Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Hiyo siku nakumbuka nilikuwa natoka Mbeya,tupo kwenye coaster,muda wa saa tano hv usiku,tulikuwa mafinga,abilia wote wanasinzia,mmoja akacheki mtandaoni,akasema Jiwe kafa,watu wakashituka,usingizi ukaisha,story zikaanza hakuna aliyelala mpaka tunafika Morogoro,watu walikuwa kama wametoka kifungoni,Jiwe alikuwa shetani
Mkuu we acha tu
 
Ilikuwa usiku, nikasikia Tanzia. Kifupi kwanza si kulala hadi asubuhi, na hamna msiba niliowahi kutoa machozi kama wa hayati Magufuli. Mimi ni mmoja wa watanzania tulioumia sana na kufariki kwake. R. I. P Magufuli
Pole
 
Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.

Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"

Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.

msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.

Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.
Na sisi tuliopata taarifa kafa tarehe 9 March tu comment wapi?
 
Hivi kifo chake hakikutangazwa kwanza na makamu wake? I mean watu walianza kupata habari kabla Samia hajatangaza? NB: Sizungumzii ule uvumi uliokuwepo tangu aanze kuugua mpaka kwenye tarehe 12 Chahali alipoandika rasmi kwenye Twitter kuwa amekufa. Naulizia serikali kutangaza rasmi. Turudi kwenye mada: Mimi niliposikia ni mgonjwa nilikuwa na mashaka kwani kile kipindi kingine alivumishwa tena anaumwa taabani. Kengele ya tahadhari ilianza kulia siku gazeti la Daily Nation lilipoandika kuna kiongozi kalazwa Nairobi Hospital. Nilijua hili gazeti hawakurupiki lakini cha ajabu kesho yake wakaandika tena hakuna kiongozi aliyelazwa. Baade nikapata habari kutoka chanzo cha kuaminika kuwa ni kweli amepata corona ila hali yake haijulikani. Siku mama Samia alipoenda Tanga na kusema kuchekiwa chekiwa ni kawaida kwa binadamu nilijua lazima kuna jambo ila nikasema huenda ame-recover. Nilijua rasmi alfajiri baada ya taarifa kutolewa usiku. Na hili la kutangaza usiku lilikuwa ni timing kwani walikuwa hawataki habari itoke mchana.
Nadhani mwamba alikufa kwa Covid-19
 
Taarifa niliipata asubuhi baada ya kuamka...sikustuka kwa kuwa nilijua Hilo one week before...
 
Mimi nilikuwa porini nalina asali na kutafuta dawa za mitishamba.

Usiku tumelala huko huko porini kuna dogo mwenzetu mmoja alikuwa na radio usiku tumelala akafungua kiredio chake akapata taarifa ya huo msiba akaniamsha kunijulisha sikushituka chochote nikarudi kulala kutokana na uchovu wa kutembea toka asubuhi porini.

Kesho yake nimetafuta network nikampigia jamaa mmoja kuconfirm kama ni kweli akasema ni kweli basi kilichoendelea sijui maana sikufuatilia tena habari hizo toka Samia aapishwe.
Naona hayo madawa ya asili yalishakuharibu kichwa.
 
Binafsi niliumia sana siku hiyo hakuna wimbo uliokuwa ukiniumiza kila nikiusikia kama ule wa Msechu- UMETUACHA salama. Taarifa za kifo nilizipata mida ya saa sita usiku nikiwa kwenye basi la fikoshi Iringa to Mwanza. Jamaa alikuwa mwamba!!!
 
