Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Namkumbuka dada mmoja wa Kimasai aliyenitonya dhalimu kafa tangu tarehe 11 March. Siku hiyo huyo dada aliruka ruka kwa furaha kubwa sana. Wala sikumlaumu kwani kama mfanyabiashara Arusha na Dar biashara zake zimeyumba sana kutokana na sera MUFILISI na kwa muelekeo huu wa samia sidhani kama kutakuwa na ahueni anytime soon.

Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.

Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"

Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.

msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.

Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.
 
Namkumbuka dada mmoja wa Kimasai aliyenitonya dhalimu kafa tangu tarehe 11 March. Siku hiyo huyo dada aliruka ruka kwa furaha kubwa sana. Wala sikumlaumu kwani kama mfanyabiashara Arusha na Dar biashara zake zimeyumba sana kutokana na sera MUFILISI na kwa muelekeo huu wa samia sidhani kama kutakuwa na ahueni anytime soon.
Arusha watu walifunga biashara sana, mmojawapo mie
 
Watu tunazika watu wetu kwa corona kila siku halafu yeye anasema Tanzania haina corona! Alistahili sana kufa kwa corona hiyo hiyo.
Aaaaaa mimi nilishtusha na kilio cha Mke wa Jirani yangu nyumba ya pili...Upuuuzi mtupu,nikikumbuka Ndio week imepita nimemzika Baba yangu kwa uongozi wakizembe kwakuzembea Corona,nikasa bora nayeye aende tu
 
Nyie jamaa jamii yenu inaonekana ni ya watu wa fitna na umbea sana yani unapigiwa simu kupewa taarifa ya meko kufariki, real? Mkiacha shida zote tulizonazo kama taifa!
Cool
 
Mie nilikua kitandani najiandaa nilale nikapigiwa simu na sister angu ananiuliza kuna habari gani huko mjini nikamwambia huku shwari hakuna shari akasema mbona nasikia Rais amefariki? Nikacheka sana nikamtoa wasi wasi sister atulie tulii kuna wazushi wanapenda kuzusha mambo akasema ameona kwa Zamaradi kapost, nikashtuka kidogo nikamwambia wait nitamcall back, mie mbio mbio hadi Jamii Forum nakutana na TANZIA kuuuuubwa, nililia kwa uchungu daaaah hadi leo hua napata ukakasi sana kumuita Hayati Magufuli nahisi bado yupo nasi,

Continue to rest easy Mzalendo wa kweli,

[emoji24][emoji24]
Duu acha tu
 
Huwa nachelewa kulala lkn siku iyo sijui ilikuwaje nikalala mapema, na huwa nalala wasafi fm ikiwa on maana napendaga kusikiliza miziki sana...

Basi imefika saa tisa usiku nikastuka usingizini, ila nikashangaa wasafi fm wanapiga ule wimbo wa "tukutane paradisoo, tukutane paradisoo", nikajua hapa kimenuka.

Kuingia twitter nikakuta wananzengo wamelipuka mnoo kwa furaha+majonzi.
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
uzuri sikuhio nililala mapema, baada ya kuumwa kutwa nzima hoi hoi...
nilikuja kuambiwa saa11 alfajiri moyo wangu ulipasuka,sikua na amani kutwa nzima kwa mara ya kwanza niliuona msiba unavyoumaga kwakweli ilikua ni gafla mno mpaka leo nashindwa kuamini. [emoji22]
Duuu pole
 
Siku hio sister kanipigia simu saa 5 usiku, nikaikaushia tu nikahisi jambo zito linakuja. Sio kawaida kunipigia late night.

Baadae ananitumia sms eti magufuli kafariki, dah nilizima simu, nikalala! Like nothing happened.

I lost my Job because of him.
And now I am a senior un employed fellow.

