Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Mzigo huu unapatikana kwa bei Poa. 230,000/- Wahi sasa. Ni "Strong SRT 4922A" new model. Contact Me on 0715-240140.

Daa! hii kitu huwa naivutia subira. Ubaya haina punguzo la Pasaka, Krismas, Sababa, Nanenane wala Siku ya walalahoi. Ngoja niendelee kusubiri.
 
kama umefanikiwa kupata Aljazeera kwa signal ya juu kabisa, basi uki blind scan unaweza kupata chnls nyingi za India,na Korea, kuna baadhi zina Indian movies, ila wakt mwingine zipo ON na OFF.

Aljazira nilipata signal ya juu {85-90}. kwakuwa rcva yangu haina blind scann,Nilieka tp manual na nikapata channels zaid ya 20 lakini sita pekee ndio zinafanya na hizo zingine zote zina symbol ya($) na ukijaribu kuplay hazifanyi
 
Usipokuwa makini na mwangalifu na ugonjwa wa ASAS unaweza kuwa kama bendera mtu akikuambia tu huku kuna chnl tayari utaanza kugeuza ungo wako bila sababu ya lazima na pengine chnl unayoitafuta haipo katika eneo unaloishi. Tujifunze kutafuta kwanza uhalisia wa habari kabla hatujaanza kugeuza nyungo zetu.

Aidha napenda pia kusema kwa mara nyingine tenakuwa rcva yoyote ya mpeg4 ni mpeg2 na rcva yoyote ya DVBS-2 ni DVBS-1 na kinyume chake si sahihi

hapana, ngoja nikurekebishe.
Siyo kuwa receiver yeyote ya mpeg4 = na mpeg2
na pia dvb-s = dvb 1
hapo ni kuwa channel zozote zinzzokamata kwenye mpeg 2 pia huukamata katika dvb-s hivyo ni
mpeg 2 = dvb- s
Na tena channel zinazokamata katika mpeg 4 vilevile hukamata na kwenye dvb-s2 hivyo
mpeg4 = dvb- s2
 
Mazee kama una ungo wa ft 8 unaweza kupata Yahsat1 na local chnls zote bila shida yoyote. Yahsat kuna chnls nyingi za movie SD NA HD, KAMA VILE MBCs zote, Dubai zote, Fox, gem,Discovery, star movies, etc ni patamu hata kuliko E7wa. Yahsat ipo karibu sana NSS 12,ILIPO K24 YA KENYA. UNANYANYUA DISH KIASI CHA 4CM YAANI UNAACHA MUHIMILI KUZAMA NDANI 4CM. KWA LNB ULIYO NAYO UNAPATA BEAM ZOTE WEST NA EAST. UTAENJOY ILI MBAYA.

salaam wandugu,ilo dish naelekeza jua linapo zamia au linapo chomozea ili kuipata huyo ndege Yahsat 1? ,pia naomba kujuzwa ni dish la ku la cm ngapi ili niipate Eutelsat 8Weast A? naombakuwasilisha wanajopo.......wasalaaam...(NIPPO DAR-ES-SALAAM,CHANIKA KARIBU NA BUYUNI)
 
Natamani kupata channel za rwanda,burundi-urundi,drc,zimbabwe,botswana,zambia na malawi jamani nisaidieni.
 
hapana, ngoja nikurekebishe.
Siyo kuwa receiver yeyote ya mpeg4 = na mpeg2
na pia dvb-s = dvb 1
hapo ni kuwa channel zozote zinzzokamata kwenye mpeg 2 pia huukamata katika dvb-s hivyo ni
mpeg 2 = dvb- s
Na tena channel zinazokamata katika mpeg 4 vilevile hukamata na kwenye dvb-s2 hivyo
mpeg4 = dvb- s2
Kwa urahisi ni hivi: Mpeg4= wake na mpeg2=wanawake. Ukiwa na mlinganyo huo ni sahihi kusema wake (wanawake walioolewa) wote wa watu ni wanawake ila si kweli kwamba wanawake wote ni wake za watu. Kwa mtazamo huu ndugu josephjul40 bado kuna shughuli kubwa ya kuendelea kueleza mambo ya msingi kabla watu hawajaweza kutega nyungo. Kutegeza ungo inaweza kuwa rahisi sana (kwani watu wengi hufanya kwa mazoea) Layman anaweza kujua kuwa ALU (Artemether Lumefantrie) inatibu malaria lakini hawezi kujua ni kwa namna gani inatibu. Ndivyo ilivyo na kwa watu wanaoweza kutega nyungo kwa mwelekeo fulani. Kama kuna yeyote ambaye haamini ninachosema awe wa kwanza kujibu swali hili : NI KWA NINI UNGO WA PACKAGE YA AZAM UNAELEKEZWA MAGHARIBI WAKATI SATELAITI YAKE IPO MASHARIKI? (NI MUHIMU UNITAJIE SATELAITI HII).Fatilia kuona majibu yatakayoletwa hapa.
 
