Niliwafikisha wale samaki kwa ile familia na nikawahakikishia kuwa yule bwana yupo huko anapambana. Familia yake kwa maana ya wazazi wakamtuma mdogo wake amfuate akawa deported nyumbani.
Sasa yeye alikuta mambo yameharibika kidogo.
Ilikuwa hivi, wakati anaondoka kwanza hakuaga,akaenda mafia kulima nyanya,.kakaa miaka 2 huko bila mafanikio,akaamu kujichanganya kwenye samaki...basi akalowea huko. Kibaya zaidi wakati akiondoka alimuacha mkewe ana ujauzito wa kujifungua.Mke wake akajifungua salama huku baba na mama mkwe ndio wakimhudumia kwa kila kitu.
Baada ya miaka minne kupita bila taarifa ya jamaa yuko wapi,baba ake na mama yake wadhani kuwa huenda mwanao alishafariki au kuuwawa,waka mweleza binti akaolewe kokote maana yeye bado mdogo,kuendelea kumsubiria mtu asiyejua atarejea lini baba akaona sio busara,lakini yule binti akagoma kuondoka pale nyumbani,akidai kuwa yeye alishaolewa pale kwa hy niwa pale na hataondoka ataendelea kumsubiria jamaa hata kama ni miaka 30.
Sasa,kuna nyimbo fulani hivi za kilugha chetu wanawake huwa wanaziimba wakati wanafanya shughuli zao ndogondogo hapo nyumbani.Nyimbo hizo hubeba jumbe mbalimbali kama Upendo,majonzi msamaha, furaha ya kuwa na familia n.k. Sasa yule binti alikuwa akiimba nyimbo za kumiss mume wake na wakati mwigine alilia, baba mkwe hizo nyimbo zikawa zinamuumiza sana na kumtesa na kuumia,akawa anajihisi kuwa yeye ni mkosaji,labda mwanae hakumlea vyema katika maadili mazuri ndio maana kamkimbia mkewe.
Baba akaamua atafute mbinu ya angalau kumfariji mkwe. Akawaita wanawe wote wakiume pale nyumbani,akafanya nao kikao na kuwaomba kwamba waone namna gani wanaweza kumhudumia shemeji yao kimwili,wamtongoze wapambane hadi apatikane mshindi, atakayempata ndiye atakuwa mumewe kwa kipindi chote na kwa mahitaji ya mengine tofauti na ya kimwili familia itaendelea kutoa,yeye kazi yake ni kumgonga tu. Mshindi aliopatika......na ni mdogo mtu,yaani wanayefuatana na jamaa.Akawa anakula mzigo na yule binti akawa anapozea na kuponea hapo.
Sasa...ujio wangu na taarifa kuwa yule jamaa yupo Loya,kanipa na samaki hizi...kamongo wa kukaushwa na jua na kambale wa kukunja wa kukaushwa na moshi...na pesa kwa mke wake tsh elfu 70,walitaharuki....na mzee wake kwa maana ya baba akatokwa na machozi,mama huko sijui maana kimila sie huwa hatukai sehemu moja na wanawake.Mzee akamuru iuzwe ngombe pesa ipatikane jamaa aletwe hata kwa kufungwa kamba. Jamaa kweli akafuatwa akaletwa.
Anarudi nyumbani anamkuta mkewe mja mzito...ana mimba ya mdogo wake.!!! Usiku ulipoingia akagoma kwenda kulala kwa mkewe,akalala kwenye ghetto la wasioowa. Asubuhi kunakucha kikao cha ndugu kikakaa,kesi ikaendeshwa na jamaa akatiwa hatiani na ukoo kwa makosa takriban manne...mosi kuodoka nyumbani bila kuaga,pili kuondoka nyumbani bila kumuaga mkewe huku akitambua kuwa ni mja mzito..hivyo kuhatarisha maish yake na mtoto,tatu pamoja na kuondoka hakutoa taarifa yuko wapi baada ya kufika huko alikokwenda na nne kwa nini aligoma kwenda kulala kwa mke wake....
Kiufupi jamaa aliadhibiwa fimbo nyingi tu na akaambiwa akachunge mifugo miaka 2 na kunywesha, aombe msamaha kwa mke wake na waendelee kuishi...na ikawa ivyo.
Jamaa yupo kijijini kwao na alishakuwa na maisha mazuri tu na familia kubwa,mwanae yule wa mdogo wake alikuwa binti yupo sekondari na jamaa hana kinyongo na mdogo wake....nadhani alieleweshwa akaelewa...Upendo huvumilia yote.
Sent using
Jamii Forums mobile app