Ulimwengu aliponzwa na kujitapa Utustsi!!

Ulimwengu aliponzwa na kujitapa Utustsi!!

Heshima mbele wakuu wote hapa, mchango wangu mdogo:-

1. Ulimwengu alikuwa magazeti ya chama na Mkapa kwa muda mrefu sana, yes ni friends na wanajuana sana tena kwa karibu, lakini only kikazi na sio personal kama Ruhinda na Mushi, au Ngiwilizi walivyokuwa na Mkapa.

2. Kwenye uchaguzi wa 1995 Ulimwengu alipewa nafasi ya kushiriki kwenye kampeni kambi ya Mkapa, alishiriki kikamilifu na walikuwa very close only na namna ya kumanipulate mass kuhusu Mkapa as a person na kiongozi anayefaa na the Mr.clean things, kuwepo kwa Mwalimu ninaamini ndiko hasa kulikomfanya Mkapa kuwajumuisha kina Ulimwengu, Warioba, Butiku, Salim na wengineo wa the hiyo likes, lakini siamini kwamba binafsi in his heart Mkapa aliwataka hawa wote kua karibu naye kisiasa, na alilithibitisha hilo kwenye term ya pili kwa kuwatupa wote nje!

3. Kagame ndiye aliyeanzisha choko choko zilizoishia Balozi Bandora, Ulimwengu, na Mwenyekiti wa zamani wa CCM Bukoba kuambiwa sio raia, kuna a lot of complex things in the middle, Ulimwengu aliishia kuongezewa tu na wapambe wa Mkapa, kwenye hili soo la uraia lakini Mkapa was never involved. Ulimwengu alianza kumshambulia sana Mkapa baada ya kuachwa kwenye kampeni, lakini walioamua kumshugulikia walikuwa ni wapambe wa Mkapa sio yeye binafsi hakuhusika.

4. Wapambe wa Mkapa walilifikisha suala la uraia bungeni, ambako kamati ya ulinzi na usalama ilikubaliana nao kwamba hawa watatu sio raia either wafukuzwe au wapewe nafasi ya kuomba makaratasi upya, Mkapa aliposikia haya akakasirika sana na kufoka sana na kufutilia mbali huu uamuzi wa kamati ya bunge, kwa hiyo wakaendelea mpaka kuwepo kama raia, (nafikiri Ruhinda alihusika sana na huu uamuzi wa Mkapa against bunge). Haikusaidia kitu Ulimwengu akazidisha mashambulizi dhidi ya Mkapa kwenye magazeti yake.

5. Mkapa kwa pembeni akaanza kuwalalamikia wapambe wake kwamba huyu Ulimwengu hana shukrani, ndipo katika kumfuatilia kwamba Ulimwengu anpata wapi kiburi hiki, wahusika wakagundua kwamba alikuwa ni Kagame's man, ndipo siku moja Mkapa akasema sana kwenye mkutano mmoja wkamba hawa waandishi wengine uchwara wanajifanya wanajua huku kumbe wanafadhiliwa na viongozi kutoka nje, tunaweza kuwaomba hao viongozi wa nje waache kuwapa huo ufadhili, haikuchukua muda sana baada ya kuingia kwa Mtandao, Ulimwengu akaanza kwenda chini financially ninaamini Kagame alipewa masharti na somebody kuacha kumfadhili ili mambo yake Kagame yafanikiwe na bongo. Na Mtandao wamekuwa wakimpiga vita sana recently kwa sababu zao wanazozijua wenyewe.

Since then imekuwa ni downhill kwa ulimwengu, lakini najua kuna ndugu yake humu JF angejitokeza kuweka wazi yaliyomjiri.

Respect.

FMeS!
 
Nchi hii, hata haieleweki. hakuna mfumo madhubuti kweli wa ku-monitor vitu kama hivi kama ni kweli? yale yale ya RA na Uraia. Kama umeshawahi kushika uongozi katika nchi hii, hakuna aliyejua kuwa si raia?
 
