Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Nyie jamaa jamii yenu inaonekana ni ya watu wa fitna na umbea sana yani unapigiwa simu kupewa taarifa ya meko kufariki, real? Mkiacha shida zote tulizonazo kama taifa!
Hujaona kwamba kuna shida moja ilikuwa imetoroka yenyewe hapo?😝😝😝😝😝
 
Bado una majonzi.Pole sana.Hata kuandika tu unatetemeka.
 
Nilikua sehemu nimekaa nakunywa soda...akaja jamaaa fulani ananambia oya baba amevuta nikashtuka sana na kumpa pole nyingi...ikabd nimuulize mnazika lini na lin utaenda mbeya??....

Nashangaa ananijibu magufuli na mbeya wapi na wapi....heee nikashtuka kumbe magu?? Nikajua baba ako nilishangaa sana jamaa ananambia hivyo huku analia sana[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]....ikabd nimpe pole akapokea pole yangu nikaendelea kunywa soda
 
Nilikuwa nimelala usiku kama saa sita na kidogo, nikamsikia mtoto wa sista ananiita ile natoka ananiambia kuna mtu kamtumia msg Whatsapp kwamba Magufuli kafa hivyo aweke TBC wanatangaza.

Ndio mbio tukakimbilia kuwasha TV na kukuta Mama SSH anatangaza.
 
dah! Imebidi nicheke tu.
 
Mimi iyo siku nilikua nipo na mtoto ndani aisee. Usiku mzima mechi imechezwa hakuna alokumbuka simu.

Ile asubuh kama saa 1 ivi naamka nakutana na news kila kona ya mtandao na sms kibao kwamba mwamba kavuta.
Ile namwambia yule manzi aisee nilijuta kumwambia alihamishia msiba gheto acha aanze kulia pale wakati mimi huzuni hata sina.
 
Sasa magufuli alikuwa na jema lipi?[emoji16] Hadi uhuzunike?
 
Hujawahi kufiwa?
 
Unasisimka magufuli kufariki?
 
Unamkubari kwa lipi propaganda zake?
 
Siku 3 kabla ya tangazo la Kifo chake.

Nilipitishwa ktk(ulimwengu wa roho)

Nilimuona JPM akiwa na mpambe wake.

Jpm Alionekana akiwa na huzuni saana,

Kuna briefcase ya flan ya Rais yule mpambe wa Rais alimkabidhi mtu flan(Ambae alikua kivuri sikumtambua sura wala jinsia).

Shortly Nilikuja kuelewa na kukumbuka maono hy usiku ule baada ya tangazo la msiba.



Taarfa za msiba.

Nilikua nimelala wakaja madogo,(walienda kucheki mechi bandani)

Wanaongea kwa sauti ya juu mpk nikashtuka nikaamka.

Ile kufungua mlango nikaskia "Jamani Magufuli kafariki"

Nikamuuliza we umejuaj?

Akaanza kuelezea.



"Si tulikua tunaangalia mpira ghagla akasimama juu muhuni mmoja, akasema kwa sauti kubwa...JAMAAAANI EEEH TAYARI!!!...wakasema kaachini acha ujinga,tyr nini..

Aksema TAYARI MAGU KAVUTA..

KAMA HAMUAMINI WEKENI TBC 1..

Ikawekwa tukamwona Samia Anahutubia kwa huzuni"

Hatujaendelea na mpra wote tumetawanyika"

Aisee tukawasha tv na redio tukakuta nyimbo za misiba zinapigwa .

Nilichoooka nilisikitika niliporudi kitandani ndo nikakumbuka siku 3 nyuma yale maono niliyoyaona kumbee yalikua na maana hyo.

Nilitokwa machooozi.
 
Ilikuwa usiku, nikasikia Tanzia. Kifupi kwanza si kulala hadi asubuhi, na hamna msiba niliowahi kutoa machozi kama wa hayati Magufuli. Mimi ni mmoja wa watanzania tulioumia sana na kufariki kwake. R. I. P Magufuli
Mnachekesha sana
 
Itoshe kusema nilikunywa sana jameson na kupata wanawake 4 wazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…