Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Ulishawahi kukimbiwa na kuachiwa bili mezani? Ilikuaje?

Mwaka umekuwa na mambo mengi sana, tupunguze stress kidogo.....Ulishawahi kupata aibu hii?

Miaka ya nyuma kidogo nikiwa bado mwanafunzi form 4 nadhani kuna jibaba enzi hizo buzi, likanipa mistari na kuniita mahali jioni, nikajisema si kula tu??? Naenda mie...mida imefika nikachukua simu ya sister nikampigia na kumtaarifu nakuja ila nakuja na sister angu akasema hamna shida njooni.

Haooo tukatinga na viatu virefu jamani halafu mfukoni hatuna hata sh 100, tax tumechukua akaenda kulipa, tukaagiza kitimoto kg 2 na vinywaji, pale mezani yupo na wenzie wanne wakati tunawait msosi uje yule dingi akaanza kunishika shika basi nikawa namind namwambia nipo na sista angu usinishike tuongee tu, akafanya hivo kama mara tatu mi nakataa....bwanaweeeehhh eti akamind akaanza kunifokea na hakuishia hapo akatufukuza bila hata nauli[emoji23][emoji23] vinywaji hatujamaliza wala kitimoto haijafika....ana dhambi yule fala [emoji16]

Hapo mida kama ya saa mbili hivi tukaanza kutembea kwa miguu kutokea kona ya Bwiru hadi mitaa ya rufiji nyie! nyie! tumeomba lift kwenye daladala wapiii tumenyimwa tukavua na viatu tukakanyaga peku moja mbili hadi home make miguu ishachoka ...huwa nacheka nikikumbuka huo mtoko.

Nimemkumbuka hili tukio baada ya kisa kilichotokea juzi, nilikua mitaa flani naendelea kuukaribisha mwaka, meza ya pembeni akaja demu mkare akaagiza wine akaanza kuipiga ile kunywa kulamba mwendo wa kumsubiria sponsor aje, baada ya muda jamaa akatimba, jamaa mapepe hata haendani na yule demu kwakweli japo hayanihusu [emoji16]

Dem kuona mlipa bill kaja akaongeza na spidi na akachangamka, mara ikaagizwa chupa ya pili, jamaa anaagiza Heineken zake pale anapiga na watu offer....imefika saa nne akatoka kama anaenda kuongea na simu daaahhh mtoto kaachiwa bill pale ilibidi aache simu

Epuka aibu, beba pesa yako, happy new year familia
Ww utakua ni kuruthum au tausi pale mitaa ya uswahilin rufiji.
 
Hii jeuri nzuri sana
Unafikiri hata ni jeuri basi…ni vile mtu hutaki nzi nyingi.

Sasa yanini mtu kukudharaulisha aise..ninacho ni mimi sina ni mimi usilete mbambamba.
Ni upuuzi tu
 
Hii ya majini ilishamkuta rafiki yangu mmoja mkurya kipindi tuko chuo. Alibeba demu walikutana bar akaenda naye lodge kufika ile wamevua nguo akaanza eti nataka nyama kama kapandwa maruhani. Wambura alitoka nduki suruali akalivalia mapokezi.

Hahhaaaa ni mbinu tu Za kuikataa mechi ukiona hauwezi kukimbia
 
Ziliwekwa bia tano nilivofikisha bia ya nne nikanywa nusu then nikazuga kwenda chooni nikatokomoa kusikojulikana, Alieniachia bill alikuwa jamaa yangu yaani mwenye utani wa ngumi. Uzuri niligundua mapema kuwa alinipa offer kiutani. Nampigia simu anasema waambie wakupe kazi ya kuosha glass

Mi Huo utani sitaki
 
Mkuu usichochee mgogoro kuwa mwanaume.
Huyo fala apenda utsni wa kitoto.
Usiniharibie amani yangu jioni hii
Okay, usikubali kutaniwa huo ujinga hata kwen mfano bora ukinukishe utakuja ombwa namba na mamende
 
Back
Top Bottom