Ulimwengu wa Scania unaisha. Zuchu Howo ndio mpango mzima

Youtong miaka 5 halisumbui? Oyaa ni kampuni chache tu wamefanikiwa hilo tena kwa kua wana gari nyingi ndo maana kila baada ya miaka 2 wanaleta vifurushi vipya...na Youtong na wenzie wengi unaowaona wana miaka 5 hapa bongo zaidi ya 90% majiko yameshabadilishwa wameweka msweden.
 
Mbona unagongwa na Toyo unakufa
 

Utalinganisha hayo mabox na Scania?

Ni vizuriujue kuwa rahini ni aghali.
 
How haziwezi kuichallenge scania kwa kua kila gari ina ubabe wake

Pigisha howo ruti ndefu for long time uone kama atatotoboa kwa scania
HOWO ikibeba full mzigo kupeleka Congo Kupitia Tunduma, mwenye mzigo ataukuta bondeni kwenye milima ya Kitonga
 
Truck za mchina ni nzuri ila upate genuine spare

Life span zake ni one year

Ila scania ukifunga spea OG miaka 3 inadumu hata hivyo bado ni ghali that why matajiri wanaenda Kwa mchina

Pia gari za mchina Zina mafundi wengi na easy kufanya maintenance
 
GSM yard hap kurasini ni Kuna faw na howo new model (zuchu)

Hizi howo zinapigwa service ni well maintenance Hakuna ilikwishawai guswa injini

Gari ukiitunza haileti chokochoko

Zuchu wanapewa madereva smart wazoefu
 
Kinachofanya ni bei
Hapo ndio mchina anapowazidi wazungu
soko lao si kwa Tanzania na ndio maana uwezo wetu ni kununua mitumba iliyotumika huko wanakoweza kumudu gharama za hizo ndinga.Kuna duka moja maeneo ya kisutu combination plier(koleo) inauzwa 65,000 imeandikwa made in Finland wakati zile tunazozisifu za tronic ni 10,000.
 
Ukijua kiundani viwanda vya magari HOWO anahitaji miaka zaidi ya 50 ndo ajaribu kuanza kupambana na SCANIA.. Traton Group ndo anamiliki SCANIA ila pia Traton na subsidiary ya Volkswagen Group.

Hizi Scania nyingi zinazotumika Tz ni used lakini bado unakuta jiko linaita na kwenye route Ndefu na ngumu ukimuweka mchina hamalizi mwaka anaishia juu ya mawe.

Angalia mfano mwepesi bus zote zinazoenda masafa marefu na njia ngumu unakuta machine wamefunga Scania 113 kwa nini wasipeleke YUTONG? Itaenda speed miezi miwili mitatu ila baada ya hapo inajifia na matatizo yanakuandama kila kukicha, Kiufipi mchina anatachotaka sio kulinda brand wala nini anataka kutengeneza pesa leo apite ivi.. ndo maana utaona gari ni E number ila inafunguliwa jiko kisa inapoteza compresion inaanza kuwekwa sleeve.. wakati huo huo kuna SCANIA usajili AK.. Bado unavuta trailer SUPERDOLL kwenda DRC

Kama unataka kuwa na magari mapya kila wakati na njia laini na fupi basi mchina atakufaa sana ila kama unataka mkataba cheza na SCANIA ukijiweza zaidi sogea kwa ACTROS
 
Kukariri tu 😆mbeya dar kuna chuma za kichina nyingi dar tarime dar bukoba dar geita kote mchina kateka tena hizo 113 nani atumie karne hii kwenye mabasi ndio unakuta soketi za ukutani zipo kwenye basi kwa ajili ya charge, gari mbele ina dumu la maji , malessas, kisbo, nenga, newforce, abood, civito, abc, njombe na sweet africa wote wanaenda mbali na Chinese brands
 
Mbaya zaidi rungwe, sauli si walikuwa na scania vipenzi vyenu haya sasa wako wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…