Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Uza simu hio unayoingia mayo jamii forum alafu nunua unga na michele weka ndani na gas jaza kabisa utakuja kunishukuru badae alafu ingia mtaani au njoo hulu town pita kila ofisi omba kaz kila siku ndani ya wiki utakua ushapata
Ushauri wa hovyo kabisa, simu ndo kila kitu, hata ikipatikana nafasi ya kazi au kibarua inakua rahisi watu kumjuza

Usiuze simu jamaa kaza hivyo hivyo, mi niliwai kusaidiwa na mtu humu ndani yupo USA,watu wema wapo naamini utasaidika iwe mtandaoni au mtaani usikate tamaa
 
Acha tu hiyo hali at some point katika maisha lazima uyumbe, nakumbuka 2014 nimemaliza chuo. Nikasema siendi home ngoja ni baki Mwanza ni hustle... Kodi ikaisha nika hamia kwa muhuni wangu mmoja anakaa mkuyuni, sasa huko ndo nikaja kupata ugali dagaa wa jero. Ila unapatikana mchana tu.... So kula ni kila saa sita na nusu mchana. Hauna nauli hata ya kwenda mjini kuta futa hiyo kazi, bili za maji, umeme ilikuwa changamoto sana. Demu akaja niacha maana kiukweli hakuona future... Hii ilikuwa ndo me against the world. Ila nothing is permanent in this life.
Lifel lika songa nikaja kujipata early 2016 baada ya trial and error nyingi sana
 
Nilikuwa naanza asubuhi napenda daladala lakini sijui naenda wapi, kikifika mwenge pale naenda kukaa kuna bar moja pale mwenge stendi enzi hizo sijui panaitwa kwa mama nani sijui, makaa pale weee siagizi chochote mpaka saa 10 ndiyo narudi home Dah sitasahau
 
Usiombe biashara ife au kazi iote mbawa, naishi maisha ya kuungaunga mwezi wa pili sasa baada ya kibarua kuota nyasi, poleni sana kwa mliowai kuishi maisha haya, maisha ya kula mlo mmoja na kutojua kesho yako, maisha ya kula leo saa saba mchana mpaka kesho saa saba mchana, hatari ogopa.

Jamaa unakonda ubaki kichwa tu, nimejiapiza hata home likitokea tatizo siwezi kwenda kwa muonekano huu.

Kama umewahi kupita nyakati kama hizi share hapa na wadau siku yako ilivyokua inapita kwa kuungaunga.
Kawaida ndio bongo africa kama kuna kalaana flani hivi..!
 
Don't worry about a thing
'Cause every little thing gonna be alright
Singin', "Don't worry about a thing
'Cause every little thing gonna be alright"

Rise up this mornin', smile with the risin' sun
Three little birds pitched by my doorstep
Singin' sweet songs of melodies pure and true
Sayin', "This is my message to you""
Singin', "Don't worry about a thing
'Cause every little thing is gonna be alright"
Singin', "Don't worry, don't worry 'bout a thing
'Cause every little thing's gonna be alright"
View attachment 3004145
Huu wimbo mjomba wangu aliupiga usiku mzima .Hii ni baada ya kukamata milioni 18.Mwaka 2002 .Mwamba alikuwa anadharaulika ila hakuna aijuae kesho.Alinunua makorokoro yote siku moja.Kitanda,tv ,redio ,desktop halafu akaenda saloon akakata nywele ,akarudi maskani akasugua miguu kwa msasa laini .Usiku mzima hii ngoma ilikuwa inarindima tu.Umenikumbushaaa mbali.Maisha?! Usimharakishe Mungu kwa kweli.
 
Usiombe biashara ife au kazi iote mbawa, naishi maisha ya kuungaunga mwezi wa pili sasa baada ya kibarua kuota nyasi, poleni sana kwa mliowai kuishi maisha haya, maisha ya kula mlo mmoja na kutojua kesho yako, maisha ya kula leo saa saba mchana mpaka kesho saa saba mchana, hatari ogopa.

Jamaa unakonda ubaki kichwa tu, nimejiapiza hata home likitokea tatizo siwezi kwenda kwa muonekano huu.

Kama umewahi kupita nyakati kama hizi share hapa na wadau siku yako ilivyokua inapita kwa kuungaunga.
Yani njaa mpaka unakula mbegu? Au hata mbegu huna?

Uko wapi mkuu?
 
Duh mkuu,mbona mimi naweza kukaa zaidi ya mwaka sijanunua nguo? Na ziko poa tu. Hapa nilipo sijanunua nguo tangu mwaka jana
Itakuwa una rundo la nguo. Na mwaka mzima hujanunua nguoa zitakuja kuchakaa kwa pamoja.
Kwa kawaida wanaume hatuna nguo nyingi. Mimi nilipopata majanga hayo nilijifunza kununua suruali 2, shati/tishert 2 boxer 2 na vests 2, pair 1 ya viatu kila mwezi kwa mwaka mzima just to keep up nilizo nazo.
 
Huu wimbo mjomba wangu aliupiga usiku mzima .Hii ni baada ya kukamata milioni 18.Mwaka 2002 .Mwamba alikuwa anadharaulika ila hakuna aijuae kesho.Alinunua makorokoro yote siku moja.Kitanda,tv ,redio ,desktop halafu akaenda saloon akakata nywele ,akarudi maskani akasugua miguu kwa msasa laini .Usiku mzima hii ngoma ilikuwa inarindima tu.Umenikumbushaaa mbali.Maisha?! Usimharakishe Mungu kwa kweli.
Mjomba alikua na machungu sana
 
Nilikuwa naanza asubuhi napenda daladala lakini sijui naenda wapi, kikifika mwenge pale naenda kukaa kuna bar moja pale mwenge stendi enzi hizo sijui panaitwa kwa mama nani sijui, makaa pale weee siagizi chochote mpaka saa 10 ndiyo narudi home Dah sitasahau
Unatoka magetoni ili ionekane unaenda kushughulika kumbe huna mishe yoyote, usiombe yakukute
 
Niliishi hayo maisha.
Yalikua magumu mno ni kipindi ambacho niliona kumbe nina talent nyingi sana.

Nilikuwa nafundisha sehemu mbili kwa mda tofauti tofauti.

Nilikua saidia fundi.
Nilikua mission town.
Nilikua mpanga matukio.
Nilikua mpokeaji wageni jijini hapa.
Nilifanya kazi ya welding.

Katika harakati zote nilikua natembea kwa mguu sana rangi tatu to mbande.

Gerezani to rangi tatu. Pita short kati sana.

Ukiambiwa watu wanakunywa energy na juisi mkuu ni kweli kabisa maana ndo ilikua zangu, kuna mda nafanya kazi jua kali ni kunywa maji tu.

Ukifika mda wa kula pale kazini wenzangu wakiagiza chakula mimi natoa sababu kibao kumbe nia yangu kujibana tu ile pesa ambayo ningenunua chakula nafanya mambo mengine

Namshukuru Mungu msoto wote huo sikupata vidonda vya tumbo.

Kuna kipindi nilikua nafundisha chekechea. Watoto wanasumbua hatari ila niliweza ku control vile viumbe mpaka wazazi wakanipa maua yangu.

Maisha yale yalinipa despline ya matumizi ya pesa..

Katika upambanaji wako wote jitahidi uwe na simu kubwa, uwe na mawasiliano na watu maana connection zipo huko

Ondoa aibu alafu pambana

Nilifanya mambo mengi sana, japo sijajipata kiivo ila kwa sasa akili imepevuka najua nataka nini. Najua nafanya nini.
 
Back
Top Bottom