Ulishawahi kukutana na mtu aliyevaa nguo zinazofanana na zako? How did you react to it?

Siku moja nilimuomba mkaka anisaidie kazi moja hivi akasema njoo mabibo. Nilikutana naye getini tukaingia wote ile kutembea kutoka getini nikaona watu wanatukodolea macho sana ila sikuwatilia maanani, ile tumefika tunakaa mwenzangu akasema hivi umegundua kuwa tumevaa sare? Ndio nikaona kumbe wote tumevaa juu nyekundu chini nyeusi... wakati wa kuondoka ilibidi ilibidi kila mtu aondoke kivyake maana nilijikuta nimepoteza kujiamini kabisa
 
Mie mwezi March nlikutana na mtu kavaa barakoa kama yangu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mimi nina kigari changu Ki Starlet cha kunivusha hapa na pale. Basi kila nikikutana na Ki starlet njiani lazima tupigiane honi nisipoanza mimi basi mwenzangu ataanza. Sijui hii ni kwa sisi wenye starlet tu au kwa wote!!
 

Cjui kwanini nimecheka sana 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mwaka jana nashuka lift pale jengo flani hivi hapa Dar. mara akaingia mdada ana kitenge same colour na shati nlilovaa ile tunakarbia kushuka rafiki yake akauliza "huyu ndie shemeji" yule dada aliishia kucheka ndio nikagundua kwanini ameulizwa vile. we were total strangers
 
Huwa tunachekeana😃
Being women; we sometimes hug kabisaa na kusema umependezaaa nyonyooo
 
Sikuivaa tena niligawa tangia siku hiyo sivai special ni mtumba tu.
 
mi nakutanaga na wana Yanga wenzangu tumevaa jezi za Gsm basi... nguo zingine hapana kwakweli
 
Kibongo bongo haya majezi ya simba na Yanga na timu za UK pia mashati ya kichina kawaida sana kukuta watu wamevaa sare
 
Siyo mavazi tu hata ukikutana na mtu ana drive gari kama lako unajikuta unamuwashia taa tu kumsalimia
 
GG and over2.5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…