Ulijisikiaje baada ya kugundua unaenda kuwa mzazi kwa Mara ya kwanza?


Comment inavutia mpk nimetamani nizae na kijana wa kumpenda hivi mtoto ila weeee huu ni mtego unaweza kuwa singomaza ghafla[emoji1787][emoji1787]
 
Unakuta wanaume wengine akiambiwa mimba anasepa..

All in all,
Kwenye hili wanawake hubeba mzigo mzito usiombe akifukuzwa kwao😊
All in all, kama mtu ana ndoto kubwa za kuzipambania na bado hajajipata, asimbebeshe mtoto wa watu mimba, atavuruga kila kitu kwenye maisha yake.
 
aisee yaani una kula chakula kila siku, Hadi miezi 9 itimieπŸ˜‚πŸ€”.

Huo muda na nguvu SI Bora niwekeze kwenye mambo ya misingi zaidi.
Kula ntakula ,ila sio mfululizo ya hio miezi 9 πŸ˜‚πŸ˜‚
 
All in all, kama mtu ana ndoto kubwa za kuzipambania na bado hajajipata, asimbebeshe mtoto wa watu mimba, atavuruga kila kitu kwenye maisha yake.
Kwa kweli that's why MAPROFESA WENGI 😊 unakuta anaanzisha familia uzeeni...

Huwezi kua na PEACE OF MIND still ukaweza ku publish your article in international journey 10times..

Ku opt kua responsible father it's not easy Ni kujinyima na kuacha kua selfish sometimes ku sucrifice your dreams for others
 
Mkubwa Grahams na Shadow7, Madame B semeni Jambo.
Mimi kusema ule ukweli wa Mungu kwanza mimba yangu iliingia pasi na matarajio yoyote maana kipindi nashika ujauzito ndio kwanza nilikuwa nimemaliza kidato cha pili, sasa wakati wa likizo haya mambo ya kwenda club, nikakutana na baba mtoto wa mwanangu.
Ilikuwa ngumu kuelezea ni jinsi gani wazazi wangu (r.i.p) walivyoipokea ile hali.
Ila nashukuru Mungu wazazi wangu walinielewa na kuipokea hali yangu.

Nilijifungua salama kwa msaada mkubwa wa wazazi wangu na madaktari wa Mwananyamala hospital (Mungu awatunze vyema)
Pia nilipata sapoti kubwa toka ukweni kwa baba mtoto wangu, kuanzia baba mtoto, dada zake, shemeji zangu mpaka mkwe wangu (alifiwa na mumewe)

Kiukweli nilijiona bado mdogo kupata mtoto wakati huo ila wazazi wangu walikuwa nami bega kwa bega kuhakikisha sifanyi kosa lolote katika uleaji na makuzi ya mtoto.

Sema Mungu alianza kumpenda zaidi mama yangu, mwanangu akiwa na 1 year alipata ajali mbaya ya gari na alifariki palepale akimuacha mwanangu akisalimika.
Sijakaa vyema baada ya miaka 4 mwanangu akiwa na 4 years baba yangu naye akafariki, can you imagine😭😭😭
Hapo sasa nikafunga kibwebwe na kukazana na malezi
Ni mengi sana nimepitia, ila leo hii mwanangu ni mkubwa na huwa nikiwaonyesha picha ya bibi na babu yake anasema anawakumbuka hao watu.
Malezi si lelemama haswa kwa sie ambao tulipomaliza kunyonyesha tu, watoto tukakabidhi kwa wazazi ili tufanye mambo mengine.

Kiufupi na kilichonisaidia kufahamu zaidi kuhusu malezi ya watoto na ukuaji wake ni katika kazi yangu ya ualimu.
Nilikaa, kucheza, kuwasilikiza, kuwasoma na hata kuuvaa uhusika wa mzazi.
Niliwapenda sana watoto, sana kiasi cha wengine mpaka leo hii hawasiti kuwaambia wazazi wao kuwa mimi nilikuwa zaidi ya mwalimu.

Najivunia kuwa mzazi na mlezi bora, si kwa mwanangu tu, bali kwa jamii nzima inayonizunguka.
Na bandiko la Dkt Gwajima limenipa hamasa ya kuasilli watoto zaidi, si kwamba sina kizazi, la hasha! bali nataka kulea mtoto/watoto wa mwanamke mwenzangu na kumpa malezi bora zaidi kwa maana nimeshakua kiakili na najua changamoto za malezi na ukuaji wake.

Kwa vijana sina cha kuwashauri, ila nawaambia tu wasitoe mimba, wasitupe watoto.
Waleaji tupo, tutawalea kiakili na kimwili.

Na wanawake wenzangu ambao mnahangaika kutafuta watoto usiku na mchan, ipo siku Mungu ataonyesha utukufu wake kwenu na mtabarikiwa watoto wenye afya na siha njema....πŸ™πŸ™πŸ™
NAWAOMBEA!!!

Nanyi akina kaka/baba mnaoweka wadada mimba, kama mnajijua hamtaki watoto VAENI KONDOMU au MWAGIENI SHAHAWA ZENU NJE YA UKE WA MWANAKE.
🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝🀝
 
Pole Sana, na hongera Kwa kusimamia kidete.
Kweli Ume thibitisha wewe ni mtu mbadiπŸ˜‚πŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…