Mzee wacha na mimi niilete hii!!
Kipindi niko o'level nilikuwa nikisoma Moshi ila kuna msala nilifanya shule ikabidi nihamishwe shule,so nikahamishiwa mkoani Iringa kwa uncle,ilikuwa shule ya day na mimi nlikuwa natokea home kwa uncle,basi bwana kama unavyojua shule za mikoani ukihamia mgeni shobo nyingi madem ata washkaji walikuwa wananikubali sana ukizingatia nilikuwa vizuri sana kwenye mathematics na football winga mmoja hatari sana!!
Basi kuna wana wakawa washkaji, hawa wana wapo 3 wamepanga geto moja kwa sababu kwao ni mbali na shule,na lile geto tulikuwa tukiliita "Old Trafford" mtu akiwa na demu anapeleka pale kutanfuna ila sheria ni moja "lazima aache wana tupige chabo"...
Basi kuna mwanetu akaopoa dem (wale wa kukosea namba)dem alikuwa na sauti nzuri balaa, hakuna aliyewahi kumuona huyo dem ni kuongea nae kwenye simu tu,siku hio jamaa akapanga na dem aibuke aje kumchek jamaa (dem alikuwa anatoka sehem moja panaitwa tanangozi),basi ikabidi tutoroke shule kwenda kumpokea huyu shemeji yetu maana kila mtu alikuwa na hamu sana ya kumuona kutokana na sauti yake kwenye simu!
Picha linaanza tupo stand pale dem kashuka kavaa tracksut(zile za wakuu wa mikoa wanavaaga jumamosi) dem mweusi tii,anachunusi kubwa hatari alafu zimeiva za njanoo mbaya kishenzi,jamaa akataka amkimbie tukampliz sio poa nenda tu, jamaa akamchukua dem mpaka mageton sisi tupo nyuma yao tunacheka balaa mpaka jamaa akaishiwa pozi, tumefika mageton makubaliano dem alale siku moja kesho arudi kwao,sisi tupo dirishan apo tunacheka hatari dem anamshika shika mwana, mwana kajikausha kama sio yeye, jamaa akawa anaombwa mchezo na dem jamaa hataki sisi huku tunacheka sana, tumekaa dirishani pale mpaka saa 7 hola tukasepa!!
Kesho yake ambayo dem ilibidi arudi kwao,dem hataki kwao kakaza palepale magetoni hataki kuondoka dem alikuja na viazi kibao kuja kuanza maisha na mwamba, ilibidi tuingilie kati tutumie nguvu dem asepe!
Sent using
Jamii Forums mobile app