Mauza uza said:
kunakosa gani watu kusoma UDSM na kurudi kwao????Mbona wapo watu kibao wanachukua uraia wa Marekani au UK wanasomeshwa bure au kwa mkopo na wakimaliza wanarudi makwao(original) India,Pakistan,China na hata TZ na Kenya???mbona wamarekani au waingereza hawapigi kelele???Kusoma sehemu ingine na kurudi kwenu kuwa Waziri ni Kosa?????tuache ubaguzi usio na msingi???Acheni Warwandese waendeleze nchi yao,kama nchi yenu imewashinda msitafute sababu.....
Habari ndo hio....

Mauza uza,

..serikali kupitia walipa kodi wa Tanzania inapomsomesha mwanafunzi yoyote inakuwa na matarajio kwamba ataitumikia Tanzania baada ya kumaliza masomo yake.

..hao Wachina,Wahindi, etc wanaochukua uraia wa Marekani, halafu wanasoma bure, na baadaye kuutupa uraia huo na kurudi kwao, wamefanya udanganyifu. sasa Wamarekani na Waingereza wanaweza wasilalamike kwasababu wanauwezo mkubwa wa kifedha.

..kwa Tanzania kumsomesha mwanafunzi chuo kikuu, halafu asitumikie nchi yetu, kwa kweli ni hasara kubwa sana.

..hao Wanyarwanda wangekuwa wamesomeshwa na serikali ya Rwanda, au UN kama wakimbizi, na baadaye kurudi Rwanda kutumikia nchi yao, sidhani kama kuna Mtanzania yeyote angelalamika.

..tatizo ni kwamba hawa Wanyarwanda muda wote wako hapa walikuwa wakijidai ni Watanzania.

..kuna raia wengi tu wa mataifa mbalimbali ambao walifanyakazi Tanzania ktk nafasi nyeti. watu kama Herbert Chitepo[toka Zimbabwe] aliyekuwa DPP, au Chief Justice Georges toka Trinidad. lakini wote hawa hawakuficha asili zao na baadaye kuondoka kinyemela na kuibukia makwao.


NB:

..inaelekea kuna wengine hamfahamu kashfa iliyotokea Wizara ya Mambo ya Nje.

..serikali ya Rwanda ilimteua Balozi Bandora "Mtanzania" kuwa balozi wake Ujerumani.

..Balozi Bandora aliwahi kuwa msaidizi wa OAU SG Salim Salim, Mkuu wa Idara Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Nigeria.
 
Lakini pamoja na yote haya yaliompata Ulimwengu mbona yeye hajataka kurudi Rwanda ili akapate post nzuri n kubwa toka kwa Kagame???Lazima tukubali Ulimwengu ni mzalendo kuliko hata wazawa wengine.
 
Haya mambo ni kama ushirikina vile. Yaani watu wanaogopa vivuli. Hakuna kitu kama hima empire. Hakuna kitu kama conspiracy ya pamoja ya kikundi fulani kutawala eneo hili.

Mawazo kama haya ndo yaliyosababisha mauaji ya kutisha Rwanda. Haya mawazo bado tunayo kwani ushirikina na kuamini katika nguvu zisizoonekana ndiyo hasa tatizo letu kubwa. The moment tutakapoanza kuyaangalia matatizo yetu kama yanasababishwa na sisi wenyewe hapo ndo tutakapopona huu umaskini uliotopea.

Haya madudu ya conspiracy za makabila, kuwa makabila fulani wako organized huwa yanatumiwa sana na wanasiasa mufilisi. Tribal kings wa Kenya wanaendelea kupeta kwa conspiracy stories kama hizi.

Anyway ukienda mitaani huko uswahilini kuna watu wanaamini kuwa wapemba wako organized sana huwa wanasaidiana na wanakaa vikao vya siri kuchangiana. Vile vile kuna maeneo watakwambia wachagga ni kiboko. Kabila jingine ukijenga duka likaendelea wanakuvunjia wanakuibia halafu wanawagawia ndugu zao. Labda haya mambo huwa hatuyafuatilii vizuri mitaani, lakini yapo.

Jambo moja katika haya yote mara nyingi yanaanzishwa na watu mufilisi. Kwa mfano akitokea mmatumbi akafukuzwa kazi TRA, akirudi umatumbini hatasema nimefukuzwa kazi sababu ya incompetence. Atawaambia wenzie kuwa pale wachagga wana rule. Ukiwa si mchagga umekwisha.

