Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

Uliishi maisha gani baada ya kupoteza Kazi au Biashara?

mwanawane usichomoke hapo, tena kaa tuliiiii. huku mtaani ni noma mazeee. mambo ya kuanza kujibu maswali ya interview sio kabisa. tulizana hapo hicho kidogo wapata chatosha as long as its legally earned.

ah mwanawane hilo litegemee tuu hapo mzee utajua kila aina ya punyeto 😀😀😀😀😀😀
be strong man vumilia kuwa na mkakati wa namna ya kujikwamua hapo ulipo. mademu wa sasa wewe usiwaze kabisa utambulia matusi tuu. hawa jema hawa
Hapo kwenye kukataliwa na madem aisee🤣🤣🤣😂😂 acha tu
 
Nyakati ngumu za kupoteza kazi ghafla zilikutana,na toka wakati huo,mpaka leo nsishi maisha ya kuunga kuunga,nikisikia mtu ana pesa,za kumtosheza maisha yake,na kuwapa na wengine,huwa nabaki kushangaa.Hali ni ngumu,haielezeki.
Pole sana ndugu
 
Pole sana kijana,JF ndio faraja na hongera kwa kulileta hilo hapa maana unaweza kufunguliwa fursa.

Tuko pamoja ila wewe naona una nafuu kabisa hivyo yangu nikieleza hapa utaangua na kicheko ila mwanaume ni kupambana haswa, hivi kibarua/kazi gani ulikuwa unaifanya rafiki?
 
Acha tu ndugu yangu.
Kuna huo mwaka siwezi kuusahau, nipo mjini Dar mambo yamesimama yaani yamekwama hayasogei wala kwenda.
Kipindi hicho ikanibidi nihame nilikokua naishi kwa jamaa niende Buguruni Ghana kwa jamaa yangu mwingine yeye alikua ni mlinzi.
Nilichapika na maisha yaani unatafuta hata kazi ya kufagia na hupati, kazi za nguvu hakuna, huwezi amini hadi zile za kubeba zege nazo zilihitaji connection ndio upate.
Mungu si athumani, nikapata kibarua Ubungo, mshahara laki na nusu. Ukumbuke hapo kule geto tunaishi room bei 40k kwa mwezi na tunachangia pasu. Nikawa kila siku naamka mapema sana nilikua natumia saa limoja na dakika 20 kutoka Buguruni hadi kibaruani Ubungo na hapo hakuna bajeti ya daladala.
Nilipigika vibaya mno kuna wakati ikawa inanibidi niishi kwa bajeti ya buku tu kwa siku yaani hapo nipate asbuhi, mchana na usiku. Na hapa ndipo nikaweka undugu wa karibu sana na mihogo. Kuna mama mmoja alikua napika mihogo pale Tabata TOT darajani, upande wa kushoto ukiwa unaenda Ubungo aisee alinifaa sana wakati ule nilikua nanunua mihogo ya jero ananipa vipande vinne badala ya vitatu nikipiga na maji yangu ya bomba basi saa kumi ninapopita tena wakati wa kurudi napiga ya jero tena na kachumbari nyingii ndio nitolee hadi kesho.Nakumbuka ilifika hatua nikisikia harufu ya mihogo napata kichefuchefu dadadadeqq!
Mambo yaliendelea hivyo hadi kupata kibarua kingine nikawa nalipwa 250k tukahama pale tulipokua tunakaa tukasogea kule wanaita Buguruni karibu na mabwawa tukapata chumba na kijisebule kidogo kwa 50k tukaanza na kujipikia. Na happ ndio angalau nafuu ikionekana.
Siwezi kusahau ule mwaka kwakweli, nilipata SOMO KAMILI LA NAMNA YA KUUMWA NA NJAA na ndio maana hata leo nikikutana na hustler ama dogo analalamika nja hasa hasa mitaa ya kujitafuta kama vile Buguruni, Temeke na Mbagala basi kiroho safi kama kuna mgahawa jirani namlipia chakula maana najua njaa inavyojua kunyanyasa na kutesa mwili.
Ukiwa na njaa unaweza kulia kwa uchungu na chozi lisitoke, kuna siku mwanangu mlinzi hakua na kitu ikabidi aende sokoni Buguruni kuokota mihogo akatafuna mibichi ndio siku ikaenda. Kingine kuna ile hali ya kujua unawaza kimya kimya kumbe unaongea kwa sauti aise, unashtuka mbona kama mtu anakuangalia ndio unashtuka kuwa ulikua ukiongea kwa sauti.Sijawahi kumshangaa mtu anayeongea mwenyewe barabarani, kitu nitakachofanya ni kumsalimia tu ili ashtuke basi.
Ukikuta mtu anakulilia njaa ya tumbo yaani hajala, jama unaweza kumsaidia fanya hivyo na kama una wasiwasi basi mlipoe mgahawani apooze.​
Pole kwa uliyopitia mkuu,sisi ndo tupo kwenye haya mapito tunasonga
 
Pole sana kijana,JF ndio faraja na hongera kwa kulileta hilo hapa maana unaweza kufunguliwa fursa.

Tuko pamoja ila wewe naona una nafuu kabisa hivyo yangu nikieleza hapa utaangua na kicheko ila mwanaume ni kupambana haswa, hivi kibarua/kazi gani ulikuwa unaifanya ra

Pole sana kijana,JF ndio faraja na hongera kwa kulileta hilo hapa maana unaweza kufunguliwa fursa.

Tuko pamoja ila wewe naona una nafuu kabisa hivyo yangu nikieleza hapa utaangua na kicheko ila mwanaume ni kupambana haswa, hivi kibarua/kazi gani ulikuwa unaifanya rafiki?
Nilikua nafanya kazi kiwandani mkuu
 
Mimi Nina swali,sio kwa ubaya.. huwa inatokana na Nini mtu anafanya kazi miaka mitano,but akipigwa chini miezi miwili tu analia njaa,

Hata akiba ya Kuanza biashara ndogo Huwa hakuna??hata Hela ya kula miezi sita wakati unajitafuta hakuna??

Changamoto inakuga Nini??
 
Ni kukaza mkanda. Mwaka wa nne huu mimi ni jobless mambo uliyoandika hapo ndio maisha yangu ya kawaida ya kila siku.

Sio tu kupoteza mpenzi utajikuta umepoteza hadi marafiki na ndugu zako wa karibu.
Kuna kipindi kilifika nilikuwa na wasiliana na maza tu kwenye simu.
 
Mimi Nina swali,sio kwa ubaya.. huwa inatokana na Nini mtu anafanya kazi miaka mitano,but akipigwa chini miezi miwili tu analia njaa,

Hata akiba ya Kuanza biashara ndogo Huwa hakuna??hata Hela ya kula miezi sita wakati unajitafuta hakuna??

Changamoto inakuga Nini??
Mshahara wa 300k 400k hata ukilipwa kwa miaka 10 ukija kusimamishwa mwaka tuu ni vilio na kusaga meno
Hii ni kwasabb mshahara huo ni ngumu mtu kuweka akiba hasa kama ana watu wanao mtegemea
 
Back
Top Bottom