Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ilikuwa usiku, nikasikia Tanzia. Kifupi kwanza si kulala hadi asubuhi, na hamna msiba niliowahi kutoa machozi kama wa hayati Magufuli. Mimi ni mmoja wa watanzania tulioumia sana na kufariki kwake. R. I. P Magufuli
Wape pole na wengine waliopata maumivu hapa Duniani kwa matendo yake wakati wa uhai wake. Usiwasahau na wao pia ni binadamu.
 
Daah kabla ya Tarehe 17 tarehe 9 majaliwa anaenda njombe tarehe 12samia ana ziara Tanga siku tatu kabla ya hizo tarehe malaika alikua akizungumza na mimi katika roho...
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiki kiswahili cha wapi
Nakubuka vizuri sana wakati mama samia anatangaza huyu mkuu wa wasiojulikana kafa, nilikuwa canton ya ZUG, huko swiss, nilikuwa niko macho, nafanya nakagua tax records za kamupuni yangu, maana imesajiliwa hapo zug, mara simu ikaita, ni mtu rafiki toka bay area, huko california, kaniuliza una taarifa, kauliza taarifa gani, hujasikia kaniuliza, kasema la niambie, kaniambia aliyekuwa anaua, anateka, anabadikia watu kesi za uhujumu uchumi ako na shetani sasa hivi, mara simu zinaaza kuingia kunipa taarifa,niliacha ile kazi, kaaza kujulisa watu, kila pahali, kila mtu nikimupigia wengi taarifa wanazo, ni shagwe na nderemo, furaha kweli, never ever again in tanzania, watu wanasema kwa twitter, sikulala ile usiku nilikesa nasherekea ushindi mkuu, mungu ni mkuu kuliko kijani, amina, jina lake liko juu ya majina yote
 
Alifariki Baba, alifariki Mama nilihuzunika sana tu bila kutoa chozi.
Ila kwa JPM chozi lilinitoka kwa huzuni kubwa huku mapigo ya moyo yakiwa juu sana.
Hadi leo bado ninahuzuni.
Wewe ni katili
 
Nilikua nimelala,nikaamshwa na simu za wadau!
Binafsi kama kura na hata kampeni nilimpigia sana jiwe awamu ya kwanza mpaka nikakosana na watu wangu wa karibu ambao walikua chadema,lakini baadae nikaanza kumuona jiwe simwelewi yani hasomeki nikajuuuta adi kumpigia kampeni nikajisemea kweli ccm ni ileile!
Nikaamua kuishi huku simkubali,unatamani kitu kitokee atoweke ila ukweli ile siku napata taarifa rasmi kuwa jiwe kafa huzuni ilinijia mana mwisho wa siku nae ni binadamu tu na kifo tumeumbiwa wote!
Aendelee kupumzika mwamba,sasa tuko na mama na kazi inaendelea!
Mama oyeeeee!
 
Binafsi sikushtuka. Nilikuwa nimelala zangu nimefungulia clouds niko zangu twitter naperuzi. Nikaanza kuskia clouds wamechange motion wakaweka nyimbo flani hivi ambavyo sio kawaida yao, nako sikustuka, ghafla mida hiyo ya saa 5 mwanangu mmoja hivi kaniendea hewani, kabla sijapokea nikagundua kuna kitu. Kupokea tu kanipa taarifa huku akiwa na vibe la kutosha. Basi siku hiyo nililala mtandaoni kusoma maoni ya watu. Nilichogundua ni kuwa mwamba alikuwa hapendwi hata kidogo
 
Mimi nikiri sikuwa sawa tangu tetesi za kuumwa kwake nlikuwa naomba Sana kimoyo moyo isiwe kweli yaani.badi bhana siku yenyewe nilikuwa nimetoka kazini ile nalumzika kidogo baada ya kuoga kabla ya Kula nikapitia pitia jf Kwanza ili nilale, ile naenda bafuni kirudi wife ananiambia angalia itv huku analia aisee...kwa mara ya Kwanza nikaonja uchungu wa msiba tangu nizaliwe inauma Kama nini.nilikaa Kama siku mbili sielewi elewi mpaka sasa bado kwa mbali sielewi Mimi.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Mpaka umri wa kuoa hujawahi kufiwa hata na ndugu ukaonja machungu ya msiba. Kwa nara ya kwanza ukayaonja kwenye kifo cha JPM jokate mwenyewe alikuwa anasmile tu
 
Mimi nilikuwa porini nalina asali na kutafuta dawa za mitishamba.