Haya mambo yanasemwa dhidi ya wahindi, waarabu, n.k. Kosa lenu muwe minority mahala fulani na muonekane mmefanikiwa. Basi.

Lakini ukweli mmoja ni kuwa mara nyingi wahamiaji mahala popote huwa wana-excel kuliko indiginous. Hili likitokea, conspiracy huwa ndo solution ya indiginous. Lengo ni kuwaangamiza hao wanaoonekana wanafanikiwa.

Mawazo kama haya ndo yalifanya Hittler awaangamize wayahudi, mauaji ya kimbari Rwanda na Burundi, Darfur, n.k.

As long as bado tunaamini mambo bila kufanya critical thinking, tutaendelea kuwaona wageni ndo shida!!
 
Mbona wako wengu tu mkuu.City Engineer wa Kigali aliyekuwa Engineer wa Manispaa hapa Dar es salaam amesoma UDSM,kuna Mawaziri si chini ya wawili waliokuwa wanafanya kazi baada ya kusoma hapa UDSM wako kwao.
Nadhani mtakumbuka na scandal ya Col Rusimbi jeshini.
hii scandal ya Col rusimbi ipi? tunaomba darasa please
 
hivi col rusimbi alikuwa mtutsi!!??? namkumbuka sana yeye na maj shaban[or something like that]...walifukuzwa jeshi na amiri jeshi mkuu...kwa kosa la kufanya conspiracy kwenye ajira za jeshi ikiwemo vitendo vya rushwa
 
Lakini pamoja na yote haya yaliompata Ulimwengu mbona yeye hajataka kurudi Rwanda ili akapate post nzuri n kubwa toka kwa Kagame???Lazima tukubali Ulimwengu ni mzalendo kuliko hata wazawa wengine.

Lazima tukubali ukweli Ulimwengu ni mtanzania pure just ana asili ya Burundi/Rwanda.Kama alikuwa anapata pesa na support toka kwa Kagame kulikuwa na ugumu gani kukimbilia huko na kuishi maisha ya raha mustarehe???kwa nini alikubali kuomba tena uraia na kujaza mikaratasi kibao wakati alikuwa na short cut ya kupata post nzuri sana na pesa bweleleee??Huyu ni mtanzania mwenzetu tuache propaganda za kizushi...wangapi ni wandereko,wanyamwezi,wasukuma,wachaga n.k na bado ni mafisadi kupindukia???UTANZANIA /UZALENDO SIO KABILA WALA RANGI.......ni uchungu wa nchi yako thats it.No matter asili yako or where u r coming from.Tuache huu ujinga wa ukabila/rangi..Hautusaidii.
 
Mkuu, hayo unayo yasema ni kweli kabisaaaa.. nikushuhudie tu kwa macho yangu kwenye myaka ya 1987-90 kule mjini Bukoba, kulikuwa na vijana wengi wahima wakisoma katika shule za secondary nyingi zikiwemo Ihungo, Kahororo, Bukoba sec, Rugambwa, Nyakato, na Ntungamo major seminary na nyinginezo around hapo, waliweza kujiorganise wakasingizia kwamba wana kikundi cha ngoma sijui.. wakatengeneza event ya kuwakutanisha na wakapewa ruhusa mashuleni, kumbe huko wakaenda kujiorganise na kuwaambia vijana wao huko mashuleni wasome vipindi gani kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kushika nchi huko kwao..

Na kweli ndivo ilivo kuwa wengi wakaacha masomo ya sayansi japo walikuwa nauwezo sana wakachukua masomo ya arts, kwa mkakati mahsusi wa kwamba baada ya kuchukua nchi wanaenda kufanya kazi fulani!

There after, kwenye myaka ya 2000 nilibahatika kuonana na jamaa mmoja alinishuhudia ukweli wa mipango yao, kwamba kweli walirudi kwao na kweli walishika hizo nyadhifa. Sipendi kwenda ndani zaidi mkuu, lakini ni ukweli mtupu, hawa jamaa wako well coordinated na determined!

