wa stendi
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 25,190
- 27,434
Jamaa yangu ofisini alinipigia cm usiku saa tano sikupokea nikidhani nahitajika au ananipiga kirungu cha hela kunbe alikuwa ananipa taarifa. Basi nimeamka asbh sijui nini kinaendlea nikafungua radio nisikikize bbc ile taarifa ya asbh mara radio inaimba wimbo wa gudluck "tutaonana tena mbinguni tutaonanaa "mi sikujua nimejiandaa nikawasha gari niende ofisini niko njiani nikawasha data nakuta group kumejaa mipicha na r.i.p aseee nilishtuka kidogo lakini kadri siku zinasonga ndio nikajamini mchana mda tumeenda hospitali aliko daaa niliumia sana ila ndio hivyo kazi ya mola haina makosa.Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.
Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"
Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.
msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.
Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.