Ulipokuwa unashindia Mihogo na Kunywa Maji, walikuwa wapi?

Mungu shahidi nilifanya hivyo.. Ule msemo wa adui yako muombee njaa una maana kubwa sana
Baada ya vita ya Kagera kuisha Tanzania tuliingia kwenye njaa kubwa mpaka rafiki wa Nyerere Rais wa Marekani Kennedy i think alimpa Nyerere msaada wa maindi ya njano.

Mimi siyo Mpare ila bibi yangu Mzaa mama sijui hata alifikaje upareni basi nilikuwa kwa Bibi uko nyumba ya Mungu nikiwa mdogo, siwezi kusahau ile njaa mlo mmoja kwa siku ugali na samaki wa kubanika na chumvi hapo siku hiyo ndio bonge la menu, nikikumbuka kwetu Dar kwa wazazi wangu maisha yalikuwa mazuri aisee mpaka leo mtu akiniambia hajakula siwezi kumnyima pesa ya kununuwa chakula.
 
Mimi siyo Mpare ila bibi yangu Mzaa mama sijui hata alifikaje upareni basi nilikuwa kwa Bibi uko nyumba ya Mungu nikiwa mdogo, siwezi kusahau ile njaa mlo mmoja kwa siku na samaki wa kubanika na chumvi hapo siku hiyo ndio bonge la menu,๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
mimi siyo tajiri ila nina hela ya kula. wakati nateseka, ndugu zangu upande wa baba walitaka nisome nikachunge ng'ombe zao. nikasoma kwa shida sana. kwa sasa naona wanajipendekeza hapa nawachora tu
Bila sisi ndugu wa baba usingetoboa wewe, masimango na mateso kutoka kwetu yaheshimu sana
 
Vizuri sana mkuu umenena tena kwa uchungu sanaa
 
Mkuu mwaka 1994 Ujira wa buku ulikuwa kwa mwezi au kwa siku?
 
Hakuna raha kama Mungu akikupa uwezo halafu kumsaidia anaehitaji kusaidiwa,tena kama yupo aliekufanyia ubaya ni raha zaidi kwani unamfundisha kuwa mtu mwema. Kuwa na uwezo na husaidii wanaohitaji kusaidiwa bule kabisa.
 
Pole sana kwa Kadhia hiyo ndugu Mshana.

Maisha hutupa pigo ambalo linaweza kukuamsha kwa namna ya kuona mambo kwa jinsi yalivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