Kwenye heading nilielewa kwamba wewe na mkeo mlilala kituo cha polisi ila kumbe mkeo ndiye alikulaza kituoni.
Pole sana!
Ila huyo Mnyiramba achana naye jumla.
Kawaida mwanamke akishakupeleka polisi hapo hakuna mapenzi.
Kwanza anaweza akakuua!
Mimi kuna mmoja aliwahi nipeleke, nikaitwa dawati la jinsia, nikaenda.
Wakaanza ngonjera na vitisho kuwa nimempiga. Nikawaambia aeleze vizuri kosa ni lipi, aksema hakuwapikia watoto alikuwa anajisikia vibaya. Akaulizwa kama alitoa taarifa kwangu, akakataa.
Kimwanamke kimoja kikaanza, hata kama hakupikia watoto, huna haki ya kumpiga. Nikamuuliza unao ushahidi kama nimempiga, akasema mimi nimepokea malalamiko, nina uwezo wa kukuweka lockup. Nikamwambia, majadilianao yameishia hapa, nipelekeni mahakamani.
Basi wakachachamaa kuwa nina kiburi, watamsaidia mke wangu na watanipa fundisho, nikasema nasubiri. Kimbembe ikawa mke wangu hataki niwekwe lockup. Maana anajua jinsi nilivyokuwa na react sikuwa natania, ndoa ingeisha. Wakamwambia aandike maelezo, mimi nawekwa lockup then mahakamani. Wife akawajibu sina ushahidi mahakamani, na sitaki awekwe lockup maana hana kosa. 😂
Kilichoendelea ni yeye kukoswa kofi na kidada kimoja, eti unatusumbua. Kidogo akaja OCD akasikiliza marumbano, akawambia msizunje ndoa za watu, huyu dada anampenda mmewe, waacheni huru.
Kurudi home hana hata nauli, anatembea kwa miguu. Nikampa nauli ya daladala, nikapanda boda boda nikaondoka. Home nikawachukua watoto nikaondoka nao kwenda matembezi bila kumpa taarifa. Jioni hatukurudi, 😂😂 ngoja niishie hapa story ndefu na inachekesha mwishoni.