Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

Ulishawahi kulazwa kituo cha polisi na mkeo?

point 3 kwa katandoa.
Niliwekwa ndani na mke wangu baada ya mimi kugoma kutoa mchango wa kumdhamini kaka yake aliyekamatwa na pembe za ndovu.

Zilitakiwa milioni 5 kumdhamini kaka wa mke wangu, ndugu zake walijikusanya wakachanga milioni 3. Zile mbili zilizopungua mke wangu alikuja kuniomba nitoe hizo hela ili kukamilisha malipo ya dhamana.

Sikuwa na hiyo hela, nilimwambia wazi kuwa sina hela. Kilichotokea sasa baada ya kumwambia hivyo alinifokea kwa ukali akinituhumu kuwa nina roho mbaya na sipendi kusaidia ndugu zake Ila naweza kuhonga malaya tu huko mitaani.

Sikufurahishwa na hayo aliyoniambia so nilimfata na kumcharaza kwa vibao vitatu vya shavu ili kumshikisha adabu. Alipiga yowe la uchungu na kutoka baru akatokomea sijui wapi huko.

Baada ya kama lisaa limoja hivi nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni polisi akinitaka nifike kituoni, nilishangaa Ila niliitikia wito.

Nilipofika kituoni mshangao wangu ukawa mkubwa zaidi baada ya kumkuta mke wangu yupo hapo na alifika hapo kuripoti kuwa nimemshambulia kwa kukusudia. Nilishindwa kujitetea maana ni kweli nilimpa Kichapo.

Afande aliyeshughurikia hayo malalamiko ya mke wangu alisema hawezi kulimaliza hilo suala muda huo maana ilikuwa ni saa mbili usiku, atalishughurikia kesho yake asubuhi. Afande alimtaka mke wangu arudi nyumbani Ila mimi sikuruhusiwa kurudi nyumbani bali nilitakiwa kulala hapo kituoni.

Muda mfupi baada ya mke wangu kuondoka niliamriwa na afande wa zamu kuvua viatu na mkanda wa suruali kisha nikasukumwa kwenye kachumba kasiko na dirisha wala taa nikawa nimelala polisi kwa mara ya kwanza.

Nililala kwa usiku mmoja tu, asubuhi tuliyamaliza mambo ya kipolisi kishikaji nikaachiwa huru asubuhi hiyo.

Nikiwa na hasira kali sikurudi home niliamua tu kuachana na huyo mwanamke wa kinyiramba.

Tuliowahi kulazwa polisi na wake zetu tujuane hapa.
 
Huko kumalizana kishikaji,,ndio kumalizana gani??embu fafanua inaweza kuwa ni mbinu Bora ya kutumia endapo na Mimi huyu wangu naye akibahatika siku kunipeleka Kwa wafanyakazi wenzangu
Mkuu ni kweli nilikuwa na kosa ambapo kisheria nilipaswa kufikishwa mahakamani.

Afande alinifuata korokoroni alfajiri akanipa njia ya kujinasua kwenda mahakamani nayo ni kumpa 50k, nilimuelewa na ndivyo tulivyomalizana kishikaji kwa kumpa afande hiyo hela, sijui afande alivyomwambia mke wangu, Ila my wife aliniambia tu kuwa kafuta kesi hivyo twende nyumbani.

Hasira ilibaki kwangu niliyelala kituoni usiku mzima, sikuongozana naye kurudi nyumbani.
 
Kwenye heading nilielewa kwamba wewe na mkeo mlilala kituo cha polisi ila kumbe mkeo ndiye alikulaza kituoni.


Pole sana!

Ila huyo Mnyiramba achana naye jumla.

Kawaida mwanamke akishakupeleka polisi hapo hakuna mapenzi.

Kwanza anaweza akakuua!
 
Mimi mke wangu alichukua 3M ya biashara akamkopesha shoga yake anaedaiwa kwenye mikopo nyonya damu wakati shoga yake hana kazi yoyote itakayo msaidia kulipa hilo deni.
Ikabidi niende polisi mwenyewe nikawaambia polisi waniweke ndani maana nikibaki nje ntamuua wife.
 
Mkuu ni kweli nilikuwa na kosa ambapo kisheria nilipaswa kufikishwa mahakamani.

Afande alinifuata korokoroni alfajiri akanipa njia ya kujinasua kwenda mahakamani nayo ni kumpa 50k, nilimuelewa na ndivyo tulivyomalizana kishikaji kwa kumpa afande hiyo hela, sijui afande alivyomwambia mke wangu, Ila my wife aliniambia tu kuwa kafuta kesi hivyo twende nyumbani.

Hasira ilibaki kwangu niliyelala kituoni usiku mzima, sikuongozana naye kurudi nyumbani.
✊✊Usirudie tena Mke ni Wa Kwako,,lakini Binadamu ni wa Gavamenti Sawa!!
 
Back
Top Bottom