Ulipata milioni yako ya kwanza ukiwa na umri gani?

Ulipata milioni yako ya kwanza ukiwa na umri gani?

definition ya kutoboa ndio kushika kibunda?

maana mjomba wangu ali kuwa 24 wakati huo, na ali vuna 15m mbele ya macho yangu.
kupata 1M+ kwa umri mdogo 18yrs au under ni kipengele kwa bongo kama ukifanikiwa kuipata kuna namna fulani unakuwa umetoboa kama utakuwa na plans nzuri za kuizalisha.
 
Kwanza niliipata huko nyuma sana kwenye dili za kuuza shaba ,nikiwa mdogo sana ...kuna sehemu nyumba ziliungua ,tukaenda kuokota shaba na vyuma tukauza .

Chuo mwaka wa kwanza nilipata pesa ya kujikimu ile batch ya kwanza mara mbili 😅, halafu nikiwa mwaka wa pli nilipiga mil 8 kwa online pyramid scheme ila nishatemana nazo...Pesa kama zote niliweka home kwenye ukarabati wa nyumba fresh ila sio mwekezaji mzuri.

Nilitumia pesa sana ,nilitumia bila ya kuzalisha kwa mwaka 1.5 ikabaki mil 1 ,ghafla napata ajira naanza na take home ya 2.4 acha tu basi ,nili'hang sana watu wanajua mimi tajiri mpaka leo .

Niliishi juu juu ila sikuwahi kubaki mikono mitupu tangu nishike pesa mara ya kwanza.
 
Noma sana 17yrs kushika M1 kibongobongo ni mafanikio makubwa.
Sio kweli mafanikio kama utafanya jambo la maana. Umri huo wengi tuna mihemko. Mimi sikua nakunywa wala kufanya starehe. Ila hizo hela hadi leo sijui zilipotelea wapi. Zaidi muda baadae ndio nilianza kununua shamba na ujenzi at 24. Tena na hela za umri huo. Zile za kupata kwa pupa sikuwahi nunua hata jeans ndani.
 
Nilipata nikiwa na miaka 18 nkafungua biashara ya chakula kibaha pale.

Mi sikuwepo kusimamia sikuwahi kula faida ya Ile biashara mpaka ilipokufa rasmi.
Mtu niliyemwachia Kila siku Alikuwa ananipigia simu twende kwa mganga.

Mpaka kesho sitokuja kufanya biashara ya chakula aisee
 
Back
Top Bottom