Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Ni kukaza mkanda. Mwaka wa nne huu mimi ni jobless mambo uliyoandika hapo ndio maisha yangu ya kawaida ya kila siku.

Sio tu kupoteza mpenzi utajikuta umepoteza hadi marafiki na ndugu zako wa karibu.
Kuna kipindi kilifika nilikuwa na wasiliana na maza tu kwenye simu.
Kuna kazi kipato cha mwezi Ukikigawanya kwa bajeti ya kila siku unakosa hata kidogo cha ku save, unakua unafanyia kula,kodi na kuvaa mara moja moja..
 
Duh mkuu,mbona mimi naweza kukaa zaidi ya mwaka sijanunua nguo? Na ziko poa tu. Hapa nilipo sijanunua nguo tangu mwaka jana
Nguo zinachoka kutokana na quality, idadi ya nguo ulizonazo, shughuli za kuingiza kipato unazofanya.
Sasa mtu unakuta anasuruali 5 yaani mwaka tu zinachoka kutokana na kuzifua mara kwa mara.
 
Ila mamaza wana roho nzuri sana aisee. Ata isiwe kwa mtoto wake ila mwanamke mwenye mtoto uwa anakua na huruma kwa mtoto yoyote (naamini hivyo).

Kuna siku nimetoka Posta, nipo Mwendokasi. Kuna mchongo nilifukuzia afu ukafeli vibaya sana. Yaan sikua na maisha.

Nipo kwenye Mwendokasi haina watu wengi kwasababu ilikua mchana, nikawa naongea kumbe mwenyewe hafu sijui. Napiga hesabu hivi na vile kugeuka pembeni kuna mama ananiangalia kwa huruma. Nikazuga naimba. Akaniambia hujambo mwanangu, dah. Simjui kabisa ila ile ujambo imetoka moyoni. Nikamjibu sijambo shikamoo. Tukapiga story 2 3 nikashuka Ubungo.

Inaonekana aliona kijana mafaili yamecorrupt akasema anichangamshe kidogo na ilisaidia. Au usikute ana kijana umri tunaendana akasema labda na mwanangu anapitia kipindi kigumu hivi.

Wabarikiwe sana wazazi.
Sio wote, wa kwangu hayuko hivyo
 
Bwana bwana usiombee kupitia hii hali. (wouldnt wish it even for my worst enemy) jobless corner isikie tuu kwa wenzio maana ikupate mbona utajua maisha yakoje. Tena ombea ikukute wakati huna mchuchu, kama una mchuchu aisee nakwambia ndio utakapo tambua kuwa woman = devil reincarnated.

Mie nilibwagwa na kuambiwa sina mbele wala nyuma kama mche wa sabuni. Mzazi anakusikitikia tena wa mama ndio kabisa unamuona tuu anauzunika, acha kabisa maumivu yake ni balaaa.

All in all mwanawane wewe pambana tuu ndio mapito ya maisha always bliv good is going to happen na muhimu sana angalia sana wale watakao kuwa nae katika wakati huu maana siku neema ikishuka hao ndio wakula nao.
mche wa sabuni
 
Don't worry about a thing
'Cause every little thing gonna be alright
Singin', "Don't worry about a thing
'Cause every little thing gonna be alright"

Rise up this mornin', smile with the risin' sun
Three little birds pitched by my doorstep
Singin' sweet songs of melodies pure and true
Sayin', "This is my message to you""
Singin', "Don't worry about a thing
'Cause every little thing is gonna be alright"
Singin', "Don't worry, don't worry 'bout a thing
'Cause every little thing's gonna be alright"
 
Mungu ni mwema! Amini tu ipo siku atakufungulia milango!
Nakumbuka 2020 niliacha kazi mahali baada ya kuona kuna boya mmoja ananipelekea umbea kwa boss!

Nikapiga chini ile kazi nikiamini haitachkua mda ntapata nyingine, mzee hapo ndo nilikoma, nilikaa mwaka na nusu sina mbele wala nyuma, nikipiga mizinga marafiki wote nliokuwa nao, bado ndugu, hapo nna mke na mtoto wa mwaka mmoja,

Ilifika mahali mtoto akabaki kichwa na tumbo kubwaa, anakula ugali hata usio na mboga....tulikula dagaa mpaka tukanukia dagaa, inafika muda hakuna chakula ndani kabisa na huna hata sent na na na huna wa kumpiga kizinga tena.....hii hali sitakaa niisahau!

Ila Mungu alikuja kunikumbuka, angalau nikapata mahali angalau hata milo 3 inapatikana sasahivi, ila ile hali imenifunza, kila nikikumbuka najikuta naweka hakiba! Sasa hivi nimekusanya imefika mil 10 nataka nifungue biashara ya kuniboost maana hiz ajira hazitabirika asee!
 