Na niwabaguzi wa kufa, Yaani wadada wao ni warembo sana, lakini ukimuoa, kaa tayari hata kaa azae nawewe, atakuja mgeni hapo kwenu atadaiwa ni binamu/kaka/mjomba huyo ndo atakuzalishia watoto wenye pua ndefu utakao walea ukidhani wa kwako! na atahakikisha unasaidia kila jamaa mwenye pua ndefu atakaye kutana naye popote akidai ni 'mwenewachu' Ndugu yangu.

Well pengine si vyema kusema haya but ndo ukweli.
Sisi TZ nani anatuandalia viongozi? Mafisadi? I think you need to aim above the mark in order to hit the mark. Kama hatutaki kujiorganioze, ili kushika hatamu za uongozi leo na baadae, mi naona dawa si kuwarudi watu wenye asili ya Rwanda. Tutachemsha bwana mana hiyo kazi tutakayojipa itakuwa yenye lawama kubwa kuliko kuwa ma mikakati ya kutayarisha viongozi sisi kama sisi.Ilivyo sasa where is the training ground for future leaders? UVCCM? Mi sioni!Au kule PCCB ambako walichukua young blood nyingi wakati wanaanza. Lakini wanaandaliwaje? Wawe waongo kuiita rushwa si rushwa mpaka bunge liamke kama Richmond?
 
Lazima tukubali ukweli Ulimwengu ni mtanzania pure just ana asili ya Burundi/Rwanda.Kama alikuwa anapata pesa na support toka kwa Kagame kulikuwa na ugumu gani kukimbilia huko na kuishi maisha ya raha mustarehe???kwa nini alikubali kuomba tena uraia na kujaza mikaratasi kibao wakati alikuwa na short cut ya kupata post nzuri sana na pesa bweleleee??Huyu ni mtanzania mwenzetu tuache propaganda za kizushi...wangapi ni wandereko,wanyamwezi,wasukuma,wachaga n.k na bado ni mafisadi kupindukia???UTANZANIA /UZALENDO SIO KABILA WALA RANGI.......ni uchungu wa nchi yako thats it.No matter asili yako or where u r coming from.Tuache huu ujinga wa ukabila/rangi..Hautusaidii.

Kwanini unasema lazima??!! wewe ni nani hadi uwalazimshe watanzania kukubali?? kama ni kibaraka anaefadhiliwa na mataifa ya nje ni wajibu wetu kujiridhisha kuhusu tabia yake...
 
Lazima tukubali ukweli Ulimwengu ni mtanzania pure just ana asili ya Burundi/Rwanda.Kama alikuwa anapata pesa na support toka kwa Kagame kulikuwa na ugumu gani kukimbilia huko na kuishi maisha ya raha mustarehe???kwa nini alikubali kuomba tena uraia na kujaza mikaratasi kibao wakati alikuwa na short cut ya kupata post nzuri sana na pesa bweleleee??Huyu ni mtanzania mwenzetu tuache propaganda za kizushi...wangapi ni wandereko,wanyamwezi,wasukuma,wachaga n.k na bado ni mafisadi kupindukia???UTANZANIA /UZALENDO SIO KABILA WALA RANGI.......ni uchungu wa nchi yako thats it.No matter asili yako or where u r coming from.Tuache huu ujinga wa ukabila/rangi..Hautusaidii.

Kwa hiyo mtu yoyote aingia Tanzania bila kibali? Una taka kusema kuwa mtu asiye Mtanzania apewe nafasi ambazo ni stahiki za raia mpaka sehemu nyeti za nchi? Kwa maneno yako basi hata mgeni utataka waje kuwa raisi wa Tanzania. Kuipenda Tanzania haikupi haki za uraia wa kitanzania. Unadhani nchi zingine wana ruhusu kila mtu tu awe raia? Mambo muhimu kama haya yakionglewa msi kimbilie kusema ubaguzi kwa sababu tu mnajua ni a sensitive issue. Ndiyo wale wote mtu aki tajwa fisadi kama siyo mweusi mna kimbilia kusema oh ubaguzi. Stop using discrimination as an excuse for everything..
 
