Back in days
Hapo nimerudi chuo kwenda kufanya Supplimentary, nilikuwa na kama 500k mfukoni. Nimefika nikapambana nikapata pakulala,, doh , shetani la kamari likanipitia maana nilikuwa Mraibu wa kubet miaka hiyo,, nikaplace bet ya 100k,, inplay, ikaliwa.
Hasira ya kukimbiza hasara nikaweka 250k ikaliwa tena,
Hasira zikapanda huku najipa moyo ntairudisha labda , nikafanikiwa kula jumla nikawa na 130k kwenye Account ya bet.,, Shetani likanimbia weka yote upate zaidi, bwana bwana nikaweka Holaa,, nikaliwaa.
Hasira zikazidi kuwa kali Zaidi nikamalizia kudeposite tena 136k, nikala ikafika 200k, nikaanza kupata amani kwa mbali. Oooh mchezo ule usivyokuwa na baraka na ulivyolaaniwa ikaliwa yoote. Bare in your mind hapo mfukoni imebaki kama 14,000/= na Sup ratiba imekaa vibaya natakiwa nisubir mpk wiki ya tatu.
Nilianza kushindia muhogo mmoja kwa siku, na hapo ndio niliona picha halisi ya njaa, nikagundua pia ukiwa na Njaa haulali.
Wiki ya mwisho nilikaa siku 2 nakumbuka bila kula nakunywa maji na karanga tu.
Nauli ya kurudi nyumbani nilikuwa sina ikabid nikawaombe wale matrafic wa Pale Nane nane Dodoma waniombee lift alooh.
VIJANA KAMARI NI UMASIKINI.