Ulimwengu wa roho ni timilifu

Mkuu hebu vuta picha,kama raisi anazaliwa tausi na kwenda kuishi ikulu,je kina sie kalagabaho tutazaliwa nani maisha ya baadae???
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nzi bila shaka
 
Umeongea deep sana. ni wachache ambao watakuelewa
 
Hakunaga bahati mbaya hata Siku moja
 
Mkuu,ni kweli kwamba wanasiasa ni washirikina wakubwa,je wanaweza kwenda kwa fundi na kumtambua mtu mwenye FAKE ID(utambulisho wa kujificha jina kama hapa JF) na kisha wakampiga kipande au kumfata mpaka alipo na kumfanyia fitna?

Maana hawa jamaa kupita kwenye TV za asili jambo la kawaida tu!
 
Usiende kwa waganga! Usitafute ufumbuzi wa matatizo yako nje ya utaratibu wa kusahihisha uumbaji kama kusafisha nyota na kufanya kafara na matambiko
Laana za ukoo zinatokana na kutaka kusahihisha michoro yetu
Kwa hiyo tuwaachie wachawi wajinafasi?

Wewe kumbe bure kabisa
 
Uko sahihi na ndio maana wengi walioingia kwenye ushirikina kwa nia ya kutaka kutoka kimaisha mafanikio yao yamekuwa ni ya muda na mwisho wa siku wamejikuta wakirudi pale walipotoka au hali zao kuwa mbaya zaidi.
 
Anachosema mshana jr ni kweli kulingana na bible. Biblia imeelezea predestination/kukusudiwa kimbele. Ndio maana Mungu alisema shukuruni kwa kila jambo. Liwe jema au baya tushukuru tu kwa sababu yeye ndiye kila kitu.

Ukitaka kuangalia pre destination kwenye Maisha yako chunguza hili. Ulipokuwa mtoto mdogo wakati ukikua uliwa na kupanga mambo mengi nanpengine kufikiria ungekuwa nani baadaye. Ungeoa mke yupi, watoto fulani, nyumba fulani etc.
Lakini leo almost mambo sivyo yalivyo salaaleh! Mahali ulipo hukuwahi kupawazia, status uliyonayo hukuwahi kuifikiria kabla, mke, watoto, mali na maisha kwa ujumla siyo yale uliyowazia zamani. Hii inaashiria nini??? PREDESTINATION.
Tangu unakuja Duniani ulishapangiwa njia ya kupita na huwezi kuikwepa. Hapa chini ni mfano wa pre destination unaoongelewa na Biblia:
Waefeso 1:3-5
[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
[4]kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
[5]Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.

Kwa hiyo ukijiona ni mkristo leo hujifanyi hivyo, bali ulishakusudiwa hilo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Maana yake alikujua na kukuchangua kimbele ili uwe hivyo. Kwakuwa anajua mwisho kabla ya mwanzo ndio maana alikuwekea njia ya wewe kufikia kile alichokukusudia. Hilo ni kweli kabisa
 
Yeremia 29: 11

"Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho"

English:" I know the plans I have for you...."

I have for you. ... Yani alishapanga, mipango IPO siku nyingi sana
 
Usiende kwa waganga! Usitafute ufumbuzi wa matatizo yako nje ya utaratibu wa kusahihisha uumbaji kama kusafisha nyota na kufanya kafara na matambiko
Laana za ukoo zinatokana na kutaka kusahihisha michoro yetu
Kaka mimi sijawahi kwenda kwa waganga, ila katika kufanikiwa kwangu kunatokana na kukwepa kodi na udanganyifu mdogo mdogo katika kazi zangu enzi nikiwa nimeajiriwa kwa mfano kudai kurudishiwa ghalama za usafiri zaidi ya nilivyotumia n.k, je hapa nilipo nipo ndani ya mchoro wangu?
 
Ndio kuna road map very perfect one! Wanaoenda motoni ni wale walioedit ruti zao.. Motoni ni adhabu ya kukengeuka nackuharibu
 
Haya ni ya kawaida mbaya ni kumdhulumu mhitaji ama fukara! Yani hata kile kidogo alichonacho unataka kiwe chako! Unajua kwanini anapitia hayo maisha? Sometimes huwa tunabeba laana bila kyjijua
Angalia mgambo wengi walivyo na maisha ya dhiki!(sorry ni mfano tu)
 
Hapana hizo ni story tu za vijiweni..hakuna ukweli kwenye hilo
 
Yan ufe raisi uzaliwe tausi???Afu uishi tena ikulu???Ngoja ninywe chai kwanza
[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]

Nimejikuta Nacheka tuu
 
Hapa Nimekuelewa Pasipo Hata Kwenda Tuition Mchikichini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…