Ulimwengu wa roho ni timilifu

Uncle Naona Unaongea Kwa Ushahid
 
Wacha weeehh, lkn sidhani kabla ya kuzaliwa roho ijue itazaliwa wapi, ni roho gani atakayependa aishi Tanzania, ni roho gani atapenda awe masikini, ni roho gani atapenda ainuke kimaisha na kupotea tena, ni roho gani atapenda afiwe na wazazi akiwa angali mdogo, nk nk nk. Kama roho wangekuwa na uwezo huu basi leo hii hakuna mtu ambae angekuwa anaishi maisha ya tabu kama ilivyo kwa binadamu sasa, kwani zingekataa kuingia katika miili ambayi itataabika maana hakuna apendae kuiumiza roho yake. Kama haizana uwezo huo basi tayari roho zipo limited na modificated.

Ni mawazo tu
 

ni kweli fuatilia mafundisho ya pythagoras ya transmigration of soul na re incarnation.
 
Mkuu nakufuatilia sana na upo vizuri aisee
 
 

kuna uchaguzi wakufanya aither uchague path of destruction (mauti) au uzima(baraka, mafanikio n.k), yote mawili yako kwenye maagano kwa hilo unapochagua agano la mauti/laana/shetani usitegee unaweza kutumia nguvu zako kubalisha chochote hata ufanye nini hutoweza, ukichagua uzima utafanikiwa tu, lakini uchaguzi unaweza kuwa ulifanya na mababu zetu na tayari uliingizwa kwenye huo mkataba hatua muhimu ni kujitoa kwenye huo mkataba ndipo uingie mkataba mpaya.
 
Bado nina safari ndefu ya nikufahamu Mshana jr, ila niaanza kukuelewa kidogo, na kama niko sahihi utakuwa mtu mzuri
 
Bado nina safari ndefu ya nikufahamu Mshana jr, ila niaanza kukuelewa kidogo, na kama niko sahihi utakuwa mtu mzuri
[emoji3] Agynasa mpendwa sijawahi kuwa mbaya ila perception ya watu kwenye hizi makala imenijengea image tofauti kabisa ....nashukuru kama umeanza kunielewa[emoji6] [emoji6]
 
Ulimwengu wa roho hauyumbishwi...formula zake ziko kama zilivyo michoro yake ni kamili na kamilifu unapojaribu kuisahihisha na ishu za waganga nyota na ngekewa unajitafutia dhahama usiyoiweza

Utafanikiwa kwa kipindi tu lakini asili itakurudisha kwenye shina lako kiroho..pale ulipotakiwa kuwa na hapo ni sawa na kujaribu kunyoosha bati lililopinda na kupondeka

Ulimwengu wa roho hauna modifications! Ishi maisha yako ukijibidiisha na ufanyayo katika mstari sahihi...usijaribu kutoka nje ya mstari kwa kuchanganya ya rohoni na ya kidunia ...hutafika mbali


Mkuu hapo nimekuelewa sana,kwa hiyo hata wale wanajitahidi kukufanyia ushirikina ili usifanikiwe maana yake wanajidanganya tu,[emoji2] [emoji2] [emoji2][emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Mwisho wako utasimama wewe na wao kuanguka vibaya...ila tu kama utasimama ulipo bila kujiunga katika mahangaiko yao ya visasi vijicho husuda na kutesana
 
Usiende kwa waganga! Usitafute ufumbuzi wa matatizo yako nje ya utaratibu wa kusahihisha uumbaji kama kusafisha nyota na kufanya kafara na matambiko
Laana za ukoo zinatokana na kutaka kusahihisha michoro yetu
Hapo kwenye laana za ukoo sasa mbona imani inatuambia kuwa kuna laana tulizorithi kutoka kwa mababu zetu...... utaratibu wa kujitakasa ukoje?
 
Hapo kwenye laana za ukoo sasa mbona imani inatuambia kuwa kuna laana tulizorithi kutoka kwa mababu zetu...... utaratibu wa kujitakasa ukoje?
Hizo walishamkasirisha Mungu na zitaondoka baada ya kizazi cha tatu ama cha nne.... Sanasana kinachofanyika ni kupozapoza tu kwa ibada na matambiko ya kawaida...kuendelea kufanya kafara za kuchinja ni sawa na kuzidi kuzilisha zile roho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…