Mimi nikiri sikuwa sawa tangu tetesi za kuumwa kwake nlikuwa naomba Sana kimoyo moyo isiwe kweli yaani.badi bhana siku yenyewe nilikuwa nimetoka kazini ile nalumzika kidogo baada ya kuoga kabla ya Kula nikapitia pitia jf Kwanza ili nilale, ile naenda bafuni kirudi wife ananiambia angalia itv huku analia aisee...kwa mara ya Kwanza nikaonja uchungu wa msiba tangu nizaliwe inauma Kama nini.nilikaa Kama siku mbili sielewi elewi mpaka sasa bado kwa mbali sielewi Mimi.
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Yaani ndo nilikua na 2 toka nirudi hospitali kufanyiwa operation ya tumbo. Group la whatsup la primary mtu akapost nikamwambia dont post kwanza ngojea credible sources maana tunajua zaman tu sema kuwa official ndo ilichelewa. Akanambia ni kweli tayari. Nikazama kuchek kwa mitandao na TBC 1. Basi status za unafiki ndo ziliniondolea ugonjwa kabisa.. kila status watu wanajiliza wakati ndo walikua wanamwombea kifoo. Nilipatwa na hasira maana ndo unafiki wenyewe. Nilikua nachat na babes pia[emoji23]
Maybe anaweza akawa alikua na furaha kunizidi. Ilikua balaa.. hata kuongea na miye waapi... basi life likasonga. Sema later sikuona sababu sana ya kufurahi japo ile ya kutumia pesa zetu kumzungusha kila mahali kulazimisha aonekane alipendwa iliboa.
Mzee wangu walichinja beberu[emoji23][emoji481] wafanya biashara wa dar, moshi na arusha ni wahanga wakubwa sana wa mwendazake.
 
SIKU hiyo nilichelewa kulala nikawa busy nacheki movie, baadae nikasema goja niingie online kidg ndipo mfanyakazi mwenzangu Kwenye group ikaingia sms kasema pumzika mwamba kisha kaweka emoji za kulia nikshtuka nikampigia akanambia Magufuli kafa [emoji24][emoji24][emoji24] sikuamini asee.


Nililia siku mzee anaagwa Mwanza baada ya clip moja kuiona anasaidia mama kipofu kule Mara nililia sana.

RIP. mzee
 
Nlikua getoo
Nkafungua status naona watu kama 20 wametupia picha ya magu!
Wala sikuwaza
Kuja kufunguaaa kumbee hee!!!!!!!!
Ikabid nizame kwenye trusted site ya ayo dah kumbe kweli[emoji26]
 
Mimi nilikunywa Whisky mapema nikalala.

Sa saba nasikia sauti dirishani kwangu, mshana, mshana amka tukanywe bia jamaa katili kafariki.
Dah..........
 
Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.

Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"

Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.

msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.

Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.
Nlitoa ofa ya kufa mtu kwa masela wenzangu,nusksi mungu aliipenda kuliko sisi
 
Nyie jamaa jamii yenu inaonekana ni ya watu wa fitna na umbea sana yani unapigiwa simu kupewa taarifa ya meko kufariki, real? Mkiacha shida zote tulizonazo kama taifa!
jikite kweye mada, au wewe ulikuwa unafaidi wakati wa jiwe, hakuna mtu wenye akili poa ambae hakuona jiwe kufa mungu kaondoa muakilishi wa shetani tanzania,
 
Mie nilikua kitandani najiandaa nilale nikapigiwa simu na sister angu ananiuliza kuna habari gani huko mjini nikamwambia huku shwari hakuna shari akasema mbona nasikia Rais amefariki? Nikacheka sana nikamtoa wasi wasi sister atulie tulii kuna wazushi wanapenda kuzusha mambo akasema ameona kwa Zamaradi kapost, nikashtuka kidogo nikamwambia wait nitamcall back, mie mbio mbio hadi Jamii Forum nakutana na TANZIA kuuuuubwa, nililia kwa uchungu daaaah hadi leo hua napata ukakasi sana kumuita Hayati Magufuli nahisi bado yupo nasi,

Continue to rest easy Mzalendo wa kweli,

[emoji24][emoji24 mmmmmmm
 
Back
Top Bottom