Acha tu ndugu yangu.
Kuna huo mwaka siwezi kuusahau, nipo mjini Dar mambo yamesimama yaani yamekwama hayasogei wala kwenda.
Kipindi hicho ikanibidi nihame nilikokua naishi kwa jamaa niende Buguruni Ghana kwa jamaa yangu mwingine yeye alikua ni mlinzi.
Nilichapika na maisha yaani unatafuta hata kazi ya kufagia na hupati, kazi za nguvu hakuna, huwezi amini hadi zile za kubeba zege nazo zilihitaji connection ndio upate.
Mungu si athumani, nikapata kibarua Ubungo, mshahara laki na nusu. Ukumbuke hapo kule geto tunaishi room bei 40k kwa mwezi na tunachangia pasu. Nikawa kila siku naamka mapema sana nilikua natumia saa limoja na dakika 20 kutoka Buguruni hadi kibaruani Ubungo na hapo hakuna bajeti ya daladala.
Nilipigika vibaya mno kuna wakati ikawa inanibidi niishi kwa bajeti ya buku tu kwa siku yaani hapo nipate asbuhi, mchana na usiku. Na hapa ndipo nikaweka undugu wa karibu sana na mihogo. Kuna mama mmoja alikua napika mihogo pale Tabata TOT darajani, upande wa kushoto ukiwa unaenda Ubungo aisee alinifaa sana wakati ule nilikua nanunua mihogo ya jero ananipa vipande vinne badala ya vitatu nikipiga na maji yangu ya bomba basi saa kumi ninapopita tena wakati wa kurudi napiga ya jero tena na kachumbari nyingii ndio nitolee hadi kesho.Nakumbuka ilifika hatua nikisikia harufu ya mihogo napata kichefuchefu dadadadeqq!
Mambo yaliendelea hivyo hadi kupata kibarua kingine nikawa nalipwa 250k tukahama pale tulipokua tunakaa tukasogea kule wanaita Buguruni karibu na mabwawa tukapata chumba na kijisebule kidogo kwa 50k tukaanza na kujipikia. Na happ ndio angalau nafuu ikionekana.
Siwezi kusahau ule mwaka kwakweli, nilipata SOMO KAMILI LA NAMNA YA KUUMWA NA NJAA na ndio maana hata leo nikikutana na hustler ama dogo analalamika nja hasa hasa mitaa ya kujitafuta kama vile Buguruni, Temeke na Mbagala basi kiroho safi kama kuna mgahawa jirani namlipia chakula maana najua njaa inavyojua kunyanyasa na kutesa mwili.
Ukiwa na njaa unaweza kulia kwa uchungu na chozi lisitoke, kuna siku mwanangu mlinzi hakua na kitu ikabidi aende sokoni Buguruni kuokota mihogo akatafuna mibichi ndio siku ikaenda. Kingine kuna ile hali ya kujua unawaza kimya kimya kumbe unaongea kwa sauti aise, unashtuka mbona kama mtu anakuangalia ndio unashtuka kuwa ulikua ukiongea kwa sauti.Sijawahi kumshangaa mtu anayeongea mwenyewe barabarani, kitu nitakachofanya ni kumsalimia tu ili ashtuke basi.
Ukikuta mtu anakulilia njaa ya tumbo yaani hajala, jama unaweza kumsaidia fanya hivyo na kama una wasiwasi basi mlipoe mgahawani apooze.​
dah tunapita mengi sana pole mkuu
 
Mungu ni mwema! Amini tu ipo siku atakufungulia milango!
Nakumbuka 2020 niliacha kazi mahali baada ya kuona kuna boya mmoja ananipelekea umbea kwa boss!

Nikapiga chini ile kazi nikiamini haitachkua mda ntapata nyingine, mzee hapo ndo nilikoma, nilikaa mwaka na nusu sina mbele wala nyuma, nikipiga mizinga marafiki wote nliokuwa nao, bado ndugu, hapo nna mke na mtoto wa mwaka mmoja,

Ilifika mahali mtoto akabaki kichwa na tumbo kubwaa, anakula ugali hata usio na mboga....tulikula dagaa mpaka tukanukia dagaa, inafika muda hakuna chakula ndani kabisa na huna hata sent na na na huna wa kumpiga kizinga tena.....hii hali sitakaa niisahau!

Ila Mungu alikuja kunikumbuka, angalau nikapata mahali angalau hata milo 3 inapatikana sasahivi, ila ile hali imenifunza, kila nikikumbuka najikuta naweka hakiba! Sasa hivi nimekusanya imefika mil 10 nataka nifungue biashara ya kuniboost maana hiz ajira hazitabirika asee!
Pole na hongera mkuu
 
Umenifanya nivute taswira mpaka chozi likapita, cha muhimu ongea na wanaume wenzio na ke waliokomaa, wakiskia issue yyte wakuite, kikuu ongea na muumba wako , yaani Mungu kinywani chako asitoke, yote yatapita .
Ameen!
 
Back
Top Bottom