Ulishawahi kukutana na mtu aliyevaa nguo zinazofanana na zako? How did you react to it?

Ulishawahi kukutana na mtu aliyevaa nguo zinazofanana na zako? How did you react to it?

Siku moja nilimuomba mkaka anisaidie kazi moja hivi akasema njoo mabibo. Nilikutana naye getini tukaingia wote ile kutembea kutoka getini nikaona watu wanatukodolea macho sana ila sikuwatilia maanani, ile tumefika tunakaa mwenzangu akasema hivi umegundua kuwa tumevaa sare? Ndio nikaona kumbe wote tumevaa juu nyekundu chini nyeusi... wakati wa kuondoka ilibidi ilibidi kila mtu aondoke kivyake maana nilijikuta nimepoteza kujiamini kabisa
 
Mie mwezi March nlikutana na mtu kavaa barakoa kama yangu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mimi nina kigari changu Ki Starlet cha kunivusha hapa na pale. Basi kila nikikutana na Ki starlet njiani lazima tupigiane honi nisipoanza mimi basi mwenzangu ataanza. Sijui hii ni kwa sisi wenye starlet tu au kwa wote!!
 
Niliibiwa nguo wakati nasoma chuo nilikua nakaa off-campus, kesho yake napita mitaa ya ubungo nikakutana na mtu kavaa jeans na shati kama langu, da ikabidi nimsogelee kwa ukaribu kuangalia vishikizo vya shati kwani kimoja kiling'oka nikashonea uzi wenye rangi tofauti, nikakuta ni lenyewe daah nikabaki nimesimama tu bila kujua pa kuanzia huku jamaa ndo huyo anakatiza Barabara.

Cjui kwanini nimecheka sana 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mwaka jana nashuka lift pale jengo flani hivi hapa Dar. mara akaingia mdada ana kitenge same colour na shati nlilovaa ile tunakarbia kushuka rafiki yake akauliza "huyu ndie shemeji" yule dada aliishia kucheka ndio nikagundua kwanini ameulizwa vile. we were total strangers
 
Huwa tunachekeana😃
Being women; we sometimes hug kabisaa na kusema umependezaaa nyonyooo
 
Sikuivaa tena niligawa tangia siku hiyo sivai special ni mtumba tu.
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya Cold War, jeshi na ujasusi wa KGB. Leo ngoja tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Eti ndugu zangu Watanzania;

HUMAN BEHAVIORAL PSYCHOLOGY.
============
Ulishawahi kukutana na mtu ghafla (kwenye sherehe, daladala au njiani) aliyevaa nguo zinazofanana na za kwako? How did you react to it? mlipungia mkono, mlipeana tabasamu, mlimfuata kumsalimia au ulikwepesha macho?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher
 
mi nakutanaga na wana Yanga wenzangu tumevaa jezi za Gsm basi... nguo zingine hapana kwakweli
 
Kibongo bongo haya majezi ya simba na Yanga na timu za UK pia mashati ya kichina kawaida sana kukuta watu wamevaa sare
 
Siyo mavazi tu hata ukikutana na mtu ana drive gari kama lako unajikuta unamuwashia taa tu kumsalimia
 
Kuna jamaa alinipa kaunda suti yake bure anayotokelezea ofisini akasema inambana. Siku mbili badae nikasikia kwa mshikaji eti jamaa kanipa suti baada ya kuniona eti nimevaa suti kama yake halafu nimekaa chini nasuka mkeka (nabeti). Jamaa hajui kama kazi yangu ni sawa tu na yake tofauti yeye anatumia elimu. Kwa hasira na mimi nikaigawa bure suti yake kwa muuza juice ya miwa. GG ikawa imetoa tayari.
GG and over2.5
 
Back
Top Bottom