Sikia nikwambie sina shida ndgo ndgo wala kutaka attention ya watu nimeamua nishare story yang baada ya kusoma za wengine.
Wengi wanataka niendelee hvy ngoja niwape ubuyu
Brina achananna wahuni binafsi nataman usgushe mzigo mzima.usisahau kutuambia mafanikio ulopata. Ila kama wewe ndo ulikuwa na product ya pilipili please please chonde chonde njoo pm,

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka tu nimefika alinihug nikaanza kulia akawa ananibembeleza.
Hii ilikua fiction nzuri ila umeanza kuharibu kwa kuingiza uHINDI,

Na wewe ni mwanaume possibly shoga, tumesomea Cuba sie tunajua jinsia kutokana na mwandiko

Lakini endelea na story, ni nzuri inavutia endapo ukipunguza uHINDI na kuweka uhalisia
 
Basi ikapita siku 2 bila baba P kunitafuta wala sikuwa na wacwac coz nilimwelewa na ni kijana mstarabu mpole na alitokea kunikubali na kunielewa mapito yangu. Siku ya 3 akanitafuta akaniuliza upo nyumban nikamjibu ndio akasema anakuja ilikua kwenye mida ya saa 6 nikaenda kununua mboga nikampikia ugali samaki. Alifika saa 7 jamani alinisuprise hatar 😘😘😘😘 kaniletea tv frij sofa meza ya kioo zulia feni kabat la vyombo yan vilikua vingi vengine sikumbuki maana alikuja na kirikuu kimejaza. Tukavipanga ndani tukisaidiana na dereva walipomaliza nikawapa chakula walinisifia na kusema kweli japokua shule nilikua tia tia maji lakin mapishi nipo vizur maana kijijin nilikua naenda na bibi kupika kwenye shughuli za watu. Baada ya kula dereva aliindoka tukabaki na baba P akaniuliza mpango wangu ni nini kusema kweli mm wakat huo nilikua nawaza Kaz ya duka au za viwandani kwani dada Asha alinambia ataniunganishia Kaz ya kiwandan huku tegeta, uzuri sikuwa namficha kitu baba P akasema ni wazo zuri lakin yeye anaona wivu eti wataniiba πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nikamuuliza Kwan ww una mpango gan na mm wakat una familia yako akasema mm nimekupenda na siwez wala haitokaa tuachane ndio maana nafanya haya yote πŸ™„πŸ™„πŸ™„ heee nikasema kwa hiyo baba P kwisha habar yake.. hahaha bas nikamwambia niajiri kwenye biashara zako akaniuliza unajua nafanya biashara gani nikamwambia hapana ww hujapenda kuniambia akasema huwa anasupply vifaa vya umeme na spea za magari pikipiki na vitu kama hivyo kwa bei ya jumla bas nikapata picha ndio maana wana pesa na maisha mazur hivyo. Basi akanambia wiki inayofuata ataenda china kufata mzigo hivyo hatakua dar kwa wiki 2 hivi nikajibebisha pale kwamba nitammis na nn hao tukazama kwenye mechi mambo moto moto, ilivyofika saa 12 jioni aliniaga akanambia kwenye mfuko (ulikua na nguo zingine za ndani) Kuna zawad zako nikafurah nikamsindikiza nimerud nikafungua ule mfuko jaman kulikua na simu ya smart Samsung nilifurah sana nikampigia tukaongea sana karibu lisaa (alikua kwenye daladala anarud kwake) basi tukakubaliana nisiwe namtafuta Hadi yeye anitext au kunipigia nikakubali sababu nilishampenda.. Nilivyomamiliza nikaenda kwa Da asha kumsabahi bas akaniuliza kuhusu baba P akawa anamsifia alivyo handsome na anavyonijali mm natabasamu tu 😊😊 nikamwonyesha ile simu nikamwambia naomba unielekeze namna ya kutumia kuiwasha kumbe baba P kashanisetia Kila kitu isipokua tu nilifungua account ya Whatsapp na FB. Dada asha akawa ananidadisi huyo baba P ni nani na kwanini hakunitafutia nyumba mm nikajua tu mwenyew ile mwanzoni. Nikabid nimweleze ukweli sijui alinishawishi vp lakin nilijikuta nimemwambia Kila kitu had nililia akanipa pole. Tukaongea mengi akanishaur nisiogope mjin ndio maisha yalivyo na mimi nina bahat niitumie vizur ili baba P anifanyie mamb makubwa. Nikamwambia naogopa mme wa mtu lakin nimejikuta nampenda heeee si ndio akaanza kunifungukia yake kumbe na yeye kazaa na mme wa mtu na kiwanja ashamnunulia. Basi bint wa watu nikaanza kufundishwa maisha akasema baba P anakupenda mno na kadata sababu sio rahis from no where mtu akufanyie mamb makubwa hivyo. Akanishauri mbembeleze akufungulie biashara na jitahid umzalie ili iwe ngumu kuachana nae akununulie kiwanja na kukujengea kwani inaonesha ana pesa nyingi sana. Mimi huyo nikakubali na nikaona nimepata shoga wa maana ananifungia akili hao tukaenda kushangaa vitu alivyoniletea baba P.
