Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Nlikuwa mvivu wa kusoma pia ila nlikuwa nafaulu tu. Hilo likanifanya nijione mimi nafaa kuishi abroad niwe mgunduzi... Baadaye nimkawaza kuwa rubani au daktari.Binafsi mimi nilikua mvivu sana kusoma (ila nilikua nabukua), sipendi kufanya test (nasingizia ugonjwa).
Ukinisaidia kwenye pepa lazima nikupite, nilikua najua sana kumodify majibu ya msaada.
Sikupenda kuwa kiongozi ila niliishi kama kiongozi.
Tiririka.
Alaaniwe aliyeniinteroduce kwa fruity loops ambayo sasa inaitwa FL studio aisee hii program ilinitoa kwenye reli kabisa hiyo miaka 2007. Badala ya kuzingatia masomo mimi nikawa busy na fruity loops nikisikiliza muziki nasikia synth, piano roll, kicks, bass nawaza nikifka home tu naanza nayo. Hapo nilikuwa o'level. Kilichofuata sasa badala ya kuwa rubani leo nafuga kuku lakini poa tu bado na deal na ndege maana hata kuku ni ndege