Toto lisiloeleweka.. darasani kipanga, halafu kwenye matukio ya hivyo natokea, kwenye matokeo mazuri nimo,kwenye watoro sikosekani. Wenye busara nimo, magumashi huku uchochoroni na wahuni wenzangu tunachoma kushi.. sio mpiga misuli lakini pepa fresh.
Primary nilipata msala mzito nikala saana mikwaju na wanangu. Mwalimu wangu wa hisabati alikuwa akinilinda saana kwenye misala misala
O level nikapiga mwalimu nikatimuliwa.
Nikahamia school ya seminary na ni muislam siku sijui wanakula mkate wa bwana nikaunga nikala, wanangu hawana mbavu,
Nikahama 4m 3 nikarudi islamic misala deile, almanusura nitimuliwe hostel, ila walimu wangu wakanitetea nikarudi. Usoni sura ya wema, matokeo mazuri, ila mimi miyeyusho yeyusho tu, kila sekta nimo [emoji1787]
A level sasa [emoji1787], msala wa kumtia mtu mimba, nikawa sitimbi school, ticha wangu wa physics alikuwa ananikubali kinooma jinsi nilivyokuwa naitendea haki FIZIKIA, sasa akawa hanielewi class hanioni, kimasomo nishashuka kumbe msala wa mimba ushanivuruga, shule ishakuwa ngumu.
Si ndio akanirukia hewani, sauti yake nikaifananisha na demu mmoja nishamsalandia saana kabla ya msala, nikampotezea, siwezi mapenzi ya kuchi kuchi hotae mimi, dah, madam kapiga simu sauti inakuja kuja akaniuliza ushajua unaongea na nani, nikavunga, akauliza tena, nikataja jina la yule mrembo, akawa kama ndio yeye,kilichofata nikashusha punch line za kibabe mnoo, mtoto naona kalainika tu, mwishoooni kabisa madam akataja jina la ubini wangu ........... mie mwalimu wako wewe..
Dah! Nikakosa pozi, akapiga, nikapokea akaniambia kumbe haya ndio yanakufanya una drop school huonekani, lakini ile ilikuwa too late kuniokoa form 6 yote ni kama sikusoma, kwa msala wa mimba.
Namkumbuka saana madam yule kidato cha 5 na 6 mwanzoni alinikubali mnooo, fizilia ilikuwa ni kama nimezaliwa na isac mewton, hiyo mechanics ilikuwa inanitii tu.