Nikawa nipo tu nyumban wiki nyingine tena imeisha baba P akanitafuta Whatsapp video call tuliongea sana basi akaniambia unachagua kazi au biashara mm nikamwambia nataman biashara tena huku huku bunju akasema umefikiria vizur sababu nahofia nikikuweka kwenye biashara zangu mke wangu atajua itakua noma. Maisha yakaendelea ushosti na dada asha ndio ukaongezeka tukawa tunakula pamoja story kibao akaniambia nimepata nafasi ya Kaz kiwandan tuende nikamwambia hapana baba P kasema akirud ananifungulia biashara hvy kasema nitulie tu had arud na yeye akanishauri ni sawa usihangaike kuwa mpole tuone.
Wiki 2 zilipita baba P akarudi moja kwa moja alikuja kwangu ilikua ijumaa akanambia amemdanganya mke wake anarud jpli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ basi kipindi hicho nilikua danger na wala sikumwambia akaniuliza upo safe au tujikinge nikasema nipo poa usijali (niliamua kufanya hv sababu dada asha alinishaur nisichelewe hata akinichoka huwa wachaga hawatelekezi mtoto) basi siku hizo tatu mamb matamu tupo ndani tu pika pakua nikawa nambembeleza sasa kuhusu biashara, kipindi hicho uwakala ulikua vizur baba P akanishauri nitafute eneo ambapo naweza kuweka meza nikaanza kazi ya kutoa na kuweka pesa weeee nilimkumbatia kwa furaha jaman πŸ’‹πŸ’‹πŸ’‹ kisses kama zote. Nilikubali haraka hiyo biashara sababu nilikua nimefanya dukan kwa mama mdogo hvy uzoefu kidogo nilikua nao na kusema kweli bunju kipind hiko mawakala sio wengi sana.
Basi baba P akaniambia nitafute eneo niongee na dalali alaf yeye atashughulikia line tena alichukua hadi kitambulisho changu maana aliniambia kila kitu kitakua kwa majina Yang hvy nichangamke ili nijue nn naenda kufanya na baada ya siku 3 aliondoka na mimi huku nyuma nafanya mchakato na dada asha aliniongoza vizur tu.
Basi week inayofuata Baba P alinipigia akasema line zitachelewa mwezi unaweza upite mimi nikasema haina shida nitasubir sina pupa. Jpl jion dada asha akaniomba nimsimdikize vicoba njian akawa ananishaur jiunge ili uwe unawekeza pesa maana kushika hela mkononi haikai basi siku hiyo hiyo nikamwambia nipo tayar nikarud home chapu na boda nikachukua pesa tukaenda nikajiandikisha nikapewa fomu za kujaza na mamb mengne nikamalizia kesho yake. Alhamic asubuh kwenye saa 1 nimelala nasikia hodi kufungua ni Baba P huyo ndani kama kawaida mahaba moto moto.
Tumekunywa chai tukaoga akasema twende bagamoyo tukatembee maana unakaa mno ndani (kipind hiki nishaachana na majuba navaa napendeza nywele zangu nabana mitindo tofaut natumia vipodozi nimedamshi hatar mshaur mkubwa da asha kusema kweli alinitoa ushamba).
Tumefika bagamoyo tumeenjoy vya kutosha jioni akanidrop yy akaenda bunju ila tulikubaliana sababu yeye anasambaza spea za pikipoki na vifaa vya umem kwann tusitafute frem akawa ananipa mzigo nauza tunagawana faida na huo uwakala nikaendelea nao nikasema sawa haina shida nipo tayari. Basi akaniambia nisubir aweke mipango sawa nikakubali. Kuna siku da asha kaja kwangu nikawa namsimulia akaniambia kubali na usikatae nikamwambia nilishamkubalia hao tukaondoka tukaenda vicoba. Nilikua nanunua hisa zangu kila jpli. Tupo vicoba si Kuna mama akasema anauza kiplot chake kidgo Kipo karibu na barabar kina frem 1 ambayo haijamalizika. Watu wakamuuliza bei akasema anauza milion 5 mweny kutaka achukue no. Basi tukiwa tunarud si da asha akasema pambania shost ukichukue itakusaidia nikamwambia hela sina akacheka akasema unatembea na gar la bank πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ changamka nikasema hapana naogopa ataniona mdangaji akasema sasa Kwan hudangi na ni mume wa mtu. Nikamwelewa nikamwambia nimetunza milion 2 kwenye cm alibaki anashangaa tena akasema kumbe ww mjanja hvy nikamwambia ndio je nikiachwa sitak kupauka tena. Basi jioni hiyo Baba p akanipigia nikamwambia jinsi nimejiunga vicoba na kuhusu hiyo frem inauzwa akanisifu kuwa na akili ya maisha akaniambia nifatilie.
