Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Mwaka 2014 nilienda singida kutembea tu. Nilikua na jamaa yangu namkubali sana ni rafiki toka chuo mpka leo mwamba alinikaribisha tena singida vizuri basi nikamjuza nimekuja kutembea siku kadhaa nimepakumbuka singida.
Mwamba akanipa na usafiri yeye akienda harakati zake na mimi nisiwe kinyonge basi jioni moja nikaenda singidani kuna hoteli inaitwa khb (katala beach hotel) kwa kipindi hicho ilikua inabamba pembeni kule ilikua inaporomoshwa regency hotel basi nikapiga kinywaji changu nikimsubiri mtoto mzuri.

Alipofika akaagiza kuku wine na alikuja na wenzake wawili wakati mimi nilimpanga siko njema mfukoni njoo mwenyewe tule goodtime na ukwel sio kwamba nilikua vibaya hapana ila nilitaka aje pekeake ili niwe huru na yeye bas akanisaliti kaja na wenzake tena wawili.

Mmoja kati ya wale rafiki zake nilishakula sana kipindi nipo chuo na yeye alikua anauza duka la nguo mjini (razack) kama sijakosea. Basi nilipoona kanisaliti na mimi nikaamua kuua kwa upanga nimeagiza vitu wamekula nikaanzisha stor na yule demu nayeye alikua ananikumbuka vizur nikatega kaenda chooni na mimi nikasubiri muda anarudi nikutane nae njiani basi ikawa hivyo nikampanga nikamwambia akifika mezani aseme hayuko njema aniombe nimpeleke home dem bila kuchomoa akakubali.

Basi ile narudi dem kaanza kutapika basi nikamchukua yeye na yule mwenzake nikawambia nyie mrudi home yule dem wangu nikamwambia agiza endelea nakuja.

Tulipopanda gari wakaangua kicheko wakimcheka yule dem wangu kwamba ni mshamba nikawapa stor yote nimempanga siko njema ila yeye kataka sifa kawaleta alaf hajajua kaniletea dem ninaempenda zaidi yake basi tukabadili kiwanja tukapoa rafiki resort mpka usiku tukamrudisha rafiki home nikabaki na dem wa zamani tukarud home na sikujuaga kwaamba yule mlupo tuliemtoroka alilipaje vile vitu.
 
Mwaka umekuwa na mambo mengi sana, tupunguze stress kidogo.....Ulishawahi kupata aibu hii?

Miaka ya nyuma kidogo nikiwa bado mwanafunzi form 4 nadhani kuna jibaba enzi hizo buzi, likanipa mistari na kuniita mahali jioni, nikajisema si kula tu??? Naenda mie...mida imefika nikachukua simu ya sister nikampigia na kumtaarifu nakuja ila nakuja na sister angu akasema hamna shida njooni.

Haooo tukatinga na viatu virefu jamani halafu mfukoni hatuna hata sh 100, tax tumechukua akaenda kulipa, tukaagiza kitimoto kg 2 na vinywaji, pale mezani yupo na wenzie wanne wakati tunawait msosi uje yule dingi akaanza kunishika shika basi nikawa namind namwambia nipo na sista angu usinishike tuongee tu, akafanya hivo kama mara tatu mi nakataa....bwanaweeeehhh eti akamind akaanza kunifokea na hakuishia hapo akatufukuza bila hata nauli😂😂 vinywaji hatujamaliza wala kitimoto haijafika....ana dhambi yule fala 😁

Hapo mida kama ya saa mbili hivi tukaanza kutembea kwa miguu kutokea kona ya Bwiru hadi mitaa ya rufiji nyie! nyie! tumeomba lift kwenye daladala wapiii tumenyimwa tukavua na viatu tukakanyaga peku moja mbili hadi home make miguu ishachoka ...huwa nacheka nikikumbuka huo mtoko.

