Ndugu zako walitaka upate elimu ili ikusaidie kuchunga n'gombe zao?!mimi siyo tajiri ila nina hela ya kula. wakati nateseka, ndugu zangu upande wa baba walitaka nisome nikachunge ng'ombe zao. nikasoma kwa shida sana. kwa sasa naona wanajipendekeza hapa nawachora tu
Kumbe kuna gazeti liliitwa kasheshe lol 😆Unalikumbuka hilo Gazeti ? Au Gen Z hamjui kuna gazeti lilikuwa linaitwa Kasheshe ?
Sawa mhengaSanifu pia
ShikamoooNipe shikamoo yangu 😃
Ndugu zangu wanaume, wakati mwingine lazima ujiulize: 🤔
Huu upendo ulikuwa wapi wakati nilikuwa nashindia mihogo na kunywa maji?” 😂
Ulihangaika peke yako, ulijijenga kutoka sifuri, halafu ulipofanikiwa/unapofanikiwa ghafla watu wanaanza kujifanya walikuwa sehemu ya mafanikio yako.
Chagueni watu mnaowazunguka kwa umakini. Si kila anayeshangilia mafanikio yako alishiriki katika safari yako.
Wakati wa shida, wengi watakutazama ukianguka. Wakati wa mafanikio, wengi watataka kusimama karibu na wewe.
Usisahau waliokushika mkono wakati hukuwa na kitu cha kuwapa.
Heshimu waliokuamini kabla dunia haijaanza kukuamini. Na zaidi ya yote, usiruhusu mafanikio yakufanye usahau ulipotoka.
Kwa sababu utajiri unaweza kukupa watu wengi karibu yako, lakini historia yako ndiyo itakuonyesha nani alikuwa pamoja nawe wakati wa struggles zako.
Sijambo kabisaMarahaba hujambo binti mremboo
Done ✔️ brother 🔥Chukua fanta kwa mangi hapo halafu nitumie lipa namba
Ankal mafix 😹1994 hiyo baba.. Nimetoka chuo niko mtaani ajira hakuna.. Nikaingia kwenye kubeba zege mzee acha kabisa.. Ujira buku
Nakumbuka siku moja nimepigika sina hata mia.. Mchana ulipita wima usiku nao ukaiga kwa mchana🙌🏿🙌🏿
Nikalala bila kitu tumboni na siku nzima nimepigika kwenye zege..! Kufika nane usiku nikajiona kabisa nazimia.. Ikabidi nifyonze colgate na kumeza cafenol 2 ili walau tumbo lipate kitu litulie..
Trust me ankal sio fix na sio mara ya kwanza kusimulia hii habari hapa JF
Hapo kwenye kufyonza Colgate ndipo fix zilipo..!!Trust me ankal sio fix na sio mara ya kwanza kusimulia hii habari hapa JF
Mungu shahidi nilifanya hivyo.. Ule msemo wa adui yako muombee njaa una maana kubwa sanaHapo kwenye kufyonza Colgate ndipo fix zilipo..!!