Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Nilikuwa bandani naangalia game ya Chelsea vs Atletico, mara nikachukua simu napitia WhatsApp stutas nakutana na RIP Magu.
 
Nilivyopokea taarifa ya kuiaga Dunia na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amiri jeshi mkuu wa majeshi yote yaliyopo TANZANIA nilihuzunika sana kwa maana ndie kiongozi wa kwanza kumpigia kura ya ndio✅✅✅✅✅ mwaka 2015...Taarifa ya msiba niliipokea kutoka kwa jamaa flani akiniambia nanukuu.'' oya mzee baba ametembea mwanzo nilimbishia akaniambia mama ndiye alie tangaza''kusema ukweli niliumia sana baada ya kuthibitisha ya kuwa ni kweli Shujaa wetu ametutoka. 😿😿😿😿
 
Kingine ambacho sitakisahau ni ile ziara ya ajabu ajabu ya samia kule Tanga na Majaliwa kule kusini,majaliwa alikiwa anakwenda Iringa na kurudi ghafla ghafla Dodoma
 
Hiyo siku nilikuwa nimepiga k-vant kubwa nikasema nipumzike nje kidogo ili nisiwasumbue wa ndani, bahati mbaya usingizi ukanipitia.
Nakuja kushituka nakuta wapangaji wapo nje wanalia. Nikajua labda nilizima, walivyoona siamki wakajua nimevuta.
Nikaamua kuamka ili kuonesha mi ni mzima, nikaona hata hawana mpango na mimi. Ndio kuna jamaa akatamka kabisa kuwa Magufuli kafariki.
 
Hiyo siku nilikuwa nimepiga k-vant kubwa nikasema nipumzike nje kidogo ili nisiwasumbue wa ndani, bahati mbaya usingizi ukanipitia.
Nakuja kushituka nakuta wapangaji wapo nje wanalia. Nikajua labda nilizima, walivyoona siamki wakajua nimevuta.
Nikaamua kuamka ili kuonesha mi ni mzima, nikaona hata hawana mpango na mimi. Ndio kuna jamaa akatamka kabisa kuwa Magufuli kafariki.
[emoji1][emoji1][emoji1] Dah umezingua mkuu
 
Nipo Mkoani Tanga Lushoto huko nacheki Game ya Uefa Chelsea vs A.Madrid sina hili wa lile kuna jamaa akaropoka Magufuli kafariki..watu fasta fasta wakaingia kwenye simu zao kuverify..aisee mpira haukutazamwa tena.
Nilikuwa ufipa walishangilia Sana wakasema Abubakar atakuwa rais sasa.
 
Nlikua nimelala jamaa mmoja akaniamsha ananiambia magufuli kavuta akanisikilizisha na post ya Millard ayo ambayo mama Samia mwenyewe ndo anatangaza kifo
Mi nikamjibu tu "poa nimeskia"
Msela akaanza kulialia kama mtt wa kike nikamtukana tukaanza kuzinguana
 
Nilikua zangu N... Naangalia series ya Jesica Jones mzee baba akanipigia simu akanipa taarifa sikuamini. Nikalog jf nikakuta taarifa, Ya Rabi roho yangu nilisikia shoti inapiga mwilini. Nilishikwa na homa usiku huo huo asubuhi naamka nilianguka chini nikazidiwa zaid. Kwa wiki mbili zote hadi April nilikua hoi mazishi nimefuatilia niko hoi I think nilipata heart attack
It was the saddest day of my life.. Jpm ni moja ya watu walinifanya nijivunie kuwa mtanzania na mwafrika. Nilimchukia Mungu kwa kuruhusu hilo kutokea Wakati bado twamuhitaji.

Ila nilijiambia kwamba death doesn't come to wicked and leave the Innocent behind. The purpose has been served by his servant JPM. Tumshukuru Mungu kwa uhai kidogo wa magufuli aliomjalia ila atuonyeshe jinsi gani yatupasa kua..

Always nilikua nikipata wasaa namuombea na nitaendelea kumuombea Mungu amjalie rehema na baraka zake.
Raha ya milele uumpe eeh Bwana.....😢😢
 
Ilikuwa usiku, nikasikia Tanzia. Kifupi kwanza si kulala hadi asubuhi, na hamna msiba niliowahi kutoa machozi kama wa hayati Magufuli. Mimi ni mmoja wa watanzania tulioumia sana na kufariki kwake. R. I. P Magufuli
Wewe ndio 7ya?
 
Kama kawaida baada za zile rumors kua jamaa hali mbaya nikawa ni mmoja wapo ya raia wenye roho mbaya kutamani jiwe lipasuke

Siku hiyo nilikua online JF mbaka saa Tano kasoro Hivi mara nikapitiwa na usingizi wa ghafla nikaja shtuka saa 10 sms imeingia kucheki sms ni binamu yangu wa kike
Kusoma kaandika Siamini Kama Magu kafa nikajua utani wa mabinamu tu Ile sijakaa sawa anko katuma sms
Oy mzee baba Magu kavuta Aisee

Fasta nikalog in JF nakutana na Tanzia

Nikajua baasi moyoni nilifurahiiiii nikajua jiwe walilolikataa waashi limepasuka paaaaaaaaaa

Nikamreplay binamu nikasema daa ndio hivyo kavuta iasee alichonijibu daaaa nikajua Kuna watu walikua na hasira na jiwe zaidi yangu et

Et aaagh Bora yule wuuwuuwuu (tunayokulaga wahehe)
Imekufa maana ilikua laana!

Nikajisemea daaa wale warusha mawe gizani itakua sherehe!
 
Aliyekufa kafa.. Kila nafsi itaonja umauti.
Kuna katabasamu kakifala kalitaka kunawiri usoni, ila baada ya kujiuliza why nitabasamu kwa kufa mwenzangu nami utafika wakati nita IZ DEDI, nikavunga tu, ila sikujishughulisha na chocbote kuhusiana na msiba.
 
Back
Top Bottom