Mkuu nimejaribu ku-study visa ulivyo wahi kukumbana navyo ukiwa umekaa karibu na akina Dada, nikijaribu kueleza kisayansi ni kwamba: Sisi wanaume tuna kawaida ya ku-secrete/toa hormones aina ya Pheromones kwenye vikwapa vyetu na mwilini, hormones hizi hazina harufu yoyote lakini zina uwezo mkubwa wa kuhamusha hisia kali kwa akina mama, si rahisi wao kujua ni kitu gani kinamsukuma atake kufanya mambo ya ngono nawe - atafanya lolote body language-wise kukuhamasisha, kumbuka wakina dada wana mbinu nyingi sana - hii si adithi ya kutunga imekuwa proven kisayansi.
Inavyo elekea kuna wanaume wenye Pheromones kali sana kupita wenzao, wanaume wa aina hiyo ni rahisi kujikuta wanafanya mambo ya ngono na akina Dada wenye Chemistry inayo shabiana na ya kwako bila kujijua. Mimi binafsi nimewahi kuambiwa na baadhi ya akina mama wengi tu kwa nyakati tofauti kwamba, nikiwakaribia na kuwapa mkono kuwasalimia huwa wanajisihisi kusisimuka!! Hii haitokei kwa wanawake waswahili wenzangu tu bali hata Wazungu na Wachina waliwahi kuniambia hivyo!! Hapa nawambieni ukweli wa Mungu sitanii - sasa nikawa najiuliza maswali mengi: Mimi sio mganga wa kienyeji, mtume wala nabii!! Sasa ili suala la kusisimua wanawake kwa kuwashika mikono tukisalimiana linatokana na kitu gani hasa? Mtu aliye kuja kunipa kujibu kuhusu conundrum yangu alikuwa ni mwanafunzi mwenzangu wa kizungu - dada huyo ndiye alinieleza kuhusu maajabu ya hormone aina ya Pheromones.
Tukija kwa msichana aliye kumwagia chai, hiyo haikuwa bahati mbaya alikusudia baada ya kujaribu mbinu nyingi kwa muda mrefu mnapo baki peke yenu nyumbani lakini akaona ulikuwa hushtuki, mlipo baki peke yenu kwa mara nyingine tena akaona hiyo ni golden chance ya kutimiza dhamila zake: Kisa mwili wako unatoa Pheromones kali sasa afanyeje.