Ulimwengu wa Haki Sawa 50/50 hakuna kulipa Faini ukimpa Mwanamke mimba au mtoto

Ulimwengu wa Haki Sawa 50/50 hakuna kulipa Faini ukimpa Mwanamke mimba au mtoto

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
ULIMWENGU WA HAKI SAWA 50/50 HAKUNA KULIPA FAINI UKIMPA MWANAMKE MIMBA AU MTOTO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Oooh! Umemzalisha mtoto wetu, lipa sijui FAINI, sijui lipa vitu gani. Sasa Sisi Watibeli tukitaka kuonyeshwa huyo Binti aliyezalishwa analetwa Mwanamke MTU mzima kabisa zaidi ya miaka 20 Huko. Come on!

Baadhi ya sheria za kimila zinautia aibu Uafrika. Zinazidi kumfanya muafrika aonekane mfano WA binadamu na si binadamu. Hayo ni mawazo finyu.

Wazazi ndio Tu/mnatakiwa FAINI Kwa kushindwa Kulea Binti zenu/zetu. Unashindwa Kulea Binti yako ajitunze na kama anashindwa kujitunza basi Ajue kujikinga na mimba alafu unakuja kulipisha Watu FAINI. Hatutalipa! Nakuambia hatutalipa! Na Sisi Watibeli Binti zetu wakipata mimba hatutadai hata Mia mbovu wala chochote. Ni Makosa yetu kushindwa kuwafunza Binti zetu Kwa nini tuwalipishe watu wengine Kwa uzembe wetu.

ATI umekutana na Binti chuo kikuu au huko mjini mpo kwenye mambo yenu. Alafu imetokea mimba alafu baadaye ATI kuna Watu wanakuambia ulipie. Utafikiri huyo Binti ni zuzu, mtoto Mdogo, au hamkuwa na mapenzi yenu.

Kama ni FAINI basi Wote mlipie, namaanisha Mwanamke aliyebeba mimba na Mwanaume aliyempa hiyo mimba. Hapo itakuwa sahihi Kwa sababu wote wamevunja Mila na desturi.

Wazazi tufundisheni Watoto wetu. Wote wakike na Wakiume. Binti akipewa mimba ni aidha kukosa kwake maadili au kosa la Walezi wake kuzembea sehemu Fulani.
Sio kosa liwe tuu Kwa kijana aliyempa mimba.

Hiyo miaka tumeshatoka, na kamwe hatutorudi.

Sisi sio kabila moja, Sisi hatutoku sehemu moja. Ikiwa tumeamua kuwa pamoja kama wanadamu basi eleweni kuwa haya ndio Matokeo yenyewe.

Sio mijitu inakuja kusema oooh sijui tunadharau tamaduni na Mila. Mila ndio ukabila wenyewe. Hivi tukisema tufuate mila na desturi hapa tutakaa? Msukuma ataoana na Mchaga? Au Mluguru na Mhaya watapanga? Thubutu! Mila ndio hizo.

Mnajifanya mnapenda Mila alafu mkiambiwa Ndoa za mitara mnatoka nduki, mkiambiwa urithiwe na Ndugu WA Mumeo hutaki. Hivi mmleogwa ninyi?

Tumeamua kuifanya dunia Babeli naam ndio machafuko, mvurugano.
Tunategemea nini kama sio hivi!
Sisi sio jamii moja, Ila kisiasa Sisi ni jamii moja. Sisi sio kabila moja na wala sio damu moja.

sisi Watibeli tupo mbele ya muda. Ninyi mlikurupuka. Ndio maana hamjui hata nini chakufanya. Mnaleta sheria za kizamani Kwa Ulimwengu wa kisasa.
mnaleta mambo ya Mila Kwa Watu wenye Mila mchanganyiko.

wewe ukitaka mambo ya Mila na desturi yafuatwe kaoe au kuolewa na kabila lako Huko. Sisi tutakushinda mapema Mno.
Mila zisizo na mantiki Sisi hatuzifuati, Mila za mawazo finyu hatuzifuati Sisi.