Habari wadau!!! Leo nimejaribu kutafuta Yahsat 1A @52.5 East, kutumia dish ya 6ft lakini kwa bahati mbaya sikufaulu.Frequence zenye nimetumia ni hizi(11900H27500) (11938H27500) (11766V27500) Iwapo shida ni frequence naomba mnijulishe maana nimekwama kabisaaa!
 
Habari wadau!!! Leo nimejaribu kutafuta Yahsat 1A @52.5 East, kutumia dish ya 6ft lakini kwa bahati mbaya sikufaulu.Frequence zenye nimetumia ni hizi(11900H27500) (11938H27500) (11766V27500) Iwapo shida ni frequence naomba mnijulishe maana nimekwama kabisaaa!
Bwana hassanM unatakiwa pia utuambie ni wapi unapatikama (location) ili kupata msaada wa kutosha. Swali la kujifunza uliuelekeza wapi ungo wako?
 
Last edited by a moderator:
Bwana hassanM unatakiwa pia utuambie ni wapi unapatikama (location) ili kupata msaada wa kutosha. Swali la kujifunza uliuelekeza wapi ungo wako?

Mimi niko mombasa; kwa sasa napata local channels kwenye Intelsat 906 @64.2E Pia napata channels zote za Intelsat 7/10 @68.5E. Hapa kwa intel 7/10, nilieka LNB mbili C @ Ku band. C band nilipata 6 channels na Ku band nilipata 75 channels. hivyo nipo na lnb tatu kwa dish moja na zina work vizuri sana. Lakini sasa nataka kuhamia Yahsat 1A @52E ambayo nimeona iko na best channels kuliko intel 7/10. Mkuu, kulingana na baadhi ya post nilipata kujua pia kuwa Yahsat ipo the same position na intel 906, hivyo nakatoa LNB zote nikabaki na moja ya Ku ndio niwe more accurate lakini niliambulia patupu. Kufikia hapa naona itakuwa rahisi sana kunipa usaidizi maana nimeeleza hali halisi ilivyo ndungu.Itakuwa vyema zaid kama nitasaidika na frequence zenye na uakika; natumia DVB-S/Mpeg 2 Receiver. siku njema!!
 
Last edited by a moderator:
hapo ni hivi
satellite; Azerspace 1
position; 46 east
fq 11169H 30000
MPEG-2/ DVB-S ONLY

PIA
Eutelsat 7 at 7 east
11492v 30000
MPEG-2/DVB-S PEKEE

Madish ni kuanzia ft 4 kuendelea
ila hapo eutelsat 7 at 7 east nimejaribu kwa kutumia dish la azam chenga tu haipo, ila kuna jamaa angu ameipata hiyo chanel kwa dish la ft 6 46east
na pia kuzingatia hizo receiver
kwenye MPEG-4 Ni chenga tupu mpaka mpeg-2/dvb-s

samahani, kuuliza ila msinichekee, Azam reciver ni mpeg2/dvb-s
 
samahani, kuuliza ila msinichekee, Azam reciver ni mpeg2/dvb-s

Azam ni MPG4/dvs-2, kama gari azam ni basi linalobeba abiria wengi kuliko Costa (mpg2/dvs). Mpg4/dvs-2 inauwezo wa kufungua channel za mpg2/dvs mradi zisiwe za kulipia, na zikiwa za kulipia iwe na account husika mf dstv. Receiver ya mpg2 /dvs haina uwezo wa kufungua channel za mpg4 hata zikiwa za bure
 
Wadau asanteni kwa shule nzuri hii, ninapata huduma ya azam TV kwa maana ya dish na kin'gamuzi, sasa nataka kupata na channel za soka hasa EPL je naweza kuzipata bila kupoteza za local, msaada tafadhali.
 
Back
Top Bottom