Haya mambo yanachanganya sana. Mm naona wanaosema hakuna ulimwengu wa roho wafanyie utafiti wa kutosha kuthibitisha km ulimwengu huo haupo. Wasisemd tu kuwa haupo kwa sababu hawaioni. Wajiulize ni kwann watu husema ulimwengu huo upo? Wana ushahidi gani? Ni vitu gani vinavyowatjibitishia kuwa ulimwengu huo upo?Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ambao unatokea akilini, kwa kawaida bila makusudi, katika hatua fulanifulani za usingizi,
Huyo mzee kutabiri hailazimishi sisi kuamini kuwa Kuna ulimwengu wa roho njo na picha digital ni kubwa saivi
Hata wale wanaosema kuwa Kuna ulimwengu wa roho nao wajiulize kwann watu wengine wanasema ulimwengu huo haupo?
Mm nilikuwa muumini mkubwa sana wa sensi hizi 5 tulizo nazo wanadamu(Wanyamama) yaani kuona, kunusa, kugusa, kuonja na kusikia. Nje ya hapo sikuamini km Kuna la ziada. Niliamini na kujihakikishia kuwa hivyo vina ushahidi na madai mengine kuwa Kuna ulimwengu mwingine mfano pepo/Ahera au miujiza sikukubaliana nayo kabisa.
Lakini kama miaka 5 tu nyuma nilianza kupitia mambo ya ajabu ambayo, km Kuna mtu atanielezea sababu zake na inatokeaje, nitashukuru sana na huenda nikaendea na Imani yangu ya awali.
Ni hivi, kuanzia mwaka 2016 nilianza kuota kuwa nipo katika eneo lililozunbukwa na kinyesi Cha binadamu. Yaan pachafu balaa. Kila nilipoota ndoto hii haikuchukua zaidi ya saa 24 bila kupata balaa. Ni balaa zilizobaribu uchumi wangu na maisha yangu kabisa.
Ndoto hii imeendelea hadi ss. Nikiota tu najiandaa na balaa. Iwe ajali, kuibiwa. Kutokea mzozo au ht kushtakiwa. Naweza kumaliza ht miezi 3 mambo yakiwa mazuri tu. Lkn siku nikiota ndoto hii lazima kitu kikubwa negative kinitokee.
Nilijaribu kuuliza kwa watu mbali mbali, watu wa Imani ya dini na hata wanafanya tahajudi. Nilijibiwa kuwa Kuna ulimwengu wa roho ambapo mambo hufanyika kabla ya kudhihirika ktk ulimwengu wa mwili. Km wanavyoita wenyewe, na mm hupata taarifa tu ya mambo ambayo yameshafanyika lkn bado tu hayajaonekana.
Nilisoma ktk psychology kuwa ndoto ni matokeo ya mambo mengi yaliyopita na yaliyohifadhiwa ktk subconscious na mawazo yanayopita akilini mwa mtu. Lkn haya yanayonitokea hayapo kabisa ktk theory hii.
Ni kwanini najua kupitia ndoto balaa linalokuja kupitia ndoto? Kuna mwanasayansi ataweza kunieleza maana ya haya yanayonitokea?
Kwa wale wa Imani ya ulimwengu wa roho, Kuna uwezekano wowote wa kuepusha balaa ambalo litanitokea baada ya kuarifiwa kupitia ndoto?
Haya mambo, km hayajakutokea huwezi kuelewa nini kinamaanishwa na wengine.
Naombeni msaada kwa hili wakuu kina Mshana Jr, Mzizi Mkavu, Kiranga nk.