Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Usiombe biashara ife au kazi iote mbawa, naishi maisha ya kuungaunga mwezi wa pili sasa baada ya kibarua kuota nyasi, poleni sana kwa mliowai kuishi maisha haya, maisha ya kula mlo mmoja na kutojua kesho yako, maisha ya kula leo saa saba mchana mpaka kesho saa saba mchana, hatari ogopa.

Jamaa unakonda ubaki kichwa tu, nimejiapiza hata home likitokea tatizo siwezi kwenda kwa muonekano huu.

Kama umewahi kupita nyakati kama hizi share hapa na wadau siku yako ilivyokua inapita kwa kuungaunga.
Una zungumzia Yale maisha ya watu kukuona dishi japo u timamu?

Maisha ya kutembea huku ukiwa hujiamini na kujiona Kama sio wewe/ yule og?

Maisha ya kuwa kwepa watu wanao kujua kwa kuhofia kuchekwa?

Maisha ya Kula vyakula vya walevi wa pombe za kienyeji virabuni?

Au Yale maisha ya kunywa pombe local ili upunguze njaa kwani pesa ya Kula hakuna?

Hakika nimaisha magumu na yanayo umiza mkuu

Niku shauri tu baada ya kukupa pole kwamba

Kwenye maisha hakuna hari inayo dumu iwe nzuri au mbaya
 
Been there
 
Kuna staff wa NMB aliachishwa kazi. Jamaa alipukutika Sana. Kwakweli wafanyakazi jipangeni mapema kabla mambo hayajaharibika. Nakumbuka aliniambia "Mdogo wangu, ukiachishwa kazi kila kitu utakachofanya kina feli sijui kwanini".
 
Usiombe biashara ife au kazi iote mbawa, naishi maisha ya kuungaunga mwezi wa pili sasa baada ya kibarua kuota nyasi, poleni sana kwa mliowai kuishi maisha haya, maisha ya kula mlo mmoja na kutojua kesho yako, maisha ya kula leo saa saba mchana mpaka kesho saa saba mchana, hatari ogopa.

Jamaa unakonda ubaki kichwa tu, nimejiapiza hata home likitokea tatizo siwezi kwenda kwa muonekano huu.

Kama umewahi kupita nyakati kama hizi share hapa na wadau siku yako ilivyokua inapita kwa kuungaunga.
Nyakati ngumu za kupoteza kazi ghafla zilikutana,na toka wakati huo,mpaka leo nsishi maisha ya kuunga kuunga,nikisikia mtu ana pesa,za kumtosheza maisha yake,na kuwapa na wengine,huwa nabaki kushangaa.Hali ni ngumu,haielezeki.
 
Pole ndugu, nilipoteza kazi nikiwa na familia ya watoto 2, usiombe hii hali ukutane nayo.

Ilichukua mwaka mzima kuwa stable kiakili.
Halafu anatokea mburukenge mmoja asiye na akili kwenye fuvu aliyeajiriwa au mwenye kibiashara cha kuingiza shilingi kadhaa za kusukuma siku ,anawananga jobless .
Jobless tunatamba kitaa na kushine [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Jobless wapewe heshima yao
 
Usiombe biashara ife au kazi iote mbawa, naishi maisha ya kuungaunga mwezi wa pili sasa baada ya kibarua kuota nyasi, poleni sana kwa mliowai kuishi maisha haya, maisha ya kula mlo mmoja na kutojua kesho yako, maisha ya kula leo saa saba mchana mpaka kesho saa saba mchana, hatari ogopa.

Jamaa unakonda ubaki kichwa tu, nimejiapiza hata home likitokea tatizo siwezi kwenda kwa muonekano huu.

Kama umewahi kupita nyakati kama hizi share hapa na wadau siku yako ilivyokua inapita kwa kuungaunga.
Naomba kujua jinsia yako Kama hutojali tafadhali
 
