Ulipokuwa unashindia Mihogo na Kunywa Maji, walikuwa wapi?

Pole sana mkuu.
 
Kwa sababu utajiri unaweza kukupa watu wengi karibu yako, lakini historia yako ndiyo itakuonyesha nani alikuwa pamoja nawe wakati wa struggles zako.
Kuna kitu umekisahau naomba niongezee maana hata mimi nimejifunza.

Ipo hivi;

Unapoianza safari ya mafanikio unakua na watu wengi wengi sana waliopembeni yako wengine wakiwa wanakushangilia wewe na mafanikio yako na wengine wakiwa wanakuongoza njia ya kupita pita huku pita hivi na huku usipite.

Sasa hapo katikati ya hao watu kuna kundi kuubwa la watu wanaoitwa wanafiki, unajua mnafiki anakuaje? Ni mtu ambae wewe unapokua umefanikiwa anapenda kua karibu na wewe yaan atajiweka karibu ili aonekane na yeye yupo kwenye nafasi ya watu waliofanikiwa.

Sasa ikitokea wakati fulani ukaanza kuanguka yaan mafanikio yako yakaanza kuyumba hili kundi kubwa la wanafiki ndio kundi la kwanza kukukimbia na kukuacha peke yako. Na usichokijua hawa wanafiki ndio kundi kubwa kwenye circle ya waliofanikiwa, waongoza njia ni kundi dogo sana na hawa hua hawakimbii hata ukianza kuyumba kwenye mafanikio yako watabakia na wewe na watakuongoza ni jinsi gani unaweza kusimama tena baada ya kuanguka.

Waongoza njia ni wale watu ambao akishapanda na ngazi kufika juu anapofika juu haitupi ngazi chini kuzuia na wengine wasipande bali uiacha ngazi km ilivyo na kuruhusu wengine wapande na wanapokaribia kufika juu wanawashika mkono na kuwavuta juu ili wafike pale yeye alipofika.

Nimeongezea uliposahau kuongezea.
 
1994 umalize chuo ukose ajira ukabebe zege
kipindi hicho waajiri wanakuja chuoni mapema
Hapo katupiga, wakati kipindi iko babu yangu kaajiriwa anatamba na diploma yake ya IDM Mzumbe..

Alikuwa msomi wa ukoo..!! 😹
 
Sasa wewe huna hela unataka ukaoe mtoto wa watu ukamlishe nini? Haya tufanye huyo ni mtu mzima anaweza kapambana pia...watoto watakaozaliwa?
 
Sasa mbona umewaandikia wanaume tu?
 
mimi siyo tajiri ila nina hela ya kula. wakati nateseka, ndugu zangu upande wa baba walitaka nisisome nikachunge ng'ombe zao. nikasoma kwa shida sana. kwa sasa naona wanajipendekeza hapa nawachora tu
Halafu sijui kwa nini, ndugu wa upande wa Baba wanakuwaga ndio wajinga wajinga, wenye roho mbaya na chuki.

Hata kwetu sisi, ndugu wa upande wa Baba ndio wajinga, maskini choka mbaya, mashangazi yenye husda na chuki.

Lakini upande wa Mama, wajomba wako vizuri financially.

Upande wa Baba sijui kunawaga na shida gani?
 
sina uhakika lakini mimi baba yangu alifariki mapema na aliyepaswa kubeba majukumu ya kulea watoto wa kaka yao ni baba mdogo. ndiye aliyerithi mali za marehemu baba lakini akagoma kunisomesha
 
Wewe unaweza piga mwanamke risasi
 
Sasa wewe huna hela unataka ukaoe mtoto wa watu ukamlishe nini? Haya tufanye huyo ni mtu mzima anaweza kapambana pia...watoto watakaozaliwa?
Kwahiyo yeye anasubiri wewe umtafutie! Hawezi kuungana na wewe kwenye kutafuta?

Wakati huuna, basi kwake si kitu. Siku ukipata anajirudisha. Vipi siku ukianguka tena?

Vijana wa kuime sahivi naona wanajiongeza wanasema "hakikisha unaoa mwanamke anayejiweza, sio anayekuja kuwa mzigo kwako"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…