Usiku tumelala huko huko porini kuna dogo mwenzetu mmoja alikuwa na radio usiku tumelala akafungua kiredio chake akapata taarifa ya huo msiba akaniamsha kunijulisha sikushituka chochote nikarudi kulala kutokana na uchovu wa kutembea toka asubuhi porini.

Kesho yake nimetafuta network nikampigia jamaa mmoja kuconfirm kama ni kweli akasema ni kweli basi kilichoendelea sijui maana sikufuatilia tena habari hizo toka Samia aapishwe.
Aseee[emoji848][emoji848]
 
Nilikuwa kitandani, nilikuwa online. Ghafla sms ya WhatsApp ikaingia kwenye group jamaa akisema akina nani wameangalia TBC sasahivi(muda huo siku hiyo), mwingine akarukia "na mimi nimesikia Magu kafa". Hadi hapo nikashtuka sana ila moyoni niliomba iwe kweli(huu ndio ukweli siwezi kuwa mnafiki hapa).

Nikaanza kutafuta ukweli wa hiyo habari kwenye vyanzo vyangu vya kuaminiki kwa kuanza na JF, ghafla jamaa kwenye group la familia akapost akisema "Chuma kimekata moto" nikamuiliza ni kweli, akasema ndio. Hadi hapo nikashusha pumzi, nikaja JF nikakuta bado Uzi haujapandishwa, nikakimbilia Channel ya Telegram ya JF, kule napo nikakuta patupu. Baada ya dk kama 5 ndio uzi ukapandishwa hapa JF. The rest ikawa historia.

Now tunataka kujenga sanamu yake kwa zaidi ya Milioni 400
Mkuu si u download twitter? Kule raia wako fasta
 
Nilikuwa nyumbani.Ilikuwa ndiyo siku pekee katika maisha yangu ambayo niliwahi kuwa na furahaa kupitiliza.

Nakumbuka kwa mara ya kwanza katika maisha yangu siku hiyo nilitoa sadaka ya kuteketeza kumshukuru Mungu kwa kuniondolea uchafu katika Taifa langu.
Khaaaaaa[emoji134]
 
Hiyo siku nilikuwa nimepiga k-vant kubwa nikasema nipumzike nje kidogo ili nisiwasumbue wa ndani, bahati mbaya usingizi ukanipitia.
Nakuja kushituka nakuta wapangaji wapo nje wanalia. Nikajua labda nilizima, walivyoona siamki wakajua nimevuta.
Nikaamua kuamka ili kuonesha mi ni mzima, nikaona hata hawana mpango na mimi. Ndio kuna jamaa akatamka kabisa kuwa Magufuli kafariki.
[emoji16][emoji16][emoji16] ukajua wanakulilia wewe[emoji1787]
 
Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.

Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"

Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.

msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.

Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.
Honestly nilifurahi.

Kama hukuumizwa na utawala wake hutoelewa.
 
Nilikuwa naandaa document flani ya jamaa, akanipigia simu, nikajua anataka nimtumie, ndiposa ananipa ripoti, kama binadamu nilistuka kwa furaha.
Kama binadamu ulishtuka kwa furaha?[emoji16][emoji1787]....nyinyi watu hamko serious
 
Sishangai kuwepo na binadamu wa aina yako wanaomini matusi ndio last option ya kutetea wanachokiamini dunia isingekua na watu kama nyinyi wenye hekima na busara wangeishi ulimwengu upi? Elimika sikufundishi
Busara yako ndio hiyo ya kumlilia Shetani Magufuli. Poor you.
 
Back
Top Bottom