Nilichangamka kwa nguvu ya da asha akasema nichakarike kabla haijachukuliwa kwani ukiwa na frem ni rahisi kufanya biashara, tulimtafuta yule mama tukaelewana uzur alikua anapenda mabinti wanaojituma kumbe wenzake tunachunaaa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kesho yake nikampa taarifa Baba P nikamwambia ni pazuri tunaweza kuchukua na itakua rahis kuanza.
Basi haikuisha hata siku 3 Baba P akanitumia pesa M 5 cash Mimi weweeee mamb si ndio haya. Hao tukaenda kwa yule mama na dada asha, Baba P akanishaur namna ya kuandikishana na kumbuka Yule mama alimleta wakili tukauziana vizur alikua mama mwenye upendo na roho nzuri.
Basi weekend Baba P alikuja nikampeleka akapaona alifurah na kunisifu kweli akaniambia line zimeshatoka kwa majina yangu hivyo niende tra na serikali za mitaa nisajili biashara kwa majina yangu. Alafu atamalizia hiyo frem mapema tu maana ilikua ni umeme, mlango plasta na sakafu tu ndio hamna. Tukafanya yetu nikamdatisha Baba P wa watu nakumbuka alirud kwake saa 6 maana mtoto alikua anaumwa.
Kusema kweli nashukuru Mungu haikuchukua mda kila kitu kikakamilika mzigo wa spea za pikipiki na vifaa vya umem baadh vikaletwa na Baba p nikaanza kazi na tulitafuta fundi akawa anawatengenezea bodaboda pale pale na alikua ananifundisha baadh ya vifaa majina yake na kila kitu, alikua fund kijana tu na tulizoeana had akawa anashangaa na urembo wangu kwann nafanya biashara Ile nikamwambia baby wangu ndio kazi zake akawa anacheka.
Baba P aliniaga anpenda kufata mzigo China hvy atarud baada ya week 2 tena Ila tulikua tunawasiliana WhatsApp na pia nampa update kuhusu biashara na kweli ilienda vizur (ndani ya week mbili palichangamka kiasi) maana hiyo mitaa nilikua mm tu ndio nauza spea hvy nilijuana na bodaboda weng wakawa wanakuja.
Kimbembe kikaanza sion siku zang na nimepitiliza alaf nilikua mchovu mchovu na homaπŸ™„πŸ™„πŸ™„πŸ™„ nikabidi jioni wakat nimerud kazini niongee na dada asha yan wala hakuwaza akawa ananipa hongera tukaenda kupima kweli mimba ipo ya wiki 5 tukarud akanishaur nijitahid nianze kliniki ila aliniambia nisimwambia Baba p kwanza nisubir had arud.
Baada ya kama wiki 3 mbele ndio nilionana na Baba P akaja kwangu alikuja jpli basi nilimpikia nikampa mapenzi motomoto akaniuliza mbona Leo unanicare hvy had sitamani kuondoka nikachekaa. Imefika jioni akanipelekà mbeleni huko Kuna sehemu nzur kweli za keenjoy tumerud saa 3 nikawa nawaza namwambiaje kuhusu mimba nilikua na hofu had alinishtukia akaniuliza shida nn (tupo kwenye gari hapo) nikamwambia Nina mimba alishangaaa akasema kwann nimefanya uzembe kiasi hiko nikamwambia sikutegemea bahat mbaya kusema kweli alichukia akaanza kunilaumu nataka kuharibu ndoa yake wakat yeye kaamua kunisaidia tu Ili tufanye starehe nilichoka 😒😒😒😒 nikasema dada asha kaniponza mm nikatoka kwenye gar nalia na yeye akaondoka wala hakuingia ndani. Nimefika nikawa na mawazo tu hapo nilikua naangalia movie basi badae naona text zake anasema lazima tutoe hiyo mimba yeye hayupo tayar kuzaa nje ya ndoa. Mm sikumjibu chochote nikazima simu. Majuto yakaanza maana sikuwah kutoa mimba na ni kitu nilichokua naogopa Sana kwani cousin yangu alitoaga mimba akafariki akiwa chuo hivyo nafsi yangu ilikua inakataa kabisa!!!

Nitaendelea
 
Hii ilikua fiction nzuri ila umeanza kuharibu kwa kuingiza uHINDI,

Na wewe ni mwanaume possibly shoga, tumesomea Cuba sie tunajua jinsia kutokana na mwandiko

Lakini endelea na story, ni nzuri inavutia endapo ukipunguza uHINDI na kuweka uhalisia
Nikushangae na ushamba wako wa kisukuma mwenzio huyu Baba P kakulia nje ya nchi amerud huku tz ndio akaanza biashara hvy ana kauzung flan hv ndio aliyenifundisha kinge and he is so romantic n friendly sio kama wewe uliyakaza sura had ukazeeka πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sahv imekuwa kama ndo style mzee msela ana amua kutuletea chai ....... ilimradi ni story tu just tusome tuenjoy maisha ya endelee
Guys hamjalazimishwa kusoma and ukitak kuamini it's fine hutak utajua mwenyew but nimeamua nishare tu na wengi PM wananisumbua niendelee
 
Guys hamjalazimishwa kusoma and ukitak kuamini it's fine hutak utajua mwenyew but nimeamua nishare tu na wengi PM wananisumbua niendelee
Hata mmi nakishauri endelea wengine tunapenda story ..... iwe ya kweli au ya uwongo potelea pote
 
Sasa si unitaje tuu baba josefu unaniitaje Baba P

alafu sikukutoa kimaisha acha uongo
 
Usikaze kichwa mkuu legeza kidogo ubongo ulirelax mbona ameshaeleza kwamba alimpigia kwanza yeye..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…