Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Mwana dada hakikisha unatoka na pesa au card ya bank katika matembezi yako muhimu.

Bora ni sahau simu lakin ni card ya bank wala pesa Kwa mkono.veri simpo
Hapa ninakupinga Chakorii.
Unataka kusema wasio na pesa wasiitikie wito?
Jambo la muhimu nashauri kabla hujaitikia wito hakikisha;
1. Unajua fika unatolewa out kwa minajili gani?...hoji kila kitu usiende kikondoo

2. Ujifika pia usifakamia hasa ikiwa ni out ya kwanza na huyo mtu.
 
Na hivi ndivyo inavyotakiwa mwanamke uwe.tena ingewezekana na bill yake ungemlipia kabisa..shwaini
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]alikunywa soda enzi zile 250 nakumbuka Mpk hapo hajaniongelesha Tena ujinga wake,hakuna kitu kibaya km kutoka huna pesa najitahidi Nile kwa mfuko wangu ulivyo
 
Hapa ninakupinga Chakorii.
Unataka kusema wasio na pesa wasiitikie wito?
Jambo la muhimu nashauri kabla hujaitikia wito hakikisha;
1. Unajua fika unatolewa out kwa minajili gani?...hoji kila kitu usiende kikondoo

2. Ujifika pia usifakamia hasa ikiwa ni out ya kwanza na huyo mtu.
Sasa kama anaekutoa out ni mtu unaemwamini halafu anaenda kukutelekezea bill nini maana Yake?hivi utatolewaje out jaman ushindwe hata kumtip waiter kisa hulipii bill wewe🤓🤓hapan.

Mwanamke beba pesa yako ya akiba fulstop
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aisee ulimuweza jamaa itakuwa hakukutafuta tenaaa aisee..
[emoji3][emoji16][emoji16]aliniheshimu na ujinga ujinga wake aliacha kwangu [emoji1][emoji1][emoji1]!!!!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Alijiandaa kulipa bill ya soda tu....

Kuna jamaa aliwahi kuandika eti ye hachezei hela akiita demu out ni glass moja ya juice na mirija miwili nilicheka jamani [emoji1787][emoji1787]
[emoji1][emoji16][emoji16][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3]juice mnakunywa wote kaaahhh
Sasa enzi red bull ndo habari ya mjini
 
Mwaka umekuwa na mambo mengi sana, tupunguze stress kidogo.....Ulishawahi kupata aibu hii?

Miaka ya nyuma kidogo nikiwa bado mwanafunzi form 4 nadhani kuna jibaba enzi hizo buzi, likanipa mistari na kuniita mahali jioni, nikajisema si kula tu??? Naenda mie...mida imefika nikachukua simu ya sister nikampigia na kumtaarifu nakuja ila nakuja na sister angu akasema hamna shida njooni.

Haooo tukatinga na viatu virefu jamani halafu mfukoni hatuna hata sh 100, tax tumechukua akaenda kulipa, tukaagiza kitimoto kg 2 na vinywaji, pale mezani yupo na wenzie wanne wakati tunawait msosi uje yule dingi akaanza kunishika shika basi nikawa namind namwambia nipo na sista angu usinishike tuongee tu, akafanya hivo kama mara tatu mi nakataa....bwanaweeeehhh eti akamind akaanza kunifokea na hakuishia hapo akatufukuza bila hata nauli😂😂 vinywaji hatujamaliza wala kitimoto haijafika....ana dhambi yule fala 😁

Hapo mida kama ya saa mbili hivi tukaanza kutembea kwa miguu kutokea kona ya Bwiru hadi mitaa ya rufiji nyie! nyie! tumeomba lift kwenye daladala wapiii tumenyimwa tukavua na viatu tukakanyaga peku moja mbili hadi home make miguu ishachoka ...huwa nacheka nikikumbuka huo mtoko.

Nimemkumbuka hili tukio baada ya kisa kilichotokea juzi, nilikua mitaa flani naendelea kuukaribisha mwaka, meza ya pembeni akaja demu mkare akaagiza wine akaanza kuipiga ile kunywa kulamba mwendo wa kumsubiria sponsor aje, baada ya muda jamaa akatimba, jamaa mapepe hata haendani na yule demu kwakweli japo hayanihusu 😁

Dem kuona mlipa bill kaja akaongeza na spidi na akachangamka, mara ikaagizwa chupa ya pili, jamaa anaagiza Heineken zake pale anapiga na watu offer....imefika saa nne akatoka kama anaenda kuongea na simu daaahhh mtoto kaachiwa bill pale ilibidi aache simu

Epuka aibu, beba pesa yako, happy new year familia
Nilikwambia tutoke ujue Nina pesa ya kutosha yaani apo everything upon me kula kunywa na ganja tutachoma🔥🔥
 
Mwaka 2007 kwenye mambo ya ujana siku moja tukatoka na washikaji kwenda kunywa. Utaratibu ilikuwa tukishakunywa bili ikija tunagawana au kama kuna aliyetoa ofa ya siku analipa yeye.
Basi siku hiyo tumekunywa ikafika mida ya saa 5 isiku jamaa wakaitana kama wanazungumza pembeni kumbe ndio wameniachia bili.
Nilistukia mchezo nikawaonesha umafia, walipofika nyumbani wakakuta mimi nimefika kabla yao na nimelala.
Bahati nzuri zaidi mtaa tuliokimbia ndio walipokuwa wanafanyia kazi hivyo wanajulikana zaidi yangu.
Sijui kama walilipa maana ndio ilikuwa mara ya mwisho kutoka nao out.
Wewe kweli ni mafia[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom