Ulipokuwa unashindia Mihogo na Kunywa Maji, walikuwa wapi?

Ulipokuwa unashindia Mihogo na Kunywa Maji, walikuwa wapi?

Ndugu zangu wanaume, wakati mwingine lazima ujiulize: 🤔

Huu upendo ulikuwa wapi wakati nilikuwa nashindia mihogo na kunywa maji?” 😂

Ulihangaika peke yako, ulijijenga kutoka sifuri, halafu ulipofanikiwa/unapofanikiwa ghafla watu wanaanza kujifanya walikuwa sehemu ya mafanikio yako.

Chagueni watu mnaowazunguka kwa umakini. Si kila anayeshangilia mafanikio yako alishiriki katika safari yako.

Wakati wa shida, wengi watakutazama ukianguka. Wakati wa mafanikio, wengi watataka kusimama karibu na wewe.

Usisahau waliokushika mkono wakati hukuwa na kitu cha kuwapa.

Heshimu waliokuamini kabla dunia haijaanza kukuamini. Na zaidi ya yote, usiruhusu mafanikio yakufanye usahau ulipotoka.

Kwa sababu utajiri unaweza kukupa watu wengi karibu yako, lakini historia yako ndiyo itakuonyesha nani alikuwa pamoja nawe wakati wa struggles zako.

Walikuwa wanapelekeana moto...Binti biKra zote Mbili hana, lakini bado tunaoa...tumekuwa kama mazezeta
 
1994 hiyo baba.. Nimetoka chuo niko mtaani ajira hakuna.. Nikaingia kwenye kubeba zege mzee acha kabisa.. Ujira buku

Nakumbuka siku moja nimepigika sina hata mia.. Mchana ulipita wima usiku nao ukaiga kwa mchana🙌🏿🙌🏿
Nikalala bila kitu tumboni na siku nzima nimepigika kwenye zege..! Kufika nane usiku nikajiona kabisa nazimia.. Ikabidi nifyonze colgate na kumeza cafenol 2 ili walau tumbo lipate kitu litulie..
Ankal mafix 😹

Kiranga wewe 1994 ulikua wapi?
 
Back
Top Bottom