Mimi nilimchapa vibao mke wangu akiwa mjamzito kisa kunitukania mama yangu. Akaenda Polisi, wakanipigia simu, nikachukua zangu karatasi tatu na kalamu nikaandika taraka kabla sijafika kituoni. Nikabeba simu, hela kama fifte zile karatasi.
Kituoni nafika, nimesimama mbele ya meza, naulizwa wewe ndio flani, wewe unamjua huyu, sijajibu zunguka huku, kofi la mhongo, vua mkanda, kiatu, saa wakanitupa sero, nikakabidhi hela, simu na zile karatasi kwenye bahasha.
Mwanamke wakamwambia rudi nyumbani ilikuwa jioni mida ya saa 10 hivi.
Mida ya saa 12 jioni naitwa sero, kumbe mke wangu amekuja kuniletea chakula na amenisamehe eti niachiliwe kimemuuma.
Afande wa zamu akasema, mpaka aje afande alienipigia simu. Ex Wife akawaambia yameshaisha, waniachie. Wakamwambia wewe umeleta mambo polisi kuna utaratibu wake, ungekuwa unataka msamehe huyu bwana usingekuja huku. Huyu atalala ndani mpaka akamilishe dhamana. Wakanitupia tena sero, nikakataa kula nikamwambia Afande hicho chakula arudi nacho huyo mwanamke.
Yule mama akalia sana pale nje, wakamfukuza wakamwambia aje asubuhi. Mtoto wangu wa miaka miwili namsikia analia baba, baba, mi nipo sero.
Kukakucha, Akawahi sana yule mama saa 12, kaleta chai. Polisi wana utaratibu wao, wakachomoa watu wa kwenda mahakamani, badae saa mbili mbili mlango unafunguliwa naitwa mimi, nafika CRO chumba cha mashitaka nawakuta jamaa, washikaji, mshua na wafanyakazi wangu wamekuja kunichomoa.
Basi tukaitwa ofisini kwa mkuu wa kituo, Afande mmoja Mwanamke ndie akasikiliza ishu yetu. Nikaonywa sana kupiga mke, kwamba ni jinai na ile ishu ningefungwa kwa kujeruhi, mambo mengi niliambiwa pale kibabe sana na yule Maza afande.
Wakanirudisha chumba cha Mashitaka, chukua vitu vyako, anataka kunikabidhi zile karatasi nikamwambia mpe huyu ndio zake anafungua kusoma ni taraka, kilio kikubwa mno na kugalagala chini. Polisi wakamwambia kama amekupa taraka nenda mahakamani ili ukapate haki zako.
Wana wakanichukua, wakanipeleka gesti, nikaoga kutoa nuksi nikaletewa nguo zingine nikavaa.
Yule mama akanipeleka mahakamani, na mimi sikurudi home, napigiwa simu na Mwenyekiti kuna samansi ya mahakamani.
Nikaenda mahakamani nikakiri kumpa taraka yule mama, wakaainisha vitu vya ndoa. Nyumba ya ndoa na viwanja viwili. Mimi nikawaambia nyumba ya ndoa ibaki ya watoto, viwanja viwili nampa moja chake moja changu. Nilikuwa na pesa akiba kama 1.5 M nikawambia mahakama nampa laki 7 na vyombo vyote vya ndani aondoke navyo.
Nyumba ikapangishwa, pesa ya mtoto mdogo nikaambiwa nitalipa hamsini kila mwezi. Mtoto mkubwa akabaki shule. Kwisha.
Mali zote nilikuwa naandikisha kampuni ambayo aliikuta yule mama. Nikaokoa mali kibao kupigwa pasu. Gari, trekta, vyote alidai mahakamani vikaonekana ni vya kampuni ambayo kaikuta na nipo mimi, mzee na mdogo wangu hiyo ilikuwa 2019. Mwanamke alikomaa sana kila kitu kiuzwe, kumbe mimi nilikuwa nafanya biashara chini ya Kampuni. Mali zangu ukinitafuta mimi hunikuti unaikuta kampuni. Tukavutana sana mahakamani, ikaonekana nimemuoa kampuni kaikuta na hajawahi kuingizwa kwenye kampuni kwa hisa au kwa kufanya kazi. Ana kazi yake nina biashara zangu. Pia nilipeleka Usia na mirathi ya mama yangu ambae katika mgao wa mirathi ya mama ndipo tulikubaliana mimi, baba na wadogo zangu tufungue kampuni na yeye nikamuoa miaka 10 baadae.
Nikaokoa mali mzee, vinginevyo ilikuwa ni pasu kwa pasu. Chezea mwanamke akiwa mjinga ila akiwa anajitambua ni hatari sana mbele ya sheria jameni. Mwanamke aliweka mpaka wakili kutaka mali zile.
Pole sana Mzee mwenzangu. Mke mbele ya sheria achukuliwi kama mke wako anachukuliwa kama "Separate entity" yaani anakufunga laivu laivu. 😁