Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Mzigo huu unapatikana kwa bei Poa. 230,000/- Wahi sasa. Ni "Strong SRT 4922A" new model. Contact Me on 0715-240140.

Daa! hii kitu huwa naivutia subira. Ubaya haina punguzo la Pasaka, Krismas, Sababa, Nanenane wala Siku ya walalahoi. Ngoja niendelee kusubiri.
 
kama umefanikiwa kupata Aljazeera kwa signal ya juu kabisa, basi uki blind scan unaweza kupata chnls nyingi za India,na Korea, kuna baadhi zina Indian movies, ila wakt mwingine zipo ON na OFF.

Aljazira nilipata signal ya juu {85-90}. kwakuwa rcva yangu haina blind scann,Nilieka tp manual na nikapata channels zaid ya 20 lakini sita pekee ndio zinafanya na hizo zingine zote zina symbol ya($) na ukijaribu kuplay hazifanyi
 

hapana, ngoja nikurekebishe.
Siyo kuwa receiver yeyote ya mpeg4 = na mpeg2
na pia dvb-s = dvb 1
hapo ni kuwa channel zozote zinzzokamata kwenye mpeg 2 pia huukamata katika dvb-s hivyo ni
mpeg 2 = dvb- s
Na tena channel zinazokamata katika mpeg 4 vilevile hukamata na kwenye dvb-s2 hivyo
mpeg4 = dvb- s2
 

salaam wandugu,ilo dish naelekeza jua linapo zamia au linapo chomozea ili kuipata huyo ndege Yahsat 1? ,pia naomba kujuzwa ni dish la ku la cm ngapi ili niipate Eutelsat 8Weast A? naombakuwasilisha wanajopo.......wasalaaam...(NIPPO DAR-ES-SALAAM,CHANIKA KARIBU NA BUYUNI)
 
Natamani kupata channel za rwanda,burundi-urundi,drc,zimbabwe,botswana,zambia na malawi jamani nisaidieni.
 
Kwa urahisi ni hivi: Mpeg4= wake na mpeg2=wanawake. Ukiwa na mlinganyo huo ni sahihi kusema wake (wanawake walioolewa) wote wa watu ni wanawake ila si kweli kwamba wanawake wote ni wake za watu. Kwa mtazamo huu ndugu josephjul40 bado kuna shughuli kubwa ya kuendelea kueleza mambo ya msingi kabla watu hawajaweza kutega nyungo. Kutegeza ungo inaweza kuwa rahisi sana (kwani watu wengi hufanya kwa mazoea) Layman anaweza kujua kuwa ALU (Artemether Lumefantrie) inatibu malaria lakini hawezi kujua ni kwa namna gani inatibu. Ndivyo ilivyo na kwa watu wanaoweza kutega nyungo kwa mwelekeo fulani. Kama kuna yeyote ambaye haamini ninachosema awe wa kwanza kujibu swali hili : NI KWA NINI UNGO WA PACKAGE YA AZAM UNAELEKEZWA MAGHARIBI WAKATI SATELAITI YAKE IPO MASHARIKI? (NI MUHIMU UNITAJIE SATELAITI HII).Fatilia kuona majibu yatakayoletwa hapa.
 
Habari wadau!!! Leo nimejaribu kutafuta Yahsat 1A @52.5 East, kutumia dish ya 6ft lakini kwa bahati mbaya sikufaulu.Frequence zenye nimetumia ni hizi(11900H27500) (11938H27500) (11766V27500) Iwapo shida ni frequence naomba mnijulishe maana nimekwama kabisaaa!
 
Bwana hassanM unatakiwa pia utuambie ni wapi unapatikama (location) ili kupata msaada wa kutosha. Swali la kujifunza uliuelekeza wapi ungo wako?
 
Last edited by a moderator:
Bwana hassanM unatakiwa pia utuambie ni wapi unapatikama (location) ili kupata msaada wa kutosha. Swali la kujifunza uliuelekeza wapi ungo wako?

Mimi niko mombasa; kwa sasa napata local channels kwenye Intelsat 906 @64.2E Pia napata channels zote za Intelsat 7/10 @68.5E. Hapa kwa intel 7/10, nilieka LNB mbili C @ Ku band. C band nilipata 6 channels na Ku band nilipata 75 channels. hivyo nipo na lnb tatu kwa dish moja na zina work vizuri sana. Lakini sasa nataka kuhamia Yahsat 1A @52E ambayo nimeona iko na best channels kuliko intel 7/10. Mkuu, kulingana na baadhi ya post nilipata kujua pia kuwa Yahsat ipo the same position na intel 906, hivyo nakatoa LNB zote nikabaki na moja ya Ku ndio niwe more accurate lakini niliambulia patupu. Kufikia hapa naona itakuwa rahisi sana kunipa usaidizi maana nimeeleza hali halisi ilivyo ndungu.Itakuwa vyema zaid kama nitasaidika na frequence zenye na uakika; natumia DVB-S/Mpeg 2 Receiver. siku njema!!
 
Last edited by a moderator:

samahani, kuuliza ila msinichekee, Azam reciver ni mpeg2/dvb-s
 
samahani, kuuliza ila msinichekee, Azam reciver ni mpeg2/dvb-s

Azam ni MPG4/dvs-2, kama gari azam ni basi linalobeba abiria wengi kuliko Costa (mpg2/dvs). Mpg4/dvs-2 inauwezo wa kufungua channel za mpg2/dvs mradi zisiwe za kulipia, na zikiwa za kulipia iwe na account husika mf dstv. Receiver ya mpg2 /dvs haina uwezo wa kufungua channel za mpg4 hata zikiwa za bure
 
Wadau asanteni kwa shule nzuri hii, ninapata huduma ya azam TV kwa maana ya dish na kin'gamuzi, sasa nataka kupata na channel za soka hasa EPL je naweza kuzipata bila kupoteza za local, msaada tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…