Nimemkumbuka hili tukio baada ya kisa kilichotokea juzi, nilikua mitaa flani naendelea kuukaribisha mwaka, meza ya pembeni akaja demu mkare akaagiza wine akaanza kuipiga ile kunywa kulamba mwendo wa kumsubiria sponsor aje, baada ya muda jamaa akatimba, jamaa mapepe hata haendani na yule demu kwakweli japo hayanihusu 😁

Dem kuona mlipa bill kaja akaongeza na spidi na akachangamka, mara ikaagizwa chupa ya pili, jamaa anaagiza Heineken zake pale anapiga na watu offer....imefika saa nne akatoka kama anaenda kuongea na simu daaahhh mtoto kaachiwa bill pale ilibidi aache simu

Epuka aibu, beba pesa yako, happy new year familia
kona ya bwiru hadi mitaa ya rufiji si mbali kivivyo unavyopaelezea aisee
dakika kumi unafika
 
Hapo ukisoma km zishafika 2m ila wanavyojua kuzirudisha utakuta inasoma 45000km 😂😂😂😂😂
🤣🤣🤣🤣tena bora angekuwa anacheza na vichalii.yeye alikuwa ana penda baba zake🤣🤣unakuta alikuwa namiaka17 shimo lamiaka40
 
Me kuna kidem cha chuo nilikuwa nachart nacho mpk tukawa wapenz kwa kuchart
1st date nikakapeleka Hyat packing kabla hatujashuka nakavuta tukis kanagoma
Tukaenda kule juu tukaagiza msosi kula tunapiga story kananiletea ooh me na boy wangu na tunapendana siwez msaliti
Kumuuliza we si tumechart mpk umenikubali "oooh yes but but but zikawa nyingi niliamka pale nikaondoka kanashangaa
Nikabadili kiwanja nikaenda sehem nyingine nikaagiza msosi nikaanza kula nisepe home
Alipiga sm yule dogo alilia nikamuonea huruma nikarud nikalipia na kumwonya " hapa ni mjini sio huko kwenu sombanyasoko ukiamua kula cha mtu uwe tayali kuliwa "
[emoji23]
 
🤣🤣🤣🤣tena bora angekuwa anacheza na vichalii.yeye alikuwa ana penda baba zake🤣🤣unakuta alikuwa namiaka17 shimo lamiaka40
😂😂😂 Hawa wanawake kungekua na kipimo cha mashine imeliwa mara ngapi dah leo ni aibu tu
 
Hata mimi ningekufukuza kunikatalia kukushika sehemu zako nyeti,wakati nasubiri kula papuchi kunakuwa na kushikwashikwa mapaja na huko kwingine
 
Nimecheka kwa nguvu jamani, mimi ilinitokea ila na boyfriend kipindi nasoma chuo, tupo kariakoo akaniambia twende tukale kuna sehemu wanachomba mbuzi, kuku nk.

Basi nikaagiza chips, potion ya mbuzi na juice yeye akaagiza wali samaki na juice hee kumbe hana hata hela mfukoni, bili imekuja ananiambia nilipe mimi yeye hela hana nikamwambia sina ila mwishowe nililipa tuu aisee nilinuna ile siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂 ukaubeba, huyo ndio shemeji yetu hadi sasa au
 
Pole sana kwa matembezi ya lazima 😂😂

Ilishanitokea ila nashukuru Mungu nilikua na kiasi mfukoni vinginevyo ingekuwa fedhea sana.
NB: Unapokutana na old friend ambae mmepotezana mda mrefu usimuamini sana, kaa kijanja watu wanabadilika sana.
Mimi huwa siendi sehemu bila hela au card ya benk maana watu sio siku hizi. Mambo ya kutiana aibu sitaki wakati nina uwezo wa kulipa.
 
Mwaka 2007 kwenye mambo ya ujana siku moja tukatoka na washikaji kwenda kunywa. Utaratibu ilikuwa tukishakunywa bili ikija tunagawana au kama kuna aliyetoa ofa ya siku analipa yeye.
Basi siku hiyo tumekunywa ikafika mida ya saa 5 isiku jamaa wakaitana kama wanazungumza pembeni kumbe ndio wameniachia bili.
Nilistukia mchezo nikawaonesha umafia, walipofika nyumbani wakakuta mimi nimefika kabla yao na nimelala.
Bahati nzuri zaidi mtaa tuliokimbia ndio walipokuwa wanafanyia kazi hivyo wanajulikana zaidi yangu.
Sijui kama walilipa maana ndio ilikuwa mara ya mwisho kutoka nao out.
 
Back
Top Bottom