hali hiyo usiwasahau waliokushika mikono kukuvusha.
4. Usirudie makosa yaliyokuweka kwenye vikwazo.
5. Tafuta chanzo kingine cha mapato hata kiduka kidogo tu. Kitakusaidia sana kujikwamua.

Mimi kuna kipindi nilikaa mwaka mzima. Japo kwa kipindi cha miezi 8 sikuwa natafuta kazi nilikua vizuri tu, miezi 4 ya mwisho nilifilisika ndio nikajua rangi ya upepo.

Baada ya miaka mitano, nikaja kukaa miezi 7 bila kazi tena. Ila week mambo yalivyofunguka nilikua na kampuni 2 mkononi zote zinanihitaji, nikachagua niliyoona bora zaidi.

Na wakati napeleka guarantor's forms nipewe mkataba, kampuni nyingine wakanipigia niende tupange mshahara na makubaliano mengine. Nikawambia ntakuja kesho yake.

Na mchana wake saa 8 na nusu nilikua na interview na kampuni nyingine.

Nothing is permanent.
God above all.
 
[emoji1666]
 
Hustle
 
Nina mwaka wa14 kazini, nikifukuzwa leo hata mwezi hauishi naanza kusota
 
We acha tu,
kipindi inafika maji unayanywa na kusifia matamu kishenzi. wenzio ni ma senior sakta hiyo
 
Hayo mambo yasikie kwa jirani.
Nilijifunza kumtumainia Mungu pekee...the rest yamebaki story tu kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…