Sikurudi nyumbani kwa siku tatu.
Tulipokuwa tunakaa sio mbali na kwao, ni mji mmoja. Nikaamua kuwapeleka watoto kwa bibi yao (mama yake) lakini nikamsimulia kilichotokea na kumuomba asimwambie nataka kumfundisha tu asiwe anapenda kukimbilia polisi kwa tatizo dogo kama hilo. Mama akakubali (alikuwa ananipenda sana kama mkwe anaemjali) akawa anampigia simu mwanae kuhakikisha yuko salama (huruma ya mzazi) lakini hasemi chochote kuhusu watoto.
Baada ya siku 3 nikarudi home peke yangu, akauliza watoto nikamwambia siku ile ulivyoamua kuwaacha na njaa ulitegemea wanaangaliwa na nani? Nimeona huwajali nimewapeleka kituo cha watoto yatima😅. In short aliteseka sana mpaka kujua watoto walipo, maana polisi aliogopa kurudi tena, nyumbani kwao hakutaka kuwaeleza ukweli wa tukio maana ni aibu kwake na kwao nakubarika sana wangembadikikia wote.
NB: ukitaka kumaliza kiherehere cha mwanamke, waweke karibu ndugu zake, hasa mama. Automatically anakosa mtetezi kwao.