Acha tu ndugu yangu.
Kuna huo mwaka siwezi kuusahau, nipo mjini Dar mambo yamesimama yaani yamekwama hayasogei wala kwenda.
Kipindi hicho ikanibidi nihame nilikokua naishi kwa jamaa niende Buguruni Ghana kwa jamaa yangu mwingine yeye alikua ni mlinzi.
Nilichapika na maisha yaani unatafuta hata kazi ya kufagia na hupati, kazi za nguvu hakuna, huwezi amini hadi zile za kubeba zege nazo zilihitaji connection ndio upate.
Mungu si athumani, nikapata kibarua Ubungo, mshahara laki na nusu. Ukumbuke hapo kule geto tunaishi room bei 40k kwa mwezi na tunachangia pasu. Nikawa kila siku naamka mapema sana nilikua natumia saa limoja na dakika 20 kutoka Buguruni hadi kibaruani Ubungo na hapo hakuna bajeti ya daladala.
Nilipigika vibaya mno kuna wakati ikawa inanibidi niishi kwa bajeti ya buku tu kwa siku yaani hapo nipate asbuhi, mchana na usiku. Na hapa ndipo nikaweka undugu wa karibu sana na mihogo. Kuna mama mmoja alikua napika mihogo pale Tabata TOT darajani, upande wa kushoto ukiwa unaenda Ubungo aisee alinifaa sana wakati ule nilikua nanunua mihogo ya jero ananipa vipande vinne badala ya vitatu nikipiga na maji yangu ya bomba basi saa kumi ninapopita tena wakati wa kurudi napiga ya jero tena na kachumbari nyingii ndio nitolee hadi kesho.Nakumbuka ilifika hatua nikisikia harufu ya mihogo napata kichefuchefu dadadadeqq!
Mambo yaliendelea hivyo hadi kupata kibarua kingine nikawa nalipwa 250k tukahama pale tulipokua tunakaa tukasogea kule wanaita Buguruni karibu na mabwawa tukapata chumba na kijisebule kidogo kwa 50k tukaanza na kujipikia. Na happ ndio angalau nafuu ikionekana.
Siwezi kusahau ule mwaka kwakweli, nilipata SOMO KAMILI LA NAMNA YA KUUMWA NA NJAA na ndio maana hata leo nikikutana na hustler ama dogo analalamika nja hasa hasa mitaa ya kujitafuta kama vile Buguruni, Temeke na Mbagala basi kiroho safi kama kuna mgahawa jirani namlipia chakula maana najua njaa inavyojua kunyanyasa na kutesa mwili.
Ukiwa na njaa unaweza kulia kwa uchungu na chozi lisitoke, kuna siku mwanangu mlinzi hakua na kitu ikabidi aende sokoni Buguruni kuokota mihogo akatafuna mibichi ndio siku ikaenda. Kingine kuna ile hali ya kujua unawaza kimya kimya kumbe unaongea kwa sauti aise, unashtuka mbona kama mtu anakuangalia ndio unashtuka kuwa ulikua ukiongea kwa sauti.Sijawahi kumshangaa mtu anayeongea mwenyewe barabarani, kitu nitakachofanya ni kumsalimia tu ili ashtuke basi.
Ukikuta mtu anakulilia njaa ya tumbo yaani hajala, jama unaweza kumsaidia fanya hivyo na kama una wasiwasi basi mlipoe mgahawani apooze.​
 
Una zungumzia Yale maisha ya watu kukuona dishi japo u timamu?

Maisha ya kutembea huku ukiwa hujiamini na kujiona Kama sio wewe/ yule og?

Maisha ya kuwa kwepa watu wanao kujua kwa kuhofia kuchekwa?

Maisha ya Kula vyakula vya walevi wa pombe za kienyeji virabuni?

Au Yale maisha ya kunywa pombe local ili upunguze njaa kwani pesa ya Kula hakuna?

Hakika nimaisha magumu na yanayo umiza mkuu

Niku shauri tu baada ya kukupa pole kwamba

Kwenye maisha hakuna hari inayo dumu iwe nzuri au mbaya
Acha Maisha yanakunyoosha mwili unanyooka kama mti
 
Usiombe biashara ife au kazi iote mbawa, naishi maisha ya kuungaunga mwezi wa pili sasa baada ya kibarua kuota nyasi, poleni sana kwa mliowai kuishi maisha haya, maisha ya kula mlo mmoja na kutojua kesho yako, maisha ya kula leo saa saba mchana mpaka kesho saa saba mchana, hatari ogopa.

Jamaa unakonda ubaki kichwa tu, nimejiapiza hata home likitokea tatizo siwezi kwenda kwa muonekano huu.

Kama umewahi kupita nyakati kama hizi share hapa na wadau siku yako ilivyokua inapita kwa kuungaunga.
Pole sana.
 
Back
Top Bottom