6 yrs without a Job
 
Nilikua jf naperuzi mida yangu ya kulala ilikua mara gafla natoka jkwaa la mahusiano narudi habri na hoja mchanganyiko nakutana na TANZIA nilisisimka usingizi ukakata machozi yakanilenga nikasema basi tena ndo huku pembeni kwa jirani nasikia Mama Samia anatangaza
Aiseeeee
 
Nikiwa hapa mji dsmlamu nilikiwanakaribia. Kulala bas Niko na jirani angu Apo katuliaa getoni kwake tuli bass jamaaa akakimbia chumbani kwangu kuwa meko amefariki duh nikasikitika snaa. Kweli nikasema wamemuaa itakuwa Jamaaa alinishangaa sna kwa jinsi nilivyoupokeee msiba huo nilidondosha Choz kbsa nikajikaza kimya kimya bas jamaa aalinishanga sana jins nilivyo upokea alizani nitafuraia ilaa uliniumma snaa ckupenda kifo chake kwa kweli
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Me nilikuwa v lounge, moshi town, nakula vyombo na mchuchu, sina hili wala lile nataka nikale zigo, mara simu inaita, na mziki, nikasema bro ni nn usiku usiku na misimu, yy hakuwa anamkubali magu, mm namkubali mbayaa, hadi kiama. Zile fununu tukawa tunabishana sana wanamzushia. Napokea simu naziba sikio moja nimsikilize freshi.
Bro ananiambia, dogo cheki tbc Samia anahutubia taifa, nilivosikia tu hivyo, moyo ukapiga paaa.
Haaaaaaa
 
Nipo Mkoani Tanga Lushoto huko nacheki Game ya Uefa Chelsea vs A.Madrid sina hili wa lile kuna jamaa akaropoka Magufuli kafariki..watu fasta fasta wakaingia kwenye simu zao kuverify..aisee mpira haukutazamwa tena.
Duuuuuu
 
Nilikuwa nyumbani.Ilikuwa ndiyo siku pekee katika maisha yangu ambayo niliwahi kuwa na furahaa kupitiliza.

Nakumbuka kwa mara ya kwanza katika maisha yangu siku hiyo nilitoa sadaka ya kuteketeza kumshukuru Mungu kwa kuniondolea uchafu katika Taifa langu.
Duuuu
 
Daah kabla ya Tarehe 17 tarehe 9 majaliwa anaenda njombe tarehe 12samia ana ziara Tanga siku tatu kabla ya hizo tarehe malaika alikua akizungumza na mimi katika roho
Nilimuota magufuli mara tatu ni baaada ya kuhutubia mbezi pale alinionyesha Mungu magufuli amekufa nilipatwa na roho ya kuomba na kujinyenyekeza mbele za bwana kitu ninacho amini magufuli alikufa tarehe 8 mwezi wa tatu
NILIMPENDA HUYU MTU KWA MARA YA KWANZA NAMUONA MAGUFULI NILIKUA NAMPELEKEA DEMU WANGU ZAWADI KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA ALIKUA ANASOMA BAOBAB GIRLS BAHATI MBAYA SIKU ILE ILINYESHA MVUA DARAJA LA RUVU CHINI LILIKATIKA MAWASILIANO YA BARABARA KUTOKA MSATA KUJA DAR KUPITIA BAGAMOYO ROAD HAYAKUWA YANAPITIKA NDIPO MWAMBA ALIPOFIKA NA KUREKEBISHA HALI NIKAMUONA NILIWAZA MOYONI HUYU ANAFAA KUA RAISI WA NCHI NA KWELI IKAWA NILIMPENDA SANA HUYU MWAMBA TOKA MOYONI SIJIPIGA KURA TENA NILIANZA KWAKE UTAMADUN WA KUPIGA KURA NA UMEISHIA KWAKE KIBAYA NA KINACHONIUMA DEMU NILIYEMPENDA KANIACHA NA MWAMBA AMELALA MILELE NINAMAUMIVU TWO SIDE NI HAYO
[emoji23][emoji23] i miss my school. Ila siku hizi hata si ya moto kama zama zetu miaka ya advance late 2000s.. tulikua wa moto sana.
 
Back
Top Bottom