Hatuna mizimu wala Ndugu yake matambiko. Hatuamini katika mambo ya laana za mababu Kwa sababu Sisi hatuamini katika Watu waliokwisha Kufa.
Kwanza Sisi wenyewe ni mchanganyiko wa makabila. Hatumilikiwi na kabila lolote lile na kamwe hatujitambulishi na ukabila Sisi.

Binti zetu hawazalishwi Ila wakibeba mimba wanaamua Kwa utashi wao. Hivyo kamwe hatuwalipishi Vijana waliowapa mimba Kwa sababu tunajua Binti zetu walikuwa na uwezo wa kutozibeba hizo mimba Ila Kwa mapenzi Yao wameamua.

Utibeli ni Upendo, ukweli, Haki na Akili. Mambo yote yatapimwa katika mambo hayo manne. Jambo lolote lisilo na upendo au Haki au mantiki au ukweli Hilo Watibeli hatutalifuata.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unazungumziaje suala la kijana kufungwa jela kwa kumpa mimba bini flani 'ati' kisa ni mwanafunzi??
 
Mila hizi za Kuafrika ndiyo zinazomdumaza Mwanamke halafu wanalialia eti mfumo dume. Hawataki kuziacha sababu wanaona kama vile zinawapa ahueni na ulinzi kumaisha.

Ni sawa na viti maalym, ni utaratibu wa kumnyanyapaa sana Mwanamke unaofanya itafsirike kuwa uanamke ni ulemavu na hivyo kuhitaji uangalizi na upendeleo maalum.

Wanafurahia utaratibu huo wa viti maalum sababu unakuja na marupurupu, heshima nyingi na nafasi za juu mdiyo maana kamwe hawaupigii kelele kulalamika kuwa ufutwe. Hata wale wanaojiona wanaume kwa kuwasaga wenzao nao wanakimbilia viti maalum vya wanawake sababu ni utaratibu wenye fursa nyingi ndani yake.
 
Unazungumziaje suala la kijana kufungwa jela kwa kumpa mimba bini flani 'ati' kisa ni mwanafunzi??
Kama amebaka afungwe bila kujali umri wa mwanamke.

Kama ni chin ya umri wa kujitambua pia ni ruhusa Kufungwa. Ingawaje umri wa kujitambua ni mtambuka kwani Watu wanatofautiana.

Ila Chini ya miaka 18 ni umri sahihi wa MTU kufungwa.

Kwani itahesabika umembaka kwani Hana Akili ya kujitambua na kujua Jambo zuri na Baya Kwa Ukubwa wake
 
Mila hizi za Kuafrika ndiyo zinazomdumaza Mwanamke halafu wanalialia eti mfumo dume. Hawataki kuziacha sababu wanaona kama vile zinawapa ahueni na ulinzi kumaisha.
Ni sawa na viti maalym, ni utaratibu wa kumnyanyapaa sana Mwanamke unaofanya itafsirike kuwa uanamke ni ulemavu na hivyo kuhitaji uangalizi na upendeleo maalum.
Wanafurahia utaratibu huo wa viti maalum sababu unakuja na marupurupu, heshima nyingi na nafasi za juu mdiyo maana kamwe hawaupigii kelele kulalamika kuwa ufutwe. Hata wale wanaojiona wanaume kwa kuwasaga wenzao nao wanakimbilia viti maalum vya wanawake sababu ni utaratibu wenye fursa nyingi ndani yake.

Watu wanapenda kuvutia upande wao. Hawaangalii Haki, ukweli, upendo na Akili.

Wanasema Watu hawafuati Mila na desturi Wakati moja ya Mila na desturi ni ukabila. Kwamba kila kabila lifuate desturi zake. Sasa nauliza kila kabila likifuata desturi na Mila zake humu tutakaa?

Nani anaamua Mila Hii ni potofu na hii sio potofu? Hapo ndipo Watibeli tunapopita Katikati yao
 
Back
Top Bottom