Ulikuwa mwanafunzi wa aina gani katika maisha yako ya shule?

Ulikuwa mwanafunzi wa aina gani katika maisha yako ya shule?

Mvivu kusoma ila nafaulu kwa msuli pepa, walimu walikua wananiaminia kua nna akili sana ila binafsi nilijiona bado hizi sio akili zangu.
Darasani sijibu maswali na sababu kuu ni kua hicho kipindi mi sisomi mambo ya nyuma nshasahau mpaka likaribie pepa.

Mpole sana, na sura ya kipadre.
Nilitaminiwa na mamanzi ila kwa ukauzu wangu sikubandua wengi.
 
nilikuwa domo zege nikiongea na mrembo mwanzo mwisho nakenua tu... warembo walikuwa wananiangalia udenda ukiwatoka lakini ndo hivyo tena mi domo kama nimebugia uji wa magimbi.

nilikuwa najulikana kwa kuweka mabanda ya chemia tu. yani nilikuwa nasoma chemistry tu😁 (chemisti)
 
Nilikuwa mtu wa kupambishwa..ni doko ila ukinijaza upepo nafanya vitu vya hatari sana..nilishawahi kupiga soksi iliyowekwa jiwe ndani na nikafunga goli.ila hadi leo vidole vya miguu vibovu..
Kupanda juu ya mizambarau na kupiga samasoti ilikuwa ni kawaida.shule michezo mingi sikuwa siriaz nilikuwa FAILURE sana.ila nilijigundua nna akili nikiwa COLLEGE.
 
Nilikuwa mwanafunzi wa kutoroka sana pale Likonde minor Seminary chini ya Rector JOHN C NDIMBO, currently ni Askofu wa Jimbo la Mbinga na GFS walikuwa ni wasichana wa Mtakatifu Luiza ( St. Louise).

Kila kosa nipo , kanisani nilikuwa sipendi kuenda , wazazi wameitwa mara nyingi shuleni, nimechaniwa sana suruali , lakini kila muhula wasitani wa juu!

Ningekuwa kilaza kama baadhi ya members wa JF wangenifukuza mapema sana.
 
nilikuwa domo zege nikiongea na mrembo mwanzo mwisho nakenua tu... warembo walikuwa wananiangalia udenda ukiwatoka lakini ndo hivyo tena mi domo kama nimebugia uji wa magimbi.

nilikuwa najulikana kwa kuweka mabanda ya chemia tu. yani nilikuwa nasoma chemistry tu[emoji16] (chemisti)
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Binafsi mimi nilikua mvivu sana kusoma (ila nilikua nabukua), sipendi kufanya test (nasingizia ugonjwa).

Ukinisaidia kwenye pepa lazima nikupite, nilikua najua sana kumodify majibu ya msaada.

Sikupenda kuwa kiongozi ila niliishi kama kiongozi.

Tiririka.
Msumbufu, mzinzi, kiburi, majivuno

To say a few mcheshi, mpole somehow 😁
 
Basi nakumbuka form 1 hiyo boarding nilikua mpole naonewa na machozi ya karibu[emoji17],eti nikiishiwa hela ya matumizi nilikua nalia na kusali, ila Mungu ni mwaminifu nikilia hivo na kusali haipiti siku 2 either mama atakuja shule kunicheki, au ntaitwa na mwalimu nikachukue pesa imetumwa[emoji3]. Aah kufika form 3 nikawa tu mpole na mkali kiasi sikutaka kuonewa kabisa. Chuo nikawa mpole zaidi
 
Back
Top Bottom