Ulikuwa mpenzi wa gazeti gani miaka ya nyuma?

Habarini wakuu!

Hakika miaka inakwenda. Miaka ya nyuma, magazeti yalikuwa na mvuto sana kuanzia front pages hadi ndani. Yalikuwepo magazeti mengi sana ila Binafsi nilikuwa mpenzi wa magazeti ya Sani na Kiu.

Hao jamaa walikuwa wabunifu sana, kurasa za mbele zilipambwa kwa picha nzuri za mastaa na vichwa vya habari vyenye kuibua hisia sana. Picha za warembo wenye maumbile mazuri na muhtasari wa habari zilizomo ndani yake. Raha ya haya magazeti ilikuwa ni zaidi hata ya kumiliki smartphones siku hizi ambazo ni kama zinaleta depression tu kwa watu. Enzi hizo hakukuwa na mambo ya kuwaza sijui fulani hajaview status yangu, mbona hajanipost, sijui kaniblock na mambo kama hizo

Kulikuwa na simulizi zilizotungwa kwa imahiri, zinazokuachia kiu ya kutaka kufatilia toleo lijalo bila kukosa. Pia kulikuwa na katuni kama vile Lodilofa, Kipepe, Kifimbo Cheza, Madenge, Baba ubaya na nyingine nyingi. Hakika ilikuwa zaidi ya burudani.

Leo nimepita ukurasa fulani nikakutana na picha za katuni za enzi hizo nikapata kurejesha kumbukumbu nyuma sana jinsi burudani hizo zilivyoweza kukonga nyoyo zetu. Hiyo ni kwa ufupi tu.

Wewe unakumbuka nini kuhusu magazeti ya enzi hizo?

Sani,sijawahi kuwa mpenzi wa magazeti ya kichawa na yale kijani baada ya sani.Na hivi sasa. Sisomi lolote.
 
Ambalo nitakalo likuta nyumbani, naenda moja kwa moja kwenye katuni, lakini gazeti la Sani lilijua kutuburudisha kabla hajaja Shigongo na magazeti yake
 
Habarini wakuu!

Hakika miaka inakwenda. Miaka ya nyuma, magazeti yalikuwa na mvuto sana kuanzia front pages hadi ndani. Yalikuwepo magazeti mengi sana ila Binafsi nilikuwa mpenzi wa magazeti ya Sani na Kiu.

Hao jamaa walikuwa wabunifu sana, kurasa za mbele zilipambwa kwa picha nzuri za mastaa na vichwa vya habari vyenye kuibua hisia sana. Picha za warembo wenye maumbile mazuri na muhtasari wa habari zilizomo ndani yake. Raha ya haya magazeti ilikuwa ni zaidi hata ya kumiliki smartphones siku hizi ambazo ni kama zinaleta depression tu kwa watu. Enzi hizo hakukuwa na mambo ya kuwaza sijui fulani hajaview status yangu, mbona hajanipost, sijui kaniblock na mambo kama hizo

Kulikuwa na simulizi zilizotungwa kwa imahiri, zinazokuachia kiu ya kutaka kufatilia toleo lijalo bila kukosa. Pia kulikuwa na katuni kama vile Lodilofa, Kipepe, Kifimbo Cheza, Madenge, Baba ubaya na nyingine nyingi. Hakika ilikuwa zaidi ya burudani.

Leo nimepita ukurasa fulani nikakutana na picha za katuni za enzi hizo nikapata kurejesha kumbukumbu nyuma sana jinsi burudani hizo zilivyoweza kukonga nyoyo zetu. Hiyo ni kwa ufupi tu.

Wewe unakumbuka nini kuhusu magazeti ya enzi hizo?

Sani, Tabasamu, Bongo na kuna lile Femina
 
Kwangu mimi hakuna nyakati nzr za kusoma kama zile nyakati ambazo tulikua tunasoma vijarida vya sani, tabasamu na bongo, hii ni kabla ya ujio wa magazeti ya udaku nafikiri. Kwa ambao walikua ktk umri wa kusoma na kukumbuka wataelewa ninachoongea hapa. Jarida linatoka mara moja kwa mwezi na kuna hadithi nzr ya Eddie Ganzel. Unakaa mwezi mzima kwa shauku ya kusubiri toleo lijalo ili uendelee na hadithi yako. Sikuwahi tena kuishi kwa shauku ya kusoma kama kipindi kile. Ama kweli siku zinaenda kasi.
 
Hakika ni nyakati bora sana kuwahi kutokea.
 
Habarini wakuu!

Hakika miaka inakwenda. Miaka ya nyuma, magazeti yalikuwa na mvuto sana kuanzia front pages hadi ndani. Yalikuwepo magazeti mengi sana ila Binafsi nilikuwa mpenzi wa magazeti ya Sani na Kiu.

Hao jamaa walikuwa wabunifu sana, kurasa za mbele zilipambwa kwa picha nzuri za mastaa na vichwa vya habari vyenye kuibua hisia sana. Picha za warembo wenye maumbile mazuri na muhtasari wa habari zilizomo ndani yake. Raha ya haya magazeti ilikuwa ni zaidi hata ya kumiliki smartphones siku hizi ambazo ni kama zinaleta depression tu kwa watu. Enzi hizo hakukuwa na mambo ya kuwaza sijui fulani hajaview status yangu, mbona hajanipost, sijui kaniblock na mambo kama hizo

Kulikuwa na simulizi zilizotungwa kwa imahiri, zinazokuachia kiu ya kutaka kufatilia toleo lijalo bila kukosa. Pia kulikuwa na katuni kama vile Lodilofa, Kipepe, Kifimbo Cheza, Madenge, Baba ubaya na nyingine nyingi. Hakika ilikuwa zaidi ya burudani.

Leo nimepita ukurasa fulani nikakutana na picha za katuni za enzi hizo nikapata kurejesha kumbukumbu nyuma sana jinsi burudani hizo zilivyoweza kukonga nyoyo zetu. Hiyo ni kwa ufupi tu.

Wewe unakumbuka nini kuhusu magazeti ya enzi hizo?

Risasi,iijumaa wikienda,mwanasport,dimba n.k
 
Back
Top Bottom