Simulizi ya kweli inayonihusu mimi mwenyewe moja kwa moja.
Sehemu ya kwanza .
1. Namna majini walivyoshiriki katika makuaji yangu .
Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikishuhudia vivuli vilivyokuwa vikinifata kila nilipokwenda, kiukweli nilikuwa nikiogopa sana ingawa nilikuwa simwambii mtu yeyote hata mama na baba .
Siku zilizidi kwenda na kila siku nilikuwa nikijionea mambo mapya na hadi kufikia wakati nilikuwa nikiona watu wenye ndevu nyingi nyeupe, mavazi maupe sana waliokuwa wakinifata nyuma ninapotembea. Ndani ya kundi la watu hao kulikuwa na watoto waliokuwa sawa sawa na umri wangu kwa kipindi kile na kulikuwa na wanamama waliokuwa wakijitanda mavazi marefu ya kuburutika hadi chini .
Kiukweli nilikuwa nikijionea mambo mengi hadi ilifika wakati ninapopita mazingira ya hatari basi wazee wale hutokea ghafla na kunizuia kupita au kubaki maeneo hayo .
Siku moja nilipokuwa kijijini kwa kina bibi niliondoka na watoto wenzangu hadi mtoni (kisimani) , lakini ghafla tulipokuwa kando ya kisima hicho niliteleza na kuingia kisimani.
Mawasiliano yangu na wenzangu yalipotea lakini kwa mbali sana nilisikia kelele zao za kutaka kuniokoa bila mafanikio.
Nilizama hadi chini ya kisima nasikuwa najua kuogelea kamwe.
Nilitapatapa sana bila matumaini lakini ghafla nikamuona mzee mwenye ndevu nyingi nyeupe, kanzu na kitambaa cha kijani na pete kidoleni alitokea na kunishika mkono . Usoni sikumuona vizuri lakini alionekana kufurahi kuniona. Alinishika sana eneo la kichwani na kifuani huku akiniangalia kwa umakini mkubwa.
Nilimuona akipuliza kiganja chake cha mkono wa kulia na kisha kunifuta kwa mkono ule mwilini kisha alinisogeza hadi kando ya kisima na kuniweka kando nje ya kisima.
Basi nilipotoka nje ya kisima wenzangu wote sikuwaona walikimbia nyumbani kutoa taarifa. Nilifata njia ya nyumbani huku kwa mbali nikimuona yule mzee akinifata nyuma . Nilifika nyumbani na kukuta watu wa kijiandaa kunifata kisimani kuniokoa. Waliniuliza maswali mengi sana lakini sikujibu yote na hata sikuwaambia juu ya kuololewa kwangu na yule mzee.
SEHEMU YA PILI: Usiku wa siku ile ulivyokuwa baada ya kuzama kisimani.
Kusema kweli sitakaa nisahau usiku wa siku ile, kwani baada ya swala ya magharibi tuu kwenye moja ya muembe uliopo nyumbani nilimuona yule mzee yupo juu amekaa. na ilipofika muda wa saa moja hivi juu ya muembe ule nikaona kunawaka taa na sikuwa naona mtu mmoja tena badala yake niliona watu wengi.
" Dada ona kule juu unawaona wale watu .." nilimuuliza dada angu, lakini alinambia yeye haoni chochote na aliniamuru tuingie ndani .
Baba aliniwekea utaratibu kuwa baada ya swala ya saa mbili niwe nimeshalalala basi baada ya chakula cha usiku nikalala lakini usingizi ulikuwa hauji hata kidogo badala yake yule mzee nilimuona yupo pembeni yangu na wazee wengine na walikuwa mmoja anatoa adhana na takbira na wengine walikuwa wakiniangalia tuu .
Nilitaka kupiga kelele lakini nilinyamaza na nikawa namuita dada yangu .
Niliita sana lakini hakuitika ni kama alikuwa hanisikii. Muda wale wazee niliona nipo nao sehemu nje na pale nyumbani palikuwa ni kama sehemu yenye msikiti hivi au ukumbi fulani mkubwa.
Nikauliza hapa nipo wapi ? Dada Aisha yuko wapi? kijana wa makamo akanijia pembeni na kunambia dada yako yupo nyumbani na hapa ni kwa Ruhaby sultan na Kamal.
Palikuwa ni pazuri sana na nje niliona farasi wazuri sana weupe na wakubwa.
Miti niliyoona ilikuwa ni mtende na palikuwa na ngamia mkubwa sana aliyekuwa na marembo ya kijani na vita vya kijani pia .