Hebu mwangalieni sasa hivi anavyo watumia watu ambao anajua ni wadhaifu sana linapokuja suala la dini! anajua wao taifa baadae dini kwanza!
Watu hawa ni Issa Shivji Prof., Haroub Othman na sasa hivi kamvaa Masoud Kipanya;
Kwa wasiojua au wasikuwa na kumbukumbu nzuri huyu Masoud Kipanya alikuwa mchora katuni kwelnye gazet la BARAZAla kidini lililofungiwa kwa uchochezi na serikali, zile tabia zake za kwenye BARAZA hajaacha. Kama wewe ni mtu wa kutafakari angalia nyendo zake nyingi utamgundua, Mfano mzuri wa hivi karibuni hebu kuwa makini angalia alichokuwa anakifanya kwenye mchezo wa Maisha plus TBC1!
Sasa mzee Ulimwengu analitambua hilo, na sasa ameanza hata kumtajataja kwenye habari za mara kwa mara kama kijana mbunifu na mwenye akili!!!
Hiyo dini kwanza inaonekana siyo lengo lake kuu, anatumia tu kupata wafuasi, lengo lake ni hiyo RWANDESE AGENCIES INTERNATIOALE!
 
Watutsi, watutsi, watutsi,
kwa wale tunaowajua hawa jamaa huwa na agenda za kikwao hasa uroho wa kutawala. Lakini wasio watutsi nao si wana akili zao?? si wanaona kinachoendelea?? na wao si wanajizatiti? Mbona Burundi, wahutu wametawaliwa kwa muda mrefu na watutsi lakini imefika hatua wakasema haiwezekani, sasa wanawatawala watutsi.

Wala tusimuonee huruma Ulimwengu, mpaka wakafikia kumvua uraia vijana walikuwa wamemfanyia kazi kiasi cha kutosha na wakaona agenda zake ni zipi au nia yake ilikuwa ipi. Bado na wengine wenye malengo kama ya ulimwengu tunawasikia. Dawa ni kuwapeleka Idara ya uhamiaji.
 
Jamaa si tayari kasema kasikia mara mbili tatu kutoka kwa wakuu mtaani na akaileta hapa ili wenye data wamwage. Sasa mbona unataka kumsakama bila kosa au kosa lake hapa ni nini???? Au Ulimwengu kwenye awamu ya nne haguswi?????????????
Ulimwengu awamu ya nne aliianza kwa kuisifia sanaaa..aliwahi kumtaja muungwana (JK) kwenye mkutano mmoja kuwa ni raisi wa kwanza bongo kukemeaa rushwaa hadharaniii...wakati mwalimu aliwahi kumchapa viboko waziri wake hadharani..lol..

aliposhtukaa muungwana ni mtupu na amezungukwa na kambi ambayo jenerali haiingiii..alifyataaaaaaaaaaaaaaa..mpaka leo..

Jenerali ni mtu wa aina gani na malengo yepi??????? BWM alimjuliaaaa.
 
Hayo ya Ulimwengu ya RA.Kweli TZ inafanywa kichwa cha mwendawazimu.
 
Je na yule mke wake wa sasa anayeishi Afrika ya kusini ni mtutsi au mtanzania?
 
Just for the purpose of putting straight Jenerali's record naomba nimkosoe Mzee wa Mbuyu katika thread yake kwa hoja aliyojenga ili kuthibitisha uswahiba wa Jenerali na Mzee Mkapa. Mzee wa Mbuyu amesema Mzee Mkapa alikuwa MC katika harusi ya mtoto wa Ulimwengu,hii si kweli,Ulimwengu hajawahi kuozesha mtoto,binti yake mkubwa Sibongile alitangulia mbele ya haki kabla hajaolewa na ana vijana wengine wadogo tu. Kama ni kumsema tumseme mengine lakini sio hili.Kuhusu kunyang'anywa uraia siku hiyo walinyang'anywa watu wanne akiwemo Castico,Bandora,Jenerali na jamaa mmoja alikuwa CCM chairman Kagera.Tujiulize nini kisa hasa cha kuwanyang'anya uraia kwa pamoja na baadae kuwarejeshea uraia huo?Pili tujiulize ni viongozi wangapi nchi hii ambao wanajulikana kabisa kwamba kwamba asili yao si Tanzania na kwa mujibu wa sheria hawajahi kukana uraia wa nchi zao za asili na ni viongozi wakubwa nchi hii mbona hawaguswi au Mzee mzima Mkapa alikuwa hawajui? Wadau mnadhani Kambarage angekuwa hai Mkapa angethubutu kumnyang'anya Jenerali uraia?
 
..inasemekana Jenerali alikuwa kwenye timu ya Kikwete wakati wa kampeni za Uraisi za 95.

..baada ya Mkapa kushinda Jenerali akahamia kambi ya ushindi ya Mkapa.

..baada ya Mkapa kuingia Ikulu, akaanza kumzawadia Jenerali kwa kumteua mjumbe ktk Tume mbalimbali zilizokuwa na ulaji mzuri kwelikweli.

..wananchi wakaanza kulalamika kulikoni Jenerali ateuliwe kwenye kila Tume ya Raisi?

..Mkapa kwa kusikiliza malalamiko hayo akaacha kumpa ulaji Jenerali.

..wakati huohuo Mkapa akaanza kucheza dili za ulaji yeye mwenyewe na washirika wake wengine.

..Jenerali akaamua kumlipizia kisasi Mkapa kwa kuanza kumshambulia kwenye magazeti yake.

..Mkapa naye akachukia akiona kwamba Jenerali hana shukurani kwa ulaji wote aliokuwa akimpa. kwa hiyo Mkapa akaamua kumlipua Jenerali ktk masuala yake ya uraia.

NB:

..kwa upande mwingine Jenerali Ulimwengu ni nani?

..hili jina halina tofauti na majina tunayotumia hapa Jamii Forums. inashangaza kidogo.

..amezaliwa wapi, amesomea wapi?

..amefanya kazi gani tangu amalize shule na ktk taasisi zipi?
Joka Kuu,jina halisi la ulimwengu ni Bwana Twaha Khalfan.Jina la Jenerali Ulimwengu alilichukua ukubwani kwa sababu enzi za ujana wake ndo kulikuwa na vuguvugu la mapinduzi Afrika na yeye alikuwa ni mwanaharakati.Kumbuka siku ya uhuru Desemba,09,1961 wakati bendera ya Tanganyika inapandishwa mjini Bukoba Ulimwengu ndiye aliyesoma utenzi wa Uhuru,upo hapo?
 
Last edited:
Just for the purpose of putting straight Jenerali's record naomba nimkosoe Mzee wa Mbuyu katika thread yake kwa hoja aliyojenga ili kuthibitisha uswahiba wa Jenerali na Mzee Mkapa. Mzee wa Mbuyu amesema Mzee Mkapa alikuwa MC katika harusi ya mtoto wa Ulimwengu,hii si kweli,Ulimwengu hajawahi kuozesha mtoto,binti yake mkubwa Sibongile alitangulia mbele ya haki kabla hajaolewa na ana vijana wengine wadogo tu. Kama ni kumsema tumseme mengine lakini sio hili.Kuhusu kunyang'anywa uraia siku hiyo walinyang'anywa watu wanne akiwemo Castico,Bandora,Jenerali na jamaa mmoja alikuwa CCM chairman Kagera.Tujiulize nini kisa hasa cha kuwanyang'anya uraia kwa pamoja na baadae kuwarejeshea uraia huo?Pili tujiulize ni viongozi wangapi nchi hii ambao wanajulikana kabisa kwamba kwamba asili yao si Tanzania na kwa mujibu wa sheria hawajahi kukana uraia wa nchi zao za asili na ni viongozi wakubwa nchi hii mbona hawaguswi au Mzee mzima Mkapa alikuwa hawajui? Wadau mnadhani Kambarage angekuwa hai Mkapa angethubutu kumnyang'anya Jenerali uraia?

Ndugu yangu, hizi ni tetesi zimesikika kwa watu wanaomfahamu vizuri tu mheshimiwa huyu...,kama wewe ulivyodai kumfahamu. Ila kuhusu aswahiba nina uhakika nao na ulianza kitambo enzi za mwalimu walipokuwa wakimdanganya mwalimu kuwa ni wafuasi wake wazuri!
Kama wewe ndiyo mkweli au la...ngoja tuendelee kupata michango mkuu....
 
Back
Top Bottom