Mkuu swali lako ni zuri sana na kulijibu linataka kituo na nitatoa mchango wangu kwa kadiri ya upeo wangu...Kitu kikubwa na cha mwanzo unapofunga Dish ni lazima ujue south ni wapi na kama ulivyo toa mfano kama satelite unayotaka iko 36°W au 68.4°E utafika vipi?...ingawa positions zote mbili hakuna satelite yeyote sijui kwa sababu gani za kiufundi.
Labda tuanze namna ya kuipata south,kimsingi unatakiwa kutumia compass au kuna option ambayo nadhani ina wepesi kwa wengi,ikifika saa sita kamili mchana ukiwa juani kivuli chako kinakuwa south nahapo ndio 0° ..sasa hatua ya pili utapata vipi position tunayoitaka.
Hatua ya pili utatumia saa kuanzia saa sita kamili (12:00) kulia east-kushoto west na mshale wa kwanza wa dakika ni 6° kwa maana hiyo utakwenda na mtiririko huo(ukienda east au west) 6° 12° 18 24° 32° 38° 42° 48° na kundelea.