Simulizi ya kweli inayonihusu mimi mwenyewe moja kwa moja.
Sehemu ya kwanza .
1. Namna majini walivyoshiriki katika makuaji yangu .
Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikishuhudia vivuli vilivyokuwa vikinifata kila nilipokwenda, kiukweli nilikuwa nikiogopa sana ingawa nilikuwa simwambii mtu yeyote hata mama na baba .
Siku zilizidi kwenda na kila siku nilikuwa nikijionea mambo mapya na hadi kufikia wakati nilikuwa nikiona watu wenye ndevu nyingi nyeupe, mavazi maupe sana waliokuwa wakinifata nyuma ninapotembea. Ndani ya kundi la watu hao kulikuwa na watoto waliokuwa sawa sawa na umri wangu kwa kipindi kile na kulikuwa na wanamama waliokuwa wakijitanda mavazi marefu ya kuburutika hadi chini .
Kiukweli nilikuwa nikijionea mambo mengi hadi ilifika wakati ninapopita mazingira ya hatari basi wazee wale hutokea ghafla na kunizuia kupita au kubaki maeneo hayo .
Siku moja nilipokuwa kijijini kwa kina bibi niliondoka na watoto wenzangu hadi mtoni (kisimani) , lakini ghafla tulipokuwa kando ya kisima hicho niliteleza na kuingia kisimani.
Mawasiliano yangu na wenzangu yalipotea lakini kwa mbali sana nilisikia kelele zao za kutaka kuniokoa bila mafanikio.
Nilizama hadi chini ya kisima nasikuwa najua kuogelea kamwe.
Nilitapatapa sana bila matumaini lakini ghafla nikamuona mzee mwenye ndevu nyingi nyeupe, kanzu na kitambaa cha kijani na pete kidoleni alitokea na kunishika mkono . Usoni sikumuona vizuri lakini alionekana kufurahi kuniona. Alinishika sana eneo la kichwani na kifuani huku akiniangalia kwa umakini mkubwa.
Nilimuona akipuliza kiganja chake cha mkono wa kulia na kisha kunifuta kwa mkono ule mwilini kisha alinisogeza hadi kando ya kisima na kuniweka kando nje ya kisima.