Ulijisikiaje siku ya kwanza umehamia kwenye nyumba yako?

Ulijisikiaje siku ya kwanza umehamia kwenye nyumba yako?

Pongezi kwenu wote mliofanikiwa kujenga na mnaopambana kujenga,kwa itakaye mpendeza naomba kupata Picha ya Chumba kimoja,sebule na jiko ili na mimi nijipange.asante
usisononeke mkuu
mbuyu ulianza kama mchicha
weka nia tu kwake yote yanawezekana
 
Waliingia wezi/ vibaka, kupitia dirisha la sebuleni. Fortunately wakashindwa kuitoa TV, Panasonic ya zamani ina kitako kipana na hakichomoki.... Kwenye kabati la koridoni wakapata pasi na kwenye showrack (koridoni) wakachukua raba zangu pea 2 zilikuwa mpya.

Ile hali ya kuwasikia watu wako ndani kwangu sebuleni wakikorokochoa korokochoa wakati mi nipo chumbani nawasikia... nilipata trauma karibia mwezi mzima nashindwa kulala vizuri.

Badala ya kufurahi ikawa struggle, nikajifunza na kufuga mbwa waliruka fence, ni fupi kiasi just uzio tu na haikuwa imeisha. Baadae nilikuja kupata clue kuwa ni vijana waangalizi wa ujenzi nyumba ya mbele yangu. Na hawajawahi kuja tena.
Pole sana mkuu
 
Unaanza unalala master bedroom, unaamka saa 6 unahamia kids room unalala kidogo, then saa 7 unakuwa umelala guest room, saa 8 unakuwa dinning umelala juu ya meza, ikifika saa 9 upo kwakochi seating room umejikunja, saa 11 unastuka upo stoo halafu pakikucha unaamkia jikoni unaendelea na breakfast.
Daaah
 
Back
Top Bottom