SEHEMU YA TATU.
Ujaji wa majini nyumbani mara kwa mara.
Baada ya safari ya Yemen bado majini walikuwa wakija nyumbani mara kwa mara lakini kipindi hiki walikuwa wanapenda sana kukaa juu ya mti wa mkuyu.
Siku moja walikuja wengi sana, ilikuwa ni siku ya ijumaa lakini hawakukaa sana waliondoka, nilishaanza kuzoea hivyo nikawa najiuliza mbona hawakukaa sana leo ?
Pale nyumbani tuliendelea na shughuli zetu na maandalizi ya swalat jumaa. Mji wa Tanga siku za ijumaa misikiti hufurika watu wengi sana, katika moja ya msikiti wetu wa ijumaa upo karibu kabisa na njia ya kwenda Pangani tuliingia kwaajili ya ibada.
Pale mlangoni kulikuwa na mzee ameshika kitabu anasoma kumbukumbu zikanijia sio yule mzee wa kisimani kweli ?
Kuangalia ni yeye nilimtambua vyema na hakuna mwingine alimfahamu mzee yule .
Alionekana kuwa makini sana na usomaji wa kitabu alichonacho , basi nami nikakaa karibu kabisa na baba , kulia kwangu alikuwa baba na kushoto kwangu alikuwa rafiki yake baba maarufu kwa jina la sheikh Yusuf ambae alikuwa ndio imam wa msikiti.
Mara baada ya swalat kumalizika , mzee yule wa kijini nilimuona akimsogelea baba na kumpa mkono kumsalimia bila baba kujua yule mzee kuwa sio mtu ila ni jini. Kisha mzee yule alinipa mkono na mimi na cha kwanza kuangalia ilikuwa ni pete yake yenye kuvutia sana.
Na hapo alinitaarifu kuwa kwao ipo sherehe na wale waliokuja na kuondoka ghafla walifata maua ya mkuyu na hapo alinitajia kazi ya maua ya mkuyu ( atakaehitaji atasema nimtajie) .
Nb: ndani ya kisa hiki natumia sana jina la mzee na sio jina lake halisi sababu nimezoea sana kumuita mzee hivyo inakuwa vigumu kwangu kutumia jina lake halisi.
Basi aliniaga na kunambia anawahi Iran kwenye sherehe huko kwao kwenye mji wake .
Itaendelea