kuna dem na dem ambae unamsaidia halafu kamani papuchu aje akupe yeye kwa hiyari yake.kuna mtoto mmoja nilishawai kumsaidia tu kwa nilichoweza kiasi cha kurisk vitu nilivyokua navyp geto lakini sikujali.
alikua mtoto flani aged kama 16yrs hivi.inavyoonekana alikua ametoka kwao(mkoani) kuja kutafuta kazi yoyote hapa mjini pasipo kumjua mtu yoyote(japo sina uhakika kama hakuwai kuishi dar kabla).
siku hio alifika kwenye nyumba ambayo kwa asilimia 99 tuliopanga ni vijana.alipofika akaanza kumuulizia mtu/jina la mtu ambae kwenye ile nyumba hatambuliki.basi mimi nkaenda zangu kazini ilikua shift ya mchana kwahio sikujua nini kiliendelea.
wakati narudi mida ya kama sa tano na nusu usiku namkuta yule dem amelala nje kajibanza kwenye kikolido flani na baadhi ya wapangaji ni wadada, walichomsaidia ni kumpa kanga tu yakujifunika(nadhani walihofia kulala na mtu ndani wasiomjua).mbu walikua wengi nkamuonea huruma.
nikamwambia twende ukalale chumbani kwangu alisitasita nkamlazimisha akakubali,na ni kweli yale mazingira alipolala yalikua magumu.tulipofika ndani nkawaza tulale wote nimle?
hapana huruma ilinijia kwa kuwaza kua huyu ana shida kwahio anaweza akaridhia kufanya chochote kwasababu tu hana namna,kwaio haitokua jambo jema kwa mtu unaejali ubinadamu.
kiukweli nilimwambia aende akaoge,akaenda akarudi nkampa chakula nilichokua nimepika akala.nikamwambia wewe sasa lala hapa mim naenda kulala chumba cha nyuma(kwa jamaa angu tunaefanya nae kazi).
basi na mimi nikala nikabadilisha nguo mbaka natoka mule ndani yule binti alikua ameshalala inaonekana alikua na usingizi sana.
kwa kuhofia kumsumbua ilinibidi nifunge mlango kwa nje,japo asubuhi yeye aliniambia ulidhani ntakuibia nikitoka(ilikua katika hali ya utani).
nashukuru kuna mdada mmoja anafanya kazi yakuuza chakula katika mgahawa wake akamchukua ili aanze kushinda nae na akampeleka awe analala kwa rafiki ake mtaa mwingine
sijajua mbaka sasa anaendeleaje kwasababu nilikuja kuhama mwezi mmoja baadae pale nilipokua kutokana